Women of Determination Award 2012 Kuhamasisha akina mama wa Kitanzania.

DSC_0567

Waratibu wa Kongamano la Woman of Determination Award and Conference 2012 toka kushoto Mama Benadeta Choma, Bi Fatma Kange na Dr. Ellen Otaro wakiongea na waandishi wa Habari asubuhi hii.

DSC_0579

Waaandaaji wakijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wao wa leo.

Tuzo za Women of Determination Award and Conference zinatazamiwa kufanyika tarehe 1 December 2012 katika hoteli ya Ubungo Blue Pearl jijini Dar Es Salaam.

Wakiongea na waandishi wa habari jijini leo, waratibu wa Tamasha hilo wamesema kuwa dhumuni kubwa la Tamasha hilo ni kujaribu kuwaweka pamoja wanawake waliothubutu ili kuchangia mawazo mwisho wa siku waweze kuwapa hamasa wanawake wa Tanzania ambao wengi wao hawana utayari wa kuthubutu. “…Wengi wa akina mama wamekuwa waoga kuthubutu tunataka kuwajengea uwezo ili waweze kuthubutu” alisema Dr. Ellen Otaro mmoja wa waandaaji wa Kongamano hilo.

Akiongea wakati wa mkutano huo na Waandishi wa Habari Bi Fatma Kange ambaye ni muasisi wa tuzo hizo amesema kuwa mwaka huu tuzo hizo zimeongezeka kwani wameongeza category ambapo wanawatambua na kuwapa tuzo wanawake ambao wamethubutu si tu kutoka jijini Dar Es Salaam bali Tanzania nzima kwa ujumla, aidha bi Kange amesema kuwa kuna haja ya kuwahamasisha mabinti zetu na kuwaweka karibu na hawa akina mama ambao wamefanikiwa ili kuwaonyesha njia kwamba wao wamefikaje fikaje.

Akichangia hoja hiyo Dr. Ellen Otaro ambaye ni mmoja wa wadau kwenye kongamano hilo amesema kuwa kauli mbiu ya wanawake wakiwezeshwa wanaweza inawafanya akina mama kusubiri kuwezeshwa jambo ambalo linafanya akina mama wengi kutofanikisha ndoto zao lakini “seeing is believing” wakiwaona wenzao wakiongea njia walizofikia kuwafanya wafike walipo, wanawake wanaweza kufanikisha ndoto zao. Aidha akijibu swali la waandishi wa habari Bi Benadeta Choma amesema kuwa Tuzo za mwaka huu zitawaleta pia wake wa viongozi na wanawake wa kawaida wakijumuika pamoja na wale kumi na moja ambao wameteuliwa na kamati kupata tuzo hizo, aidha Mama Choma amesema kuwa washindi wa tuzo hizo watapewa vyeti na ngao maalumu kwa ajili ya kumbukumbu za mchango wao kwa walichokifanya na huko mbeleni wanafikiria kuanza kutoa pesa kama hamasa kwa akina mama wengine waweze kuthubutu.

Awali akiongea na Spoti na Starehe Mama Choma alisema kuwa Kongamano hili linatofauti na mengine kimtazamo kwano pamoja na burudani na chakula cha usiku kwa siku hiyo, akina mama waweza kujifunza baada ya kusikia kutoka kwa washiriki mbali mbali, “fikiria binti akimuona Mwanamke mwenzake akiendesha ndege au basi au Daktari ambaye ametokea Kijijini akasomea kijijini lakini ni Daktari bingwa anaongea pale mbele ni wazi na yeye atajipa moyo kuwa akijitahidi na yeye anaweza” alisema Mama Choma.

Kongamano la Women of Determinations litafanyika jioni ya Tarehe 1 Desemba 2012 katika ukumbi wa Ubungo Blue Pearl ambapo Wanaopenda kushiriki wanatakiwa kulipa shilingi elfu thelathini kwa mtu mmoja na kama ni kikundi cha watu wa tano watalipa shilingi laki moja hii ikiwa ni Gharama ya chakula cha jioni, na kutakuwa na burudani ya muziki pia. aliongeza Mama Choma na kuongeza kuwa Si dhumuni lao kuwachangisha akina mama kwani wangependa akina mama wengi zaidi washiriki lakini bado hawana wadhamini wa kuzidhamini tuzo hizo na pesa hizo ni kuchangia gharama kidogo ambapo watapata na Elimu, chakula cha jioni na Muziki.

Akichangia hoja hiyo Bi. Kange amesema kuwa kikubwa ni ile elimu ambayo anakuja kuipata toka kwa akina mama wenyewe waliofanikiwa wakiongea toka kwenye vinywa vyao.

inakadiriwa zaidi ya wanawake mia tatu watashiriki kwenye kongamano hilo ambalo huu ni mwaka wa pili tangu liasisiwe. Kauli mbiu ya mwaka huu ya kongamano hilo ni Kuwajenga, Kuwatambua na Kuwaunganisha.

Advertisements

One Response to Women of Determination Award 2012 Kuhamasisha akina mama wa Kitanzania.

  1. Pretty sure he’ll have a superior go through. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: