The Kilimanjaro Connections Band yaendelea kutesa Kuala Lumpur Malaysia

251929_4163633330638_486942009_n

MBELE WAIMBAJI ALLY SAMA, DOTO RAMADHANI, NYUMA KANKU KELLY, SIJALI MORIS ( Drums), FARIALA MBUTU ( Bass), BEN OMAR ( Guitarist), DONALD ( Keyboard)

Unapokuwa nje ya nchi kila kitu cha nyumbani una kimiss hasa kwa wapenda Burudani inakuwa ni mtihani maana unakutana na burudani lakini katika utamaduni mwingine kabisa. Tangu kukua kwa uchumi wa nchi za Mashariki ya mbali kumefanya vijana wengi wa Kiafrika hasa kutoka Afrika ya Magharibi, kukimbilia nchi za Asia ambazo uchumi wake umekua kwa kiasi kikubwa,  moja ya nchi ambazo zinakimbiliwa ni Malaysia bila kusahau, Singapore, Vietnam, Hongkong na hata China.  Nchi hizi zinakimbiliwa sana na vijana hawa na kwa sasa kumekuwa pia na lindi la wanafunzi waotoka nchini Tanzania, kenya, Botswana, Zimbabwe na hata Sudani ambayo kwa watanzania wao hawako katika kutafuta maisha bali kutafuta elimu ambapo wengi wa wanafunzi wamekuwa wakikimbilia Malaysia kwa ajili ya elimu ya juu,

Iinakadiriwa kuwa Malaysia ina wanafunzi zaidi ya elfu hamsini wanatokea Afrika ambapo Tanzania pekeeina wanafunzi zaidi ya elfu kumi.  Chachu ya kuwepo kwa jumuiya hii ya Waafrika imepelekea wafanyabisahara wa Kimalay kuangalia ni jinsi gani wanaweza kujichanganya na kuangalia kuweza kuitumia jumuiya hii kibiashara, mmoja ya wafanyabiashara hao ni Mkurugenzi wa Club ya Rum Jungle ambayo ipo jijini Kuala Lumpur. Katika Club hii ndipo unaikuta bendi pekee iliyojizolea umaarufu si Malaysia pekee bali South East Asia bendi ya The Kilimanjaro Connection chini ya uongozi wake Le Gendary Kanku Kelly.

Bendi hii ambayo kwa takribani miaka zaidi ya kumi sasa imekuwa ikitoa burudani South East Asia huku miaka zaidi ya sita ikijikita jijini Kuala Lumpur imeweza kupeperusha vizuri bendera yetu na ni mahali si tu vijana wanakutana bali hata mabalozi wa kutoka nchi za Kiafrika na wanafamilia wao wamekuwa wakijumuika katika klabu hii ya Rum Jungle kupata vionjo na burudani ya nyumbani.

The Kilimanjaro Connections wamejikita kupiga muziki wa dunia nzima huku wakipiga nyimbo zote maarufu duniani na hata zile za Asia, za Kimalay na Kichina jambo linalowaongezea umaarufu na kugonjwa vichwa vya habari kula uchao. Miaka kama miwili iliyopita bendi hii nilipokutana nayo walikuwepo watu mahiri kama Maneno Uvuruge ambaye ni mcharaza gitaa maarufu ambaye binafsi nilianza kumsikia akivuma na vijana Jazz miaka hiyo nikiwa mdogo, pia kuna mtu kama Faliyala Mbutu ambaye ni mume wa ndoa wa Luiza Mbutu huyu jamaa anapiga gitaa la Bass na kiukweli namkubali sana, kuna Sijali Moris kwenye chants na Drums na kwenye Tumba, Pakacheni mzee mwenyewe Kanku Kelly.

kwa sasa Bendi hii imeongeza wanamuziki wengine wapya na line up nzima ni kama ifuatavyo, FALIJALA MBUTU (bass guitor), BEN OMARI ( guitar), SIJALI MORISI ( drums), DONALD ( keyboads) , DOTTO RAMADHANI ( Female singer), ALI SAMA ( male singer) na KANKU KELLY ( percussions& trumpet), ni timu ya watu saba ambao wanafanya kazi ya bendi ya watu 25 kwani wakiimba wimbo wa Wenge BCBG ambayo ni bendi ya watu 25 unapata kila kionjo!!

Kiukweli bendi hii inaburudisha sana na nawakubali sana binafsi, ni huku ndipo nilipomuona Queen Suzy kwa mara ya kwanza mwka 2006 ambapo Kilimanjaro Connections walikuwa wakitumbuiza Kuala Lumpur. Bendi hii imezidi kujizolea umaruufu kwani kwa sasa inapiga siku sita za wiki na kupumzika jumapili tuu hii ni kutokana na matakwa ya wadau na mashabiki wa bendi hii ambayo ina mkataba wa miezi sita kupiga katika Club hiyo kila mwaka, “Kiukweli tunashukuru jinsi tunavyopendwa hapa KL, mashabiki wanafanya mpaka tunakosa muda wa kupumzika sasa” alisema Kanku alipoongea na Spoti na Starehe.

Tunawatakia kila la heri katika shughuli zenu.

3 Responses to The Kilimanjaro Connections Band yaendelea kutesa Kuala Lumpur Malaysia

 1. Farid 4x4 says:

  Le grand Pius Mzee Tunashukuru sana kwa taarifa hizi , ila kitu kimoja tungeomba nyongeza , utupe adress au jina kamili la hotel na location yake pale KL.

 2. Farid 4x4 says:

  Huyo jamaa katika hio clip anaepiga guitar la solo ni balaa,
  aliwahi kua na sisi hapa Muscat , hatutamsahau kabisa na tunatamani arudi leo kabla ya kesho. sijaona mtanzania anakung’uta guitar kama huyu.

 3. Lashonda says:

  The show is loud and the arena is particularly dark for some performances,
  such as the trapeze acts and Globe of Steel.
  We purchased our tickets prior to the event and started planning our trip.

  The shops that are further from a tourist destination will usually have better prices.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: