Nawatakia Uzinduzi mwema Mashujaa Band lakini ninalo la kuwaambia.

Kwa mashabiki wa Muziki wa dansi watakubaliana na mimi kuwa Mashujaa Band ni moja ya bendi ambazo kwa kiasi kikubwa zimeleta ushindani mkubwa kwenye muziki wa dansi nchini ambao kwa muda mrefu ulikuwa umetawaliwa na bendi mbili za FM Academia na Twanga Pepeta.

Mashujaa wamekuwa wapinzani wakubwa wa Twanga bendi ambazo zinapiga muziki unaofanana, inawezekana ushindani huu unatokana na wamiliki wake kuwa maswahiba na kuchochewa na wanamuziki ambao wametoka bendi moja kwenda bendi nyingine hasa Twanga kwenda Mashujaa. Leo tunashuhudia Mashujaa wakizindua albamu yao ya Risasi kidole huku wakisindikizwa na nguli wa muziki barani Afrika Jean Bedel Tshituka Mpiana na bendi nzima ya Wenge BCBG. kwa wanaojua muziki wa Tanzania watakubaliana na mimi bendi hizi zimeleta mapinduzi na nafikiri MAshujaa wataweza kumfanya JB Mpiana aige kitu kutoka kwao na kesho na sisi tuseme JB Mpiana ametuiga.

Tulishuhudia Simba na YAnga zikitamba kwa muda mrefu leo hii hakuna aliyetegemea timu kama Azamu inaweza kuleta upinzani kwenye ligi ya Tanzania, mapinduzi haya katika sekta ya burudani ndiyo yaliyoibeba leo hii Mashujaa kuwa hapo ilipo, kwa nini mashabiki wawapende nyinyi na sio Twanga au bendi nyingine ni wazi kuwa wanataka kitu kipya na hakuna mwingine wa kuwapa hicho kipya zaidi yenu. Mashabiki ni wale wale ni lazima mjifunze ni nini kilipungua kwenye bendi nyingine ili nyie mkifanyie kazi kuwapa raha mashabiki, naurahi kuwaona kwenye mitandao jamii kwani mnasogea karibu na mashabiki ili waweze kuwapa mawazo yao, lakini kumbukeni ninachosema mimi hapa wapo wengi huko nyuma ambao hawana platform kama hii ya kuongelea, hatuandiki kwa nia mbaya ni kiroho safi tuu ili tuweze kujenga na kuendeleza muziki wetu wa dansi nchini.

Majuzi wanamuziki wa Mashujaa walikuwa kwenye kipindi cha Baragumu cha Channel Ten na wakinadi uzinduzi wao ambapo mashabiki wengi walipiga simu kuwapa usia na mawaidha mengi akiwemo rafiki yangu Mwaulanga. labda mi ningeongezea kidogo, Mara ya mwisho JB Mpiana anakuja nchini nilifanikiwa kuwepo kwenye kutano na waandishi wa habari na kati ya maswali aliyoulizwa ni jinsi gani anaweza kudumisha nidhamu ya wanamuziki wake ikizingatia wanawapenzi na mashabiki wengi, JB Mpiana alijibu kuwa hawaruhusu kunywa pombe kupita kiasi, kula vitu vya baridi, kunywa pombe siku ya show, huku akimtolea mfano Zulema ambaye alikuwa na tatizo la ulevi na kuwajibishwa. Ukiangalia jibu hili la JB Mpiana na jinsi ambavyo wanamuziki wa Bongo wanavyofanya utakubaliana na mimi kuwa bado tuna kazi ya kufanya.

Kwa wanamuziki wa Tanzania ulevi ni kitu cha kawaida, hawana muda wa kupumzika na ndio maana unakuta wengi wao wanakaaa kwenye chat kwa muda mfupi sana. huwezi kuwachukua wanamuziki wa bendi zetu na kuwakuta wanaimba masaa mawili mfululizo au play list ya nyimbo saba lazima unamkuta mtu amepotea jukwaani, mara nyingine hata verse yake inafikia ye hayupo jukwaani ama yuko na akina dada au kashikiria chupa ya lager akisogoa na mashabiki. mara ya mwisho JB Mpiana alipopiga pale Blue Pearl Ubungo Plaza alipiga non stop ya masaa kama matatu hivi yenye play list ya nyimbo za kutosha bila kupotea jukwaani na kila mtu aliridhika, sasa niachowaasa wenzangu MAshujaaa wakazanieni nidhamu wanamuziki wenu, wapigeni marufuku kulewa wakati wa kazi, kukaa na mashabiki wakati wa kazi, mazoea yawekwe kando na tufanye kazi muda wa kazi, Jana JB Mpiana akiongea na waandishi amewaasa esnsmuziki wa Tanzania kujituma na kuzipenda kazi zao na kuziheshimu ili waweze kufikia mafanikio, tunawatakia uzinduzi mwema.

5 Responses to Nawatakia Uzinduzi mwema Mashujaa Band lakini ninalo la kuwaambia.

 1. Anonymous says:

  mashujaa hawabahatishi brooo nimekubali

 2. Francis Ngatuka says:

  Umeongea point, mashujaa mpo?

 3. mashujaa band says:

  asante sana kaka,tumeupokea ushauri wako

 4. richard malewa says:

  Eeeeeeeeeenh ! eti Tshutuka Mukulu majina meeeeeeengi leo kaingizwa choo cha kike. JB amekuwa mtu wa kupigia uchochoroni JB huyu huyu aaaaaaaaaah ! chezeya wazee wa jiji.

  wajanja tulikuwa zetu Mzalendo tunapata YENU ya Ukweee…

  Ama kwa hakika hakuna tena hamasa kwa JB kama ilivyokuwa miaka ile na sidhani kama atatamani kupiga tena hapa nchini labda iwe kwa mambo mengine nje ya muziki ndiyo yatamvutia tena. JB wa kupiga muziki saa tisa usiku mpaka watu walewe kwanza laaaaah !

  angekuwa Mzee Mzima mwenyewe wa MALEWA ungeona shughuli yake ! mtanisamehe sana sijatembelea muda mrefu lakini imenibidi hivyo kwa yale yaliyotekea jana.

  RICHARD MALEWA

 5. Paz Lecky says:

  I think this can be an informative post and it can be educated and very handy. I would like to thank you for your efforts you may have made in creating this post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: