SG ELIOT MONDOBE Katibu Mkuu wa WMMM aliyekimbilia Canada.

Tatizo kubwa la Radio Station Zetu ni kupiga muziki wanaoujua tuu na nyimbo nyingine hazipigwi au hazipewi Air Time ya Kutosha. Hii inafanya nyinmbo nyingi kutojulikana kwa wapenzi wa muziki labda kwetu sisi wadadisi ambao tunanunua albamu na kuto forward nyimbo mwanzo mwisho.

Werasson aliondoka Wenge BCBG baada ya mzozo wa pesa na uongozi baina yake na JB Mpiana, alipoondoka alikwenda kuanzisha WMMM na vijana wake akatafuta vijana akawatengeneza wakaiva hatimaye WMMM ikatisha balaa.

SG Eliot Mandobe ambaye alijulikana kama Secretary General, au Le Secrétaire Général de l’orchestre alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na kukubalika ndani ya kundi la WMMM. Lakini kizuri hakidumu jamaa alikimbia bendi kwa kashfa ya Human Trafficking na kukimbilia Canada hasa baada ya Show ya Zamba Playa ambapo alisemwa kuwa alikimbia akiwa na maelfu ya dola ambazo alikusanya toka kwa watu ambao aliwaahidi kuwatafutia VISA ya kwenda Ulaya, Canada na Marekani kupitia mgongo wa bendi.

Suala la Human Trafficking liliwahi kumgarimu Shumbu Wemba Dio Papaa Wemba Miezi kadhaa jela huko Ufaransa na Fellix Wazekwa aliwahi kutandikwa miezi kumi gerezani huko Braxelles kwa kosa kama hilo ambapo kuna wakati VISA za wanamuziki wa Congo zilisumbua kwani Tshengeni iliamua kupitia upya maombi yoote ya VISA toka kwa wanamuziki wa CONGO. Mandobe baadaye alijiunga na familia yake ikiwa ni mke na watoto ambao walitangulia kuishi huko, Nakuacha na kibao hiki ambacho utamuona vizuri Mandobe akikamua akiwa na Tata Mukulu Werrason Ngiama Makanda ndani ya Wenge Musica Maison Merre.

Big up kwa ma people Bahati Nyakiraria wa 90.2 Moshi FM mtangazaji wa kipindi cha Tamba Africa kiukweli napenda sana mpangilio wa vipindi vyako fanyeni mpango wa kwenda Online watu wengi waweze kuwasikiliza, Mercy Mingi Papaa.

p

4 Responses to SG ELIOT MONDOBE Katibu Mkuu wa WMMM aliyekimbilia Canada.

  1. Hadj le Jbnique says:

    tatizo la redio presenter huko nyumbani kweli ni kubwa sana,binafsi nina dream ya kurudi huko siku moja na kuanzisha show on redio kwa ajili ya nyimbo na habari za muziki na wanamuziki wa congo,show itakua ni burudani ya muziki na kufanya uchambuzi ili watu wawe informed na muziki na wanamuziki wawapendao,maana wapenda muziki wa lingala huko nyumbani wamekua kama yatima hata kenya wenzetu wanatushinda kwa ku cover story za muziki wa congo bwana na ukitazama bongo ina mashabiki wengi zaidi wa muziki huo,thanks kwa zuberi musabaha wa RFA anafanya kazi nzuri sana pale redioni kila j’nne nafikiri japo huwa anaingiliwa na dokta flani wa mitishamba ambae sijui kwa nini nae akachagua kipindi cha bolingo time ya musabaha nadhani ni baada ya kuona kipind kinasikilizwa zaidi

  2. Pascal Canisio says:

    Harakati za kuua mziki wa kiafrika zinafanywa kwa makusudi na presenters wanaotamani utamaduni wa kimagharibi!

  3. Aw, this was an exceptional good article. It must have taken you great efforts to create this article… Appreciate!

  4. a lot of wonderful details and inspiration, both of which I want, due to offer you this kind of a useful information here.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: