Soyons Serieux ya BCBG yaendelea kutesa Kinshasa

Tangu kutoka albamu ya Wenge BCBG ya Soyons Serieux imeendelea kutesa mitaa ya Kinshasa.

Kwa mujibu wa mtandao maarufu na unaoaminika wa Digital Congo albamu hiyo bado inatesa kwenye mauzo, kupigwa mitaani kwenye radio na hata kwenye sherehe. “albamu hii inanyimbo nyingi nzuri na zenye mvuto na kupigwa kifundi ambazo yeyote mpenda muziki hawezi kuacha kuzisikiliza hivi karibuni…” ilisema sehemu ya habari hiyo.

Hayo pia yamedhihirika hata upande wa pili wa Mto Congo yaani Brazaville ambako JB na kundi lake la Wenge wanapendwa zaidi, amekuwa akipata mialiko mingi ya huko na kila mara kupata interview za magazeti ama radio na hata kwenye vituo vya luninga. hii ni kuthibitisha jinsi gani kazi ya Binadamu Mukullu Papaa Cherie inavyokubalika.

Habari hiyo imemalizikia kwa kuwakaribisha wapenda muziki kwenye show ya BCBG kwenye kiota chao cha Crystal Club leo jumapili kilicho kwenye barabara ya June 30 kupata burudani mwanana. Nakuacha na kibao Bologna ambacho binafsi nakipenda sana ambacho kiko kwenye albamu hiyo ya Soyons Sirieux. Jumapili njema waungwana

2 Responses to Soyons Serieux ya BCBG yaendelea kutesa Kinshasa

  1. peter says:

    Papaa Pius hii album hapa kwetu Bongo imekuwa kitendawili hata kwenye studio zetu haipatikani!! Mimi ni mnazi mkubwa wa BCBG nazipata kwa shida sana hizi album latest za KIN!! HUU NI MTANDAO MKUBWA WA MUZIKI BARANI AFRICA SISI WADAU TUNAITAFUTA HIYO ALBUM KWA UDI NA UVUMBA!!! NI KITU CHA NGUVU nawashangaa Ma DJ wa bongo!! Hii album si mchezo ni BAAAAAALAAAAAAAAAA!!!!!

  2. lots of good information and facts and inspiration, each of which I need, due to offer you such a beneficial info right here.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: