Umeninyima; Kolabo ya Papa Wemba na Mashujaa Band iliyokosa Promo

image

Pamoja na kuwa hawakufanikiwa kuzindua albamu yao lakini kwangu mimi bado MAshujaa Band ni moja ya bendi ambazo zimeleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya burudani nchini Tanzania.

Ni ukweli usiopingika kukosekana kwa kipindi cha Afrika Bambataa Clouds FM kumefanya muziki wa dansi ambao pia ulikuwa na mashabiki wengi sana nani asiyejua kuwa unapoongelea burudani unawaongelea Prime Time Promotion unawaongelea Clouds, tumeshuhudia jinsi matamasha yao yalivyo fana iwe kwa wanamuziki wa ndani au wanamuziki wa nje ya nchi, utake usitake kama unataka kitu chako kifanikiwe kwenye burudani hawa jamaa ushirikiane nao hata kama ni kwa shingo upande huna budi hiyo ndio hali halisi.

Kama kipindi kile kingeendelea kuwepo ni wazi mapenzi ya muziki huu yangeendelea kuwa juu. Mimi binafsi nilibadilishwa “dini” na kuangukia mapenzi yangu kwenye bolingo na Mr C Charls Mhamiji ambaye kiukweli kolabo yake na Njaidi naweza sema hakuna kama wao kwenye kipindi, kwa maana ya habari na muziki.

Tuyaache hayo tuangalie wimbo huu wa leo, Hii ilikuwa ni kolabo ya Mashujaa muzika na nguli mwingine mkubwa wa muziki wa dansi si tu kwa Congo bali kwa Africa kwa ujumla na ukiusikiliza wimbo huu  utakubaliana na mimi ukongwe unachangia sana, ila binafsi nakosa ladha ya vyombo hakuna kick kabisa kwa maana ya kuwa sauti imeizidi nguvu Vyombo.

All in all Mashujaa wameweza na nadhani wakifany marekebisho kwa yale matatizo madogomadogo watafanikiwa sana. Hongereni na binafsi nawakubali sana.

Advertisements

2 Responses to Umeninyima; Kolabo ya Papa Wemba na Mashujaa Band iliyokosa Promo

  1. Grand Tata Okelo says:

    Ninachofurahia Hapa ni uchambuzi unanifurahisha sana kaka.

  2. Nasib Kemba says:

    Pius unapoteza kipaji chako huko uliko andika habari tena andika habari za uchunguzi uyour very good on that.
    Congratulations Brother unatutendea haki sisi wasomaji wako.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: