Kama ulimkosa Rick Ross the Boss Fiesta huyu hapa

Tamasha la Fiesta limehitimishwa jijini Dar Es Salaam huku mwanamuziki toka Marekani Rick Ross the Big Boss akiwa ameacha gumzo.

Pamoja na kuwa na onyesho hilo moja tu la hapa Dar E Salaam mwanamuziki huyu ambaye inawezekana akawa amelipwa pesa nyingi kuliko malipo ya wanamuziki wote ukiyajumuisha waliopanda jukwaani usiku huo. Ni ukweli usiopingika kwa mwanamuziki kama huyu ambaye ni mmiliki wa Lebo ya Maycack Music mpaka amekubali kukaa ndani ya ndege kwa masaa 25 lazima amekula dela ya kutosha kwa performance yake hiyo moja tu ambayo hajailipia kodi hapa kwetu na kusepa.

Kuna haja ya kuthamini wanamuziki wa nyumbani kwa kuwapa mikataba minono ya matamasha hii itawafanya hadhi yao kupanda kwa kiasi kikubwa mbele ya mashabiki wao na kuuukuza muziki huu, kwani kumlipa mwanamuziki mmoja kupanda jukwaani ni sawa na malipo ya chumba kimoja cha Presidential Suite ambacho jamaa amelala kwa usiku mmoja kwenye hotel ya Kempisk, inawezekana wengi walienda kumuona The Big Boss ama kwa kutaka kuweka kumbukumbu kuwa amemuona kwa macho yake lakini waliburudishwa zaidi na Mwana FA, Fid Q, AY, Lina na wengine, Ni mtazamo tuu nimeut oa kiroho safi.

Kwangu mimi nadhani kulikuwa na haja ya wanamuziki kuchanganya ladha kwenye tamasha kubwa kama hili unaweza kuwaleta wanamuziki tofauti ili mashabiki wa aina hyo ya muziki nao wakaona wamewakilishwa wangevuta watu wengi kwa kutumia pesa ingawa si kidogo lakini si kama hizi za kumleta mwanamuziki kutoka Marekani.

Fiesta ya zamani ilikuwa inachanganya ladha, jaribu kufikiria kama pale angekuwepoa Koffi, Fally, Ferre au Werrason achilia mbali JB Mpiana kuna mashabiki wengi wa Bolingo wangetumbukia pale kati kushow love na watu wao anyway nadhani waandaaji wana sababu zao.

Nitaandika kwa kirefu kuhusu mtazamo wangu huu baadaye nisikuchoshe na jumatatu ya leo, Siku nema.

Advertisements

3 Responses to Kama ulimkosa Rick Ross the Boss Fiesta huyu hapa

  1. Admiring the dedication you put into your site and detailed information you provide. It’s awesome to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed material. Excellent read! I’ve bookmarked your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

  2. Really great site and exceptional and articles or blog posts.useful design, as share very good stuff with fantastic thoughts and ideas.

  3. Very interesting info !Perfect just what I was searching for!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: