Heritier Watanabehuenda akatimuliwa Wenge Musica Maison Merre

Mwanamuziki Heritier Watanabe wa WMMM

Mwanamuziki nguli na mwenye sauti ya Radi Heritier Watanabe toka kundi la Wenge Musica Maison Merre WMMM linaloongozwa na Grand Tata Werasson Ngiama Makanda anaweza kutimuliwa kundini.

Watanabe ambaye siku za karibuni amekuwa akigonga vichwa vya habari hasa baada ya kurejea kundini mwanamuziki wa siku nyingi wa kundi hilo Japonaise na kupewa uongozi. kumekuwa na vita ya kugombea madaraka kati ya Japonaise na Watanabe na kwa kiasi fulani Watanabe ambaye tangu awali anatabia ya utukutu amekuwa haheshimu ratiba za mazoezi, anagombana na wenzake kwenye kundi na hata kiongozi mkuu Werasson amekuwa hamsikilizi kilisema chanzo cha habari hizi.

Watanabe ambaye wiki mbili zilizopita aliachwa na bendi yake ilipokwenda kutumbuiza Muanda huko jimbo la Bas- Congo ikiwa nai adhabu baada ya kupayuka kwenye vyombo vya habari kuwa kuna upendeleo kwenye kundi lake na ye kuona kama hatendewi haki. Habari pia zimesema mwanamuziki Mwingine Papii Kakol aliwahi kupata adhabu kama hiyo pale alipoonyesha utovu na nidhamu wakati wa mazoezi ya “Zamba Playa” ni baada ya kukwaruzana na Wata, Wajuzi wa mambo wanasema kutoonekana kwenye show ile na hata juzi jumapili kwenye Show ya Kisenso hakuwepo inawezekana ndio byebye.

Mgogoro wa uongozi ambao washabiki wanauhusisha na matajiri ambao wanauhusiano na hasimu mwingine Koffi Olomide ambaye awali alikuwa rafiki mkubwa wa Werasson na sasa yuko kambi ya Jb Mpiana, habari zinasema kuwa Watanabe anachochewa na watu wa nje asikubali kuwa chini ya Japonaise  ambaye tangu arejee kwenye bendi baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miaka kumi amekuwa gumzo kila bendi inapopiga.

Advertisements

3 Responses to Heritier Watanabehuenda akatimuliwa Wenge Musica Maison Merre

  1. Hadj le Jbnique says:

    Hili nililitabiri toka mwanzo niliposikia Japonaise anarudishwa maison mere na kwamba eti anakuja kuwa chef d’orchestre nafasi iliyokua chini ya pappy kakol akisaidiwa na wata kwa karibu,katika hali ya kawaida nilijua tu si rahisi kukubaliana katika hilo,Na sijui Papy kakol na mdogo wake Herritier wata waligombea nini kama kweli waligombana maana huwa ni marafiki wakubwa pamoja na Abraham wa bcbg,wamejuana kabla ya maison mere na bcbg,wanashare mambo mengi sana

    hebu tumkumbuke watanabe kidogo akiwa na maison mere live hapa….

  2. Estoy entusiasmado de encontrar webs donde ver informacion tan necesaria como esta. Gracias por poner este post.

    Saludos

  3. if you always use your swimming pools, you will need to use some quality pool cleaner a lot“

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: