Nyoka Longo asherehekea Birthday yake na mashabiki wake.

Hana makuu ni mtu wa watu na ndivyo alivyoisherehekea Birthday yake ya miaka 59 akiwa na watu wengine waliozaliwa tarehe 7 September kama yeye.

Anaitwa Jossart Do yoka Longo ambaye ni moja ya Ma Legend wa muziki wa Congo alisherehekea siku yake ya kuzaliwa na mashabiki Lukuki kwa kutoa burudani safi kwa mashabiki wake waliojumuika kwenye ukumbi wa Ex-trême Ville.

Nyoka Longo ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la Zaiko Langalanga alizaliwa September 7 1953 nchini Congo zamani Zaire.

Ukumbi ulilipuka kwa mayowe baada ya Nyoka Longo kuingia ukumbini akiwa amechelewa kutokana na foleni ya kutoka Airport wakiwa wanarejea kutoka Lumbumbashi ambapo walialikwa kwenye sherehe ya siku ya Kuzaliwa ya Carine Katumbi kutimiza miaka 40, ni mke wa Moize Katumbi Chapwe tajiri na mmiliki wa T.P Mazembe na Gavana wa Jimbo la Katanga.

Sherehe ziliendelea huku watu wakiburudishwa ilipofika saa tano usiku MC wa Shughuli alialika wote walizaliwa 7th September na walifunga ndoa na kuanza kumtunza Nyoka LOngo huku muziki ukitumbuiza, Baadaye kijana wake alipanda jukwaani na kutoa mawili matatu, Ignatius Nyoka ambaye ni mtoto wake mpendwa alielezea jinsi baba yao alivyo na mapenzi na walivyofarijika kwa jinsi alivyosherehekea siku yake ya kuzaliwa.

16 Responses to Nyoka Longo asherehekea Birthday yake na mashabiki wake.

 1. Malik Kondo says:

  Kama kweli wewe ni mpenzi wa muziki wa Congo basi inabidi umpe saluti Joseph M’vula a.k.a. Nyoka Longo Jersy Ya Jossart. Huyu bwana ndo muasisi wa Cavacha mpaka kuja huu muziki tuliozoea sie vijana wa kina JB Mpiana na Werrason. Ikumbukwe mnamo mwaka 1969 huyu Josart aliwashawishi wenzake kina Papa Wemba na Evoloko waachane na muziki wa rhumba na wapige mtindo wa vijana, na wenzake wakakubali yeye Jossart akiwa ndo kiongozi wao katika bendi ya Zaiko Langa Langa. Bozi, Papa Wemba, Evoloko, Lengi Lenga, Likinga, manuwaku, Dindo Yogo, na wengine kibao ambao TZ hamuwajui wametokea hapa. Defao na shimita ni zao la Manuwaku mpiga solo wa kwanza wa zaiko. Stino, Luciyana demingongo, reddy amisi ni zao la Papa wemba mwimbaji wa zaiko, wanamuziki wengi sana kiasi siwezi kuandika ni chimbuko la zaiko. Koffi olomide alijifunzia muziki kwa papa wemba na zaiko kisha akaja kuunda bendi yake hapo baadaye 1986. Kina clan wenge wote walianza kupiga muziki wao 1981 kwa kuiga nyimbo za zaiko na baadaye walipopata uzoefu wkaja na style yao kama zilivyo bendi nyingine. Pia zaiko ndo bendi ya kwanza kuunda marepa (atalaku) mwaka 1981 kisha kufuatiwa na bendi zingine hapo baadaye.mwaka 2000 ilitunukiwa bendi bora ya karne huko Congo Kinshasa kwa mchango wao wa kukuza muziki wa congo. Hongera ya Jossart, unatisha kwa kipaji chako. Haijatokea bendi iliyokuwa na wanamuziki wenye vipaji kama zaiko na sidhani kama itakuja tokea.Bendi liyojitahidi kidogo ni viva la musica ya Papa wemba na kidogo wenge musica bcbg.

  • Djomali Aimee says:

   …Ni kweli, Zaiko ndiyo bendi pekee iliyoleta huu mtindo wa cavacha na kuigwa na orchestra Kiam na bendi zingine za Vijana miaka hiyo ya 70 na 80 mpaka sasa. Miaka ya 70 na 80 hakukuwa na bendi iliyoipa challenge Zaiko zaidi ya Stukas (bendi ya Lita Bembo), na Victoria Eleison (Emeneya Mutu ya Zamani). Miaka ya 90 ikaja Wenge Musica BCBG kidogo lakini nayo ikashindwa kuizidi Zaiko kwa umaarufu. Wenge ilikuwa inapendwa zaidi na watoto na vijana chini ya miaka 25. Miaka ya millennium kina Mpiana na Werrason walitamba sana Kinshasa baada ya Zaiko kwenda Ulaya kwa miaka 5, na Kinshasa kukawa hakuna wapinzani wa Mpiana na Werrason. Kwa kipindi hiki (2004 – 2010) muziki wetu haukuwa mzuri mpaka Papa Lutumba Simaro wa Bana OK akaingilia kati na kumshawishi Nyoka Longo arudi kuendeleza dozi Kinshasa ndipo naye Nyoka akakubali kurudi na baadhi ya wanamuziki na kuunda zaiko mpya. Sasa Zaiko imerudi kila mtu katulia tunakula “Mokongo Ya Koba” (mtindo mpya wa Zaiko unaotamba kila kona hapa Kinshasa). Kwa utaalamu wa muziki Nyoka Longo anaitwa “Vieux Bombas” ama kwa Kiswahili ni Mze wa dozi!

 2. Hadj le Jbnique says:

  Zaiko na wenge musica tout terrain kila mmoja alikua na mashabiki wake hata wakati walipopiga pamoja one stage hilo lilijidhihirisha wazi

  • Kingotolo Mboyo says:

   Kwani hukumuelewa jamaa kasema nini hapo juu. Wenge ilikuwa inapendwa zaidi na watoto pamoja na vijana wa chini ya miaka ya 25 miaka ya hiyo ya 90. Kwa maana hiyo vijana wale wale bado pengine mpaka leo ni mashabiki wa wenge au siyo? Zaiko ndiyo babu wa muziki wa vijana Congo toka miaka ya 1970, unabisha? Congo yote inajuwa hivyo au wewe siyo mcongo? Jiulize, kuna bendi yeyote Congo ambayo imekuwa na wanamuziki mashuhuri zaidi ya Zaiko ama Clan Zaiko? Jibu ni hapana na sidhani kama itatokea. Clan Zaiko ni: Zaiko langa langa, langa langa stars, choc stars, Grand zaiko wawa, viva la musica, Victoria Eleison, Koffi Olomide, Bozi Boziana, Lengi Lenga, Familia Dei, Wenge yenyewe iko influnced na zaiko langa langa ila wao tu wamekuja miaka ya mwishoni mwa 80 na kupata sifa miaka ya 90 na ndiyo maana wanapendwa sana na vijana wa leo lakini zaiko ni kweli Modele Echanger Ya biso Kaka! Nani anabisha? Unakumbuka Nyoka Longo alisemaga: “Nyoka Longo combattant, parfois battu”….mais jamais abattu! Maana kwamba Nyoka Longo mwana mapambano, kuna wakati anapambanishwa lakini hashwindwi daima juu! Ndiyo maana anaitwa mze wa dozi ama Vieux Bombas.

 3. Grand Tata Okelo says:

  Ni kweli Zaiko walianzisha na baadaye ilichukuliwa na bendi nyingine na Wenge walikuwa wa kwanza hasa baada ya mwaka 1982 Muziki wa Marekani wa kufoka ulipoanza kuwa maarufu Congo ni baada ya Ngumi za George Foremen huko Zaire, Ndipo Wenge Musica BCBG walipomuachia jukumu hilo Roberto Wunda Ikokota jahazi la Ghani na kuwafurahisha vijana na muziki wao na ndipo Wenge walipochukua hatamu kwenye muziki wa Viajana na wengineo akiwemo TP OK Jazz, Zaiko, Grand Perre Tata Bozi Boziana, MAdillu na wengineo kubaki na muziki wa Bakurutu ingawaje wengine wao waliingia kwenye ghani kidogo ambapo Gitaa la solo lilikuwa likiwaongoza Marepa na Tumba na Drums zikiwachezesha wacheza show…..!!!!

  • Djomali Aimee says:

   Wewe grand tata Okello naona unajichanganya sasa na siyo vizuri kuandika habari za kuzania ama kuambiwa. Wenge Musica tout terrain ili anza kupata umaarufu mwaka 1989 na mwaka 90 na 91 ndipo ikawa bendi bora Zaire/Congo baada ya bendi nyingi kuhamia Paris na Kinshasa kukawa hakuna ushindani. Hizo ngumi za foreman Kinshasa ilikuwa ni mwaka 1974 kipindi hata kina Mpiana walikuwa hawajaacha kujikojolea kitandani. Hiyo Wenge ilipopata umaarufu tayari Zaiko walikuwa wamesha cement umwamba wao wa kurap na wenge ikabidi ifuate nyanyo za baba zao Zaiko lakini SIYO wenge ilioanzisha kurap ni ZAIKO LANGA LANGA NKOLO MBOKA.

 4. Hadj le Jbnique says:

  KIUFUPI ZAIKO NI BENDI YA WAZEE NA WATU WA KIAZAMANI WENGE ILIKUA MAALUM KWA VIJANA HTAMAVAZI YA WENGE NA ZAIKO UKITIZAMA YANAKUELEZA NINACHOKISEMA,ILA YOTE KWA YOTE WOTE MWISHONI WALIKUJA KUELEWANA KUHESHIMIANA NDIO MAANA UNAONA HATA WAZEE WA ZAIKO WAKAFANYA SHOW YA PAMOJA NA WATOTO ZAO WENGE MUSICA,NI KWA KUWA WALIKUA WANAWAKUBALI MAANA WALIKUJA KUIGAWA KINSHASA KATIKA PANDE MBILI ZENYE NGUVU SAWA,VIJANA NA WAZEE,ILA ZAIKO LAZIMA TUKUBALI WANHESHIMA YA PEKEE KONGO KUTOKANA KUDUMU KWA MUDA MREFU,NI KAMA MSONDO NGOMA MUSIC BAND KWA TANZANIA,LICHA YA KUJA BENDI KAMA TWANGA NA MASHABIKI WAKE VIJANA LAKINI MSONDO IMEENDELEA KUDUMU NA MASHABIKI WAKE WAZEE NA VIJANA WACHACHE AMBAO PIA WANAIPENDA TWANGA,HESHIMA YA ZAIKO NILIIONA WAKATI FULANI WALIFIKA TANZANIA WAKATI HUO WENGE NAO WALIKUA TANZANIA,CHA KUSHANGAZA SIKU ALIPOTUA NYOKA LONGO ALIKWENDA KUPOKELEWA NA BALOZI WA CONGO!HALI HAIKUA HIVYO KWA WENGE

  • Djomali Aimee says:

   Licha ya kudumu kwa muda mrefu ni bendi pekee iliyotoa vipaji vya uhakika Congo. Hakutatokea tena bendi kama hii yenye watu wa vipaji, ah NKOLO MBOKA ya biso kaka. Nyoka Longo combattant, parfois battu mais jamais abattu, mwisho wa yote…hakuna cha Mpiana wala Werrason hapo, kaka ye moko toujours!

   • Hadj le Jbnique says:

    Tizama video hii then uwe fair kutoa maoni bila ushabiki kupita kiasi,tunaiheshimu na tutaendelea kuiheshimu zaiko na mzee nyoka longo lakini hatuwezi kukataa ukweli kwamba wenge ilikuja kuipa changamoto zaiko ambayo haikuwahi kuipata kabla,wenge ileweza kulipua jiji la KIN katikati na kuthubutu kugawana mashabiki na baba zao wa zaiko
    sikia “boma liwaza” ilivyopokelewa na mashabiki ndio utaelewa kirahisi nasema nini,but mwisho wa siku much respect kwa zaiko na hasa pesidaa nyoshi,kwa kuidumisha zaiko

   • Djomali Aimee says:

    Jbnique usijichanganye na kukasirika bila sababu. Ni kweli Wenge ilikuja juu miaka ya mwanzo wa 90 na kuipa Zaiko ushindani, hiyo hakuna aliyekataa. Zaiko ndo orchestre nationale du Congo, hawa ndo walioanzisha kila upigaji wa soukous kuanzia drums (Ya Meridjo), na solo la cavacha (Pepe Felly alias Manuwaku Waku Le Magicien). Hivi vizazi vya sasa wote wanafuata nyayo za baba zao Zaiko. Ushindani lazima uwepo si kwa Zaiko tu na Wenge bali hata kwa hawa Vijana wa leo kama vile Fally na Ferre ama Reddy na Montana, Wazekwa na Karmapa, Koffi na watu wote anaowaona wanapiga muziki mzuri. Bila ushindani muziki haupendezi. Naomba nikuulize, kwa muziki wa sasa unampenda nani kati ya Souverain 1er na Ya Ng’iama?

 5. Hadj le Jbnique says:

  Sijachanganya wala kukasirika kwa kawaida huwa nafurahia mijadala na chalenge kama hizi kwani napenda kujuifunza zaidi na zinasaidia kujifunza kwa tunaopenda kujifunza kwa kuwa katik hali ya kawaida binadamu huwezi jua kila kitu.Kuhusu mapenzi mimi humu kila mtu anafahamu niliipenda sana wenge musica 4×4 tout terrain toka ndani ya roho na mpaka kesho nasikiliza sana nyimbo zao utadhani zimerokodiwa mwaka jana kwa ubora zilionao,na kwa mwanamuziki mmoja mmoja wa iliyokua wenge kama unavyojua baada ya kugawanyika wengi wa wapenzi wa wenge na sisi tuligawanyika,mimi kwa kuwa toka wakati ule mpaka leo namhusudu SALVATORE DE LA PATRIA MOTO PAMBA PAPAA NA DAIDA,SURAYA na JUNIOR JB MPIANA.

  Nawaheshimu ZAIKO na nilikua nawafuatilia sana kipindi kile wakipiga shows zao pale kipwanza bar kabla ya kuondokewa na kina Beniko Popolipo,Jimmy Yaba na Petit Poisson ambao walikua wapiga gitaa mahiri ambao waliondoka kwa mkupuo na waimbaji na watunzi wao mahiri ambao waliwategemea sana kipindi kile kina Lengos,ya jp buse,ya ombale. Wengi tukadhani kuwa ndiyo mwisho wa zaiko maana yalikua ni mapengo ambayo yasingekua rahisi kuzibika.Hapa ndipo huwa mpaka leo nampa heshima Presidaa Nyoshi.

  Zaiko ilikuja upya kwa kuchukua vijana ambao watu wengi waliwashangaza. Vijana hao si wengine bali ni kina Shiro Mvuemba, Baroza, na wengineo wengi tu ambao ilifanya zaiko iwe juu.Lakini kusema kwamba wenge ilipata nafasi ya kuwashika mashabiki wa kin kwa kuwa zaiko haikuwepo kinshasa ilikua ulaya! hii inatia shaka kidogo kuiamini moja kwa moja,ndio maana nikaweka hiyo video ya zaiko na wenge on one stage ili kuonyesha kwamba zaiko walikuwepo kinshasa wakati huo ndio mana wakaweza kupiga pamoja na wenge ya kinshasa sio ya paris!

  • Djomali Aimee says:

   Naona tunatofautiana lugha kidogo. Haijawahi kutokea Zaiko ya Paris hata siku moja na siwezi kuandika uongo kwani mimi ni mpenzi mkubwa na mwana historia ya huu muziki. Soma tena makala yangu, utanielewa vizuri. Mwaka 1988 wakati Zaiko iligawanyika kwa mara ya 4 katika historia yao watu wengi tulidhani ndiyo mwisho wao lakini Prezidaa Nyoshi El Saadat (natania tu, Nyoka Longo) alikuwa imara aliibua vipaji vya hajabu mpaka kina Lengos walionekana kutokuwa na maana kwani nafasi zao zilizibwa kisawasawa. Katika upande wa solo nafasi za kina beniko xilifunikwa na kina shiro mvuemba, baroza, na Mze mzima Ya Mbuta Matima mwalimu wa walimu (RIP). Mwaka 1989 Zaiko ikaja juu sana kwa kishindo cha hajabu lakini kipindi hiki nayo wenge ilikuwa tayari imeshakubaliwa Kinshasa na public ya huko na mwaka huu wa 90 na 91 wenge ikawa bendi bora Zaire/Congo. Ifuatayo ni list ya bendi bora kipindi Zaiko inakuha juu. 1988 Bozi na Anti Choc (Clan Zaiko Langa Langa)
   1989 Choc Stars (Clan Zaiko Langa Langa)
   1990 Wenge Musica BCBG TOUT TERRAIN
   1991 Wenge Musica BCBG TOUT TERRAIN
   1992 Zaiko Langa Langa
   1993 Pepe Kalle na Empire Bakuba
   1994 Koffi Olomide (Zaiko Langa Langa)
   1995 Zaiko Langa Langa
   2000 Zaiko ilitunukiwa kuwa bendi bora ya karne
   2010 Zaiko ilitunukiwa kuwa bendi bora ya miaka 50 ya muziki wa Congo, hivyo Prezidaa Nyoshi yuko anaandaa dozi mpya na ndiyo maana anaitwa Mze wa dozi ama Vieux Bombas! Na ni Zaiko ndiyo bendi pekee katika historia ya Congo ndiyo imechukua ubingwa mara nyingi zaidi.

   • Jumapili Innocent says:

    Ni kweli, Zaiko ndiyo baba wa muziki huu unaotamba sasa lakini pia kuna ma orchestre mengine zinapiga muziki safi kama kwa sasa Werrason na Vijana wa sasa na Zaiko pia inakuja juu kwa sasa baada ya kurudi Belgium.

 6. phinias biseko says:

  napenda sana habari za wanamuziki wa congo,muendelee kubishana ili tupate habari zaidi.binafsi napenda muziki wa congo balaa.naomba muendelee mbele ndugu zangu

 7. phinias biseko says:

  muziki wa congo naamini ndo muziki bora wa mwafrika.ukisikiliza ngoma za pepe kalle kama full option,dont cry dube na ile album kali ambayo mpiga solo lofombo na wenzake wa empire bakuba walikandamiza,ni albam nzuri balaa.hiyo album ni moto na haiwezi kulinganishwa na vibendi vya majibenique au mawerasonique.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: