Licha Ya umeme kusumbua, show kuchelewa, Jb Mpiana apagawisha mashabiki Dar

[http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=OgzuCQkuNAE]

 

image

Akiwaimbisha mashabiki

image

Wacheza show wakiwajibika vilivyo.

image
Mashabiki wakiwehuka na wenge BCBG julwaani.

image
Jb akiongoza wanamuziki Wa Wenge jukwaani.

image
Mmoja Wa wanamuziki akitoa burudani jukwaani.

image

image
Maboko likoloo kila mtu mikono yulu.

image
Suveree Mukulu Bin Adam Le Charismatique Papa Cherie Salvatory Le Patria Papa Matikakana Baba Ya Bana akiwa jukwaani. Picha na GPL

Mwana muziki Jb Mpiana akiwa na bendi yake Ya Wenge BCBG kutoka Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo, jana usiku iliwapagawisha mashabiki wa muziki huo nchini waliofurika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Katika onyesho hilo ambalo lilikuwa la aina yake, mashabiki walichelewa kupata burudani kutoka kwa mwanamuziki huyo kutokana na matatizo ya umeme, kitu ambacho kilisababisha bendi ya Mashujaa kushindwa kuwakonga mashabiki.

Pamoja na kuchelewa kuanza kwa shoo hiyo, kutokana na matatizo ya kukatika kwa umeme kila muda, JB Mpiana alianza kuwatanguliza wanamuziki wake wakiongozwa na mmoja wa waanzilishi wa bendi hiyo, Shai Ngenge, na kupiga sebene kabambe kabla ya kufuatiwa na wimbo wa zamani wa Kinie Bouger, ambao enzi zake alishirikiana na akina, Ngiana Makanda, miaka ya katikati ya 1990.

Wimbo huo uliweza kuondoa kero kwa mashabiki hao na kuwasahaulisha yale yaliyokuwa yakiwatokea wanamuziki wa Mashujaa, ambao kila walipokuwa wakipanda jukwaani na wanapofika kuanza sebene umeme unakatika, jambo lililowafanya kupanda jukwaani mara nne, lakini wakishindwa kumaliza wimbo mmoja tu wa Risasi Kidole. baada ya kukuru kakara hizo ambazo ziliwashtua viongozi wa Mashujaa na kufanya mmiliki wake Mama Sakina kuanguka kwa mshtuko na Presha kukimbizwa hospitali kupatiwa huduma ya ziada, bado haifahamiki hali yake ila kwa mujibu wa wadau wanasema anaendelea vyema na wanapanga show nyingine ya uzinduzi.

JB Mpiana alionekana kuwa ni mkombozi kwa mashabiki waliokuwa wamebaki huku wakipiga moyo konde kuwa hawataondoka viwanjani hapo bila ya kumuona JB, katika uzinduzi huo kutokana na burudani safi.

Kitu ambacho kiliwashangaza mashabiki wengi ni kutokatika kwa mara kwa mara kwa umeme kama ilivyotokea kwa bendi ya Mashujaa ilipokuwa jukwaani. Mpiana aliweza kufanya kweli katika shoo hiyo kwani umeme haukukatika mpaka aliposhuka jukwaani majira ya saa 10 alfajiri, “Kiukweli JB Mpiana ametutendea haki, nimeridhika na mi nilikuja kumuona JB ambaye nimemuona na nimeridhika sana” Alisema shabiki mmoja Mabamba ambaye anaupenda muziki huu.

Katika shoo hiyo, Mpiana aliweza kupiga nyimbo mbali mbali za zamani ikiwa pamoja na Barakuda, Djodjo Ngonda, Walay Danico, Dizoizo na zile mpya katika mtindo wa non-stop.

Mashujaa ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na mara walipoanza kucheza shoo ya ufunguzi ambao imewajumuisha wanenguaji wa kike na wa kiume na waimbaji, umeme ulikatika na kazi ya kuanza kurejesha ikaanza na kuchukua muda wa dakika zisizopungua 30.

Pamoja na hizo kasoro chache JB Mpiana ametutendea Haki mashabiki wake na kuikata kiu ambayo wengi walikuwa nayo.

8 Responses to Licha Ya umeme kusumbua, show kuchelewa, Jb Mpiana apagawisha mashabiki Dar

 1. richard malewa says:

  kupenda kwingine bwana !

  show imeanza saa kumi alfajiri !

  hao walikuwa mashabiki au wanga?

 2. Lebcbgbanaarusha says:

  SHOW YA ARUSHA Triple A

  show ilikuwa bomba sana tulipagawa mbaya!! Jamaa hawa ni noma kitu live na si digital !!!

  misimbazi yangu waliitendea HAKI

 3. Bhikolo Ngona says:

  mambo vp mwana wa Mikongoti.ulifuat ilia suala la Gangnam style dance mpunda?

 4. Anonymous says:

  Ila jamaa nimwaminia ni “Mtaalamu” Mashujaa walishindwa kupiga muziki ulikuwa unazimika zimika lakini Jamaa alipongia wala haukuzima tena. Chezeya JB wa ukweli weyeee…

 5. […] Kama ulimiss show ya JB Pale Leaders Club basi pata kionjo hapo kwa picha na habari gonga hapa. […]

 6. The moment I believed about issues like: why such info is totally free here? When you create a book then a minimum of on marketing a guide you receive a percentage, because. Thank you and fantastic luck on informing men and women far more about it.

 7. I unquestionably appreciate each minor bit of it and I have you bookmarked to test out new stuff of the web site a should go through blog site!

  • When I apply this information I will be sure to use your blog in my list of sources. I really appreciate this! Using your advice has seriously increased my street credit. I truly love your writing style and how well you express your concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: