JB Mpiana alivyochengusha Mwanza

Jb Mpiana ‘Mukulu’ aka Binadamu usiku huu ndani ya himaya ya Villa Park Mwanza anamwaga mvua ya burudani kwa wapenzi wa ngoma za bendi waliojitokeza hapa.

Simple and clean…kwa wadada wa safu ya unenguaji ya bendi ya Wenge BCBG chini yake Jb Mpiana.

Wadada wa mwanza hawajasita kumtunza mkali huyu wa ngoma za dance toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Danico ndiyo wimbo jukwaani sasa..


Mashabiki na mtu wao kiunganishi muziki…


Jb Mpiana ‘Mukulu’ aka Binadamu na safu yake ya masauti..


Wadau walioamua kuwekeza ndani ya usiku huu. 

Huku akipewa tafu na JB Mpiana ‘Mukulu’ aka Binadamu pamoja na rapa wa bendi hiyo, mwanamuziki H. Baba alifanya ile inayotakiwa kwenye jukwaa  kubwa sambamba na kundi la Wenge BCBG. 

Utamu unapokolea ‘tafu’ muhimu.


Ngoma ikiendelea stejini naye H. Baba akiendelea kumwaga sumu.

 

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania H. Baba mwishoni mwa wiki alifanya show ya live akiwa na bendi ya Wenge Muzika BCBG na kuwastaajabisha wengi akiwemo kiongozi wa bendi hiyo JB. Mpiana, kwa umahiri wa uchezaji wake, umiliki wa sauti, jukwaa na upangaji safu yake. 

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania H. Baba alitumia vipande vya rap zake kunyanyua hisia za mashabiki huku sebene la nguvu likiendelea kushushwa na wana Wenge BCBG nao marapa wa bendi hiyo wakifanya kolabo nae kupendezesha show ya ujio wa Wenge Musica jijini Mwanza ulioandaliwa na QS Mhonda J, na kudhaminiwa na kampuni ya kutengeneza vinywaji vikali ya K Vant Gin na TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager..

H. Baba akiimbisha wakati mmoja kati ya wacheza show wake ‘Dogo Poteza’ akikisanukisha.


Hapo jeh..!

Picha zote na GSengo Blog

Advertisements

One Response to JB Mpiana alivyochengusha Mwanza

 1. Richard Malewa says:

  Hapo sawa lakini ile ya Leaders Club, sorry to say ile ilikuwa ni Kashfa na Aibu kwa Bin ADAM!

  Naona Mwanza hakikunuka tunasuburia live CD na DVD tuone kama kweli Bin Adam alichengua.

  Mazingira ya Mwanza na Lake Zone yote kwa ujumla ukichanganya na uwepo wa Star TV na RFA Bolingo haiwezi tetereka hata siku moja ukilinganisha na DAR.

  SAWA HATA KAMA RADIO ZA HAPA HAWATAPIGA BOLINGO SIJUI BAMBATAA NA PROMO ZOZOTE ZILE LAKINI UKWELI UTABAKI ULE ULE MUZIKI MZURI UTATOKA CONGO DRC AU BRAZAVILLE NA HUKU KWINGINE ITABAKIA KUIGA NA KUTENGENEZA MIZIKI KWENYE STUDIO AMBAYO WASANII WAKE HAWAWEZI KUICHEZA LIVE! NA DUNIA INAKUWA KIJIJI SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA MBALI SIYO LAZIMA KUFUNGULIA REDIO ZA TANZANIA ETI NDIYO USIKILIZE BOLINGO.

  WATABAKIA MIKONO JUU MIKONO JUUU IMBA BASI SAUTI INAKWAMA KWAMA! HALAFU ETI MSANII MWENYE MAFANIKIO.

  .

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: