Amour ya Dalila: Kolabo ya Koffi na Celeo iliyonogesha uhasama wa Koffi na Werrason

Werason na Celeo Scrarm Walikutana kwa mara ya kwanza kwenye msiba wa Madilu System tangu Celeo alipoondoka kwa WMMM. Inakumbukwa walipoanza WMMM wakati huo Walikuwa Didier Masela, Adolphe Dominguez, Ferre Gola, Baby Ndombe, Seseli Adjani, JDT Mulopwe, Celeo Scram, Bill Kalondji, Serge Mabiala, Didier Lacoste, Lay Chou, Michael Shendu, guitarists Flam Kapaya (solo), Japonaise Maladi (rhythm), Christian Mwepu (bass), drummers Papay Kakol and Ali Mbonda.

Baadaye Celeo Scrarm aliamua kuondoka kivyake na mpaka sasa anapiga kivyake. Katika Kolabo hii ambayo amefanya na hasimu mpya wa Koffi ambaye awali walikuwa marafiki wakubwa imeonyesha kipaji cha wote wawili. Wakati JB Mpiana akiwa kwenye kaa la moto na Werrason Koffi alikuwa upande wa Werrason na wote wawili walikuwa wakifadhiliwa na Pendejee Didie Kinuani.

Koffi anajulikana kwa kutengeneza Video Bora huku Celeo akielezwa ni muongozaji na mchaguaji location za kufanyia Video Shooting mzuri, sikiliza huu wimbo na angalia ubora wa kazi pia kisha nipe maoni yako.

2 Responses to Amour ya Dalila: Kolabo ya Koffi na Celeo iliyonogesha uhasama wa Koffi na Werrason

  1. mama nzawisa says:

    Celeo yuko juu na pengo lake wmmm hakuna atakaeliziba hilo halina ubishi,lakini mwisho wa siku maisha lazima yaendelee na watu wapya lazima wapate nafasi ya kutoka nao zinapopatikana nafasi kama hizi za kuondoka kundini kwa manguli wa aina ya celeo scram ndio mana leo tunawaona watu kama Abraham mignon baada ya kuondoka mpela afande bcbg na pia mtu kama Heritier wata kwa wmmm

  2. Aman Misana says:

    Werasson atamkumbuka daima Celeo maana pengo lake lilimuuma sana na alikuwa hajajiandaa kabisa, hongera kaka kwa kazi nzuri

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: