Cindy Olomide Mpenzi wa Koffi anayetamba Quartier Latin

Ukiachilia mbali akina Mbili Abel, Tshalla Muana ama akina Skolla Miel kwa muda mrefu Congo ilikuwa haina mwanamuziki mwingine wa kike kwenye ramani ya dunia ya muziki hasa mbele za mashabiki wa Lingala ambao wakoo ndani na nje ya Congo yenyewe.

Anaitwa Cindy Olomide, huyu bidada alikwenda kufanya interview kwa Koffi akiwa na wanadada wenzake akiwamo Monica Maire na Meje 30 ambaye  kwa kiasi kikubwa aliibuliwa na mwanamama Tshalla muana na aliwahi kuja naye Tanzania kwenye onyesho la Club E wakapiga pamoja na Mukullu Bin Adam Tshituka katika ukumbi wa Ubungo Blue Pearl.

Cindy Olomide licha ya kuwa mwanamuziki anayetamba sana kwenye bendi ya Koffi Olomide pia ni mmoja wa wake wa Koffi Olomide na ni mmoja wa wanahisa wa Quartier Latin ya Koffi Olomide. Mwanadada huyu ambaye mapenzi yao kwenye sanaa yalipelekea mcheza sinema maarufu hapa Tanzania Steven Kanumba marehemu kujifananisha na wawili hawa Koffi na Cindy na yeye na Lulu ambaye yuko rumande sasa akituhumiwa kusababisha kifo cha mpenziwe Kanumba nao waliitana Mopao na Cindy (Gonga hapa usome). Inawezekana hii ilikuwa kwa sababu Cindy alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Boss wake ambaye ni Koffi na ndivyo ilivyokuwa kwao. Sio nia yangu kulizungumzia sana hilo ila ni katika kunogesha story yangu, Mungu amlaze marehemu Pema peponi.

Cindy amejizolea umaarufu kwa kuzirudia nyimbo hasa za taratibu na kumfanya Koffi kubakia vinywani mwa mashabiki kila mara, Koffi ambaye mapema mwaka huu alifungua jumba lake la kifahari amesema anataka kuweka studio ndani ya jumba hilo ili aweze kurekodi nyimbo zake mwenyewe. Awali akiongea na Zakarie Bababaswe mtangazaji mkongwe wa burudani Koffi alisema kuwa ana hazina ya nyimbo zaidi ya 100 ambazo ameshaandika bado kurekodi. Mopao uko juu.

Advertisements

One Response to Cindy Olomide Mpenzi wa Koffi anayetamba Quartier Latin

  1. Thank you for every other excellent article.I’ve a presentation next week, and I have found what I can add in my speech. Great job!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: