Balle de Match kutambulisha mpya ya JB Mpiana na Wenge BCBG

clip_image001

Sikiliza balaa la Genta Lisimo humu!!

Mwanamuziki JB Mpiana ambaye alifunga mwaka kama wenzie kwa kuzindua Single yake mpya ijulikanayo kama Balle de Match ambayo aliizindua huko Equatorial Guinea

Hii ilikuwa ni baada ya show ndefu ambazo alizifanya hapa nchini na huko Zambia ambako aliangusha show ya nguvu. Inasemekana kuwa hii ndio itafungulia ujio wa albamu yao mpya ambayo wanamuziki wengine nao wametunga nyimbo kadhaa ndani yake kama Zoule Atshuda alias na Diego Milito. Wimbo Balle de Match ni moto wa kuotea mbali kwani Genta Lisimo amefanya kufuru humo na kwa mara ya kwanza JB ameamua kutumia electric drums kit kwenye Sebene.

Ukisikia Solo lililopigwa humu ni lile Solo kali la Metre Ficare Mwamba akishirikiana na kijana mdogo anayekuja kwa kasi Djany Solo, baada ya Rotarota utamsikia kijana anaingia hapo anagonga mpaka mwisho tofauti na ulilozoea humu Solo limesikika barabara. Hii inaashiria moto uliopo kwenye albamu ya Mpiana ijayo.

Aidha Mpiana amesema kuwa ameichelewesha albamu yake ili kuzipisha albamu za wanamuziki wenzake ambazo nazo zimeingia sokoni kwa sasa, anasema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kwani mwisho wa siku mashabiki wanaonunua CD na DVD zao ni hao hao na wanahitaji muda kusikiliza nyimbo za mwanamuziki mmoja mmoja alisema Mpiana.

Advertisements

5 Responses to Balle de Match kutambulisha mpya ya JB Mpiana na Wenge BCBG

 1. Prince George says:

  7bu napenda muziki wa Congo pia nikiwa shabiki wa Quartier Latin,Lakini nawakubali sana JB MPIANA,WERRASON NGIAMA,FERRE GOLA,NA FALLY IPUPA napenda sana nyimbo zao kwa ujumla hata Album zao baadhi ninazo kwani ninapokuwa nime2lia nyumbani huangalia moja baada ya nyingine,lugha imekuwa ttz kuielewa lkn burudani naipata haswaa,tuko pamoja wadau

 2. Juma Hussein Kitine says:

  Solo la Maitre Ficare hapa ni la kawaida tu. Hapa Bongo kuna jamaa anaitwa Ephraim Joshua wa Exra Bongo ni mkali zaidi ya Ficare. Pia kuna Elombe Kichinja wa Academia naye ni moto wa kuotea mbali.

 3. Prince George says:

  Naona kaka juma umemdharau sana FICARE MWAMBA kwa upigaji wa Solo gitar kwani huo mtazamo wako siukubali kabisa pia mm sio mwana BCBG,nawaheshimu sana Elombee Kichinja”Papaa na Arafat na Ephraim Joshua na pia nakubali kazi yao,lakini nakataa mpe tu heshima yake Metre Ficare Mwamba.Ahsante

 4. Anonymous says:

  BCBG Blog. ziko news nyingi sana za music mnazipotezea kwa sababu ya upofu wenu kwa Mpiana, habari ya mjini sasa hivi ni satelite mwezi mmoja tangu kuzinduliwa ishatazamwa Yu tube na watu zaidi ya milioni moja.

 5. Wonderful facts, great and beneficial design and style, as share good stuff with superior thoughts and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: