Porte Monnaie ya Ferre Gola

Ferre Gola alikuwa mwanamuziki wa Kwanza kabisa kuwa Recruited kwenye bendi ya WMMM baada ya kutemwa kwa JB Mpiana na inasemekana alikimbizwa na Aimelia Lyase Doming’ong’o, alipofatwa alisema ni sawa anajiunga lakini baadaye walipofanya interview na mtangazaji mahiri Zakarie Bababaswe alikaririwa akisema kuwa naye anampango wa kuja kuanzisha bendi yake, inasemwa kuwa habari hizi hazikumfurahisha sana Boss wake mpya Werrason na wakati wamekwenda kwenye show ya Zenith Werra ilibidi atoke na Ferre ili waongee baada ya kuona Ferre kama anajitenda na yuko busy sana na simu yake.

Ingawa alikaa na wakatoa albamu ya kwanza bado kiu yake ya kujitenda iliendelea na baadaye alikuja kutoka kivyake, huku wakigombea “wateja” na Fally Ipupa bado nafasi ya Ferre kwenye soko la muziki ni kubwa ukilinganisha na wenzie ambao walitoka wenye makundi yao.

Ferre  Gola amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi hasa kwa nyimbo zake za taratibu zimebamba mno, rafiki yangu Ally Juto aka Ally Tandika, Ally Magari Ally Mapicha anampenda sana huyu bwana, naomba ijumaa ya leo nikuache na kibao Porte Monnaie kibao hiki kilinde utulivu wako ijumaa ya leo.

Advertisements

One Response to Porte Monnaie ya Ferre Gola

  1. Anonymous says:

    Ferre ni balaa watupie watu live ya album mpya BOITE NOIR,ndo watamjua ferre ni nani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: