Maisha Plus 2012 yaendelea na usaili mikoani

Kipanya, Kaka Bonda na Mwanahamisi redioni

Kipanya, Kaka Bonda na Mwanahamisi redioni

Dada Mwanahamisi anaongea na vijana kuhusu umuhimu wa kutunza chakula

Dada Mwanahamisi anaongea na vijana kuhusu umuhimu wa kutunza chakula

Team iliyojitolea kuingia msituni kutafuta vijana watakaoingia kijijini (2)

Team iliyojitolea kuingia msituni kutafuta vijana watakaoingia kijijini (2)

 

Baada ya kukamilisha usaili Dodoma, Kahama, Kagera,Singida, Mwanza, Morogoro, Iringa sasa usaili unaelekea mkoani Mbeya ambapo utafanyika Sept 15 .

Crew nzima ya Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula inayodhaminiwa na banki ya NMB na Oxfam baada ya hapo itaendelea na safari kutoka Mbeya moja kwa moja mpaka Kilwa, ambapo itafanya usaili Septemba 17, kesho yake yaani Septemba 18 usaili utaelekea Masasi mkoani Mtwara.

Septemba 20 itakuwa zamu ya Wanzanzibar kusailiwa katika kumpata mwakilishi wa Maisha Plus kisha timu itarejea Dar tayari kwa usaili ambao utafanyika Septemba 22 na 23.

Kitakachofuata baada ya usaili wa Dar ni kipindi cha Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula kuanza kuonekana kwenye runinga yako. Usikae mbali na TBC1 kwasababu ndiyo itakayokusafirisha nchi nzima ukiwa kwenye sofa lako nyumbani.

Kubwa kuliko

Wakati usaili ukiendelea mikoani nchini, Huko nchini Burundi nako usaili wa kuwapata washiriki wawili ulikuwa unafanyika kwa maana hiyo safari hii shindano la Maisha Plus litakuwa na washiriki kutoka huko.

Huu ni mwanzo wa shindano hili wa kuzishirikisha nchi zote za Ukanda wa Mashariki ya Afrika.

Kwa wakazi wa Dar fomu za ushiriki zinapatikana katika duka la Masoud Kipanya lililopo Millenium Tower, Kijitionyama. Unaweza kupata usaidizi ka kupiga namba hii 0717 710303.

Usikose kupitia hapa kila mara kwa ajili ya updates za kipindi chako kizuuri kabisa cha Maisha Plus.

One Response to Maisha Plus 2012 yaendelea na usaili mikoani

  1. Chesco kagali says:

    Napenda kuwapongeza team zima ya maisha plus kwa kuvuka mipaka ya ardhi ya TZ na kujaribu kushirikisha tamaduni nyingine, hii italeta changamoto kwa wenyeji na kujifunza tamaduni nyingine.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: