Tangu kutoka albamu ya Wenge BCBG ya Soyons Serieux imeendelea kutesa mitaa ya Kinshasa.
Kwa mujibu wa mtandao maarufu na unaoaminika wa Digital Congo albamu hiyo bado inatesa kwenye mauzo, kupigwa mitaani kwenye radio na hata kwenye sherehe. “albamu hii inanyimbo nyingi nzuri na zenye mvuto na kupigwa kifundi ambazo yeyote mpenda muziki hawezi kuacha kuzisikiliza hivi karibuni…” ilisema sehemu ya habari hiyo.
Hayo pia yamedhihirika hata upande wa pili wa Mto Congo yaani Brazaville ambako JB na kundi lake la Wenge wanapendwa zaidi, amekuwa akipata mialiko mingi ya huko na kila mara kupata interview za magazeti ama radio na hata kwenye vituo vya luninga. hii ni kuthibitisha jinsi gani kazi ya Binadamu Mukullu Papaa Cherie inavyokubalika.
Habari hiyo imemalizikia kwa kuwakaribisha wapenda muziki kwenye show ya BCBG kwenye kiota chao cha Crystal Club leo jumapili kilicho kwenye barabara ya June 30 kupata burudani mwanana. Nakuacha na kibao Bologna ambacho binafsi nakipenda sana ambacho kiko kwenye albamu hiyo ya Soyons Sirieux. Jumapili njema waungwana