Wenge Musica Maison Mere – Prince Au Congo

Kiukweli kila ninapoulizwa mapenzi yangu kwa Werasson Ngiama Makanda huwa moja kwa moja narudi kwenye albamu hii ambayo kwangu mimi huwa ni Albamu ambayo naikubali sana.

Niilikubali sana hii albamu kabla sijaujua mgogoro wa Wenge vizuri, lakini baada ya kuusoma kwa ndani utagundua hapa Werrason alikuwa na kikosi kilichokuwa kimetimia sana.

Watu wengi walitaka kuonyesha vipaji vyao, Ferre, Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya ni baadhi ya majina ambayo yaliibeba sana ngao ya WMMM, Posti hii ni kwa heshima yako Pius Mikongoti Jr aka Mlala ambaye najua unampenda sana huyu bwana, anyway nilimpenda JB ili kujitofautisha na bwana huyu kwa vile tumefafa hadi majina hahahahaaa . Ukitaka kujikumbusha wote walivyokuwa recruited bofya hapo chini.

SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – IV

Kuzaliwa Kwa Wenge Musica Maison Merre (WMMM) na miaka yake mitatu ya Mwanzo

image

Baada ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko kadhaa leo tunaitazama Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, shukrani za kipekee ziwaendee watu hawa wafuatao kwa kufanikisha kuisimamisha Wenge Maison Mere kwa namna moja ama nyingine:

Wa kwanza ni mtu mmoja anaitwa Sankara De Kunta, huyu mtu alijitoa sana kuwasaidia kina Werrason kujijenga,jamaa alikua na kazi moja tu, kuwachafua Jb mpiana na Koffi Olomide na kumpandisha na Kumsifia Werrason, na kwa kweli alifanikiwa sana, jamaa alikua na vituko huyu hapa nafasi haitoshi, lakini aliipromote sana maison mere na hasa werrason binafsi, ilifikia wakati Tata Sankara ambae awali alikua mnazi mkubwa wa Adolphe Dominguez tangu enzi za wenge musica original alikua akipita mitaani huku akiimba Balingaki Baboma Werra eeeeh! akimaanisha wanataka kumuua werra, akiwataja mahasimu wa Werrason,alikua akiimba kwa style ya aina yake kiasi cha kuwafanya wengi wamuonee huruma sana Werrason wakidhani pengine ni kweli Werrason yuko hatarini kuuwawa kumbe ulikua usanii wa Tata Sankara.

image

Mtu mwingine nyuma ya mafanikio ya mwanzo mwanzo ya maison mere ni Zackarie Bababaswe, yeye pia alisaidia sana kuwa promote maison merre kupitia shows zake mbalimbali lakini na yeye pia akiitumia nafasi hiyo hiyo kutengeneza pesa binafsi, si unajua tena strategy maarufu ya “helping the weaker to overcome the stronger” halafu baadae na wewe unanufaika na hiyo strongness ya uliemsaidia.

Pia mtu mwingine aliewasaidia sana kina Werra kujijenga maison mere ni kiongozi wa wenge el paris Marie Paul, huyu aliwasaidia kutokana na connection yake na Werrason binafsi. Werra na Marie Paul wanatoka kijiji kimoja, pamoja na Reddy Amisi, pamoja na King Kester, lakini kwa sasa Werrason na hawa ndugu zake hawaongei wala kusalimiana, hali ya mahusiano miongoni mwao imekua ikilegalega kadri siku zinvyosonga mbele hasa kati ya Werrason na Marie Paul kiasi cha Marie Paul kutohudhuria hata mazishi ya baba yake Werrason miezi michache iliyopita. Msaada mkubwa ambao Marie Paul aliipatia maison mere kutokana na connection yake na werrason ni kuwaambia mashabiki wake na Wenge El Paris kiujumla wote wampe support Werrason na bendi yake na pia akawapa Maison Mere wanamuziki wake wawili, JDT Mulopwe na Manda Shante ambae baadae alijitoa hata hivyo (Kwa wasiomjua Manda Chante ni yule mwenye sauti kali kweli wimbo wa Kalay Boing wa Wenge Musica BCBG enzi hizo.

Wera na madai ya Nguvu za giza.

Pia habari za chini ya kapeti zinasema Marie Paul pia alimpa Werrason “Nguvu Zake” ambazo zinaelezwa kuwa ndio chanzo cha chuki za hali ya juu miongoni mwa watu hawa kutoka kijiji kimoja, kwani inaelezwa kuwa Werra badae hakurudisha “nguvu” hizo alizopewa kama walivyokubaliana, hapa sitaki kuingia sana lakini kwa congo hayo ni mambo ya kawaida sana. Kwa mnaoelewa Lingala mkisikiliza vizuri hapo chini kwenye video hiyo mtamsikia mwenyewe Marie Paul akiyaelezea hayo mambo ya “nguvu zake” anazozililia kwa Werrason, alijaribu kukwepa kwepa lakini mtangazaji akambana kwenye kona mpaka akafunguka. Msikilize mwenyewe hapo “Le Roi Pele” Marie  Paul anavyosema

Msikilize Marie Paul akiongelea mambo kadha wa kadhaa humu

Inasemekana nguvu hizo zinatoka kijijini kwao tu ,zilimtoa King Kester enzi zile za “kidengune”nadhani wengi mnakumbuka alivyotamba, baadae Reddy Amisi nae akazitumia, halafu ikaja zamu ya Marie Paul nae ndio akampa Werrason.

Tukiacha mazungumzo hayo baada ya habari,sasa tuende moja kwa moja kutazama zoezi la kusaka wanamuziki kwa ajili ya kuisuka Maison Mere,nani alikua wa kwanza,nani alifuatia na waliwatoa wapi hao wanamuziki twende pamoja.

FERRE ajiunga na WMMM akiwa ni Mwanamuziki wa Kwanza kuwa Recruited

Kutokana na wanamuziki wengi wa WENGE MUZIKA 4X4 TOUT TERRAIN kuondoka na Kumfuata Jb Mpiana kama tulivyoona huko nyuma,Werrason,Didier Masela na Adolphe Dominguez wakatakiwa kujipanga upya kwa kusaka watoto wa congo wenye vipaji vya muziki waweze kuwa recruit,kazi haikua rahisi pia,kwanza walianza na Ferre Gola ambae alikua ana hang tu baada baada ya kukimbizwa na Aimelia Lyase “Demingongo” kule Bcbg,hivyo na yeye akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kujiunga maison mere baada ya waanzilishi hao watatu Werra, Masela na Adolphe.

Vita Imana ni moja ya Tungo HAI za Ferre Gola ndani ya WMMM inayotamba mpaka wa Leo. Wimbo huu Uliimbwa tena akiwa kivyake.

Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya wajaribiwa WMMM

Kutoka hapo official recruitment ikawa imeanza, baada ya Ferre ku join kundini mwanamuziki aliyefuatia kujiunga na maison mere ni Bob Lorenzo, baadae akaja JDT kama tulivyoona huko nyuma kwamba aliletwa na Marie Paul kutoka kwenye bendi yake ya wenge el paris ili kumsaidia home boy wake Werrason, halafu akaja Baby Ndombe alipitia kwenye mchujo na alifaulu kwa upande wa uimbaji na alifaulu majaribio pia kama mpiga bass, baadae tena rafiki wa siku nyingi wa werra toka enzi za wenge musica ambae pia alikua mdau mkubwa wa wenge muzica enzi hizo WASENGA KIMPUNI akawaleta vijana kadhaa kutoka BANDAL (wenge musica home town), vijana hao ni huyu Fally Ipupa Celeo na Mtaalamu wa solo guitar na music arrangement kiujumla Flam Kapaya ambao walikua wanapiga bendi moja ya mtaani huko Bandal, baada ya hapo akaja mpiga drums Maradona (the second ever true drummer wa iliyokuwa wenge musica original) ambae walijiunga maison mere kipindi kimoja na Papy Kakol ambaye yeye alitoka katika group ambayo Fally Ipupa wakati fulani alikua ndio atalaku namba moja wa hiyo group kabla ya kuanza kuimba, baada ya hapo akaja kijana mmoja mwenye kipaji cha hali ya juu, kijana ambae alikua ametokea katika bendi ya JOLINO iliyokuwa chini ya uongozi wa Rio Kazadi “Rio de Janeiro” ambae kwa sasa ni muimbaji wa bcbg, pia huko JOLINO ndiko alikotokea Chai Ngenge muimbaji wa bcbg pia, kijana huyo si mwingine bali BILL CLINTON.

Fally Ipupa Afanya Interview WMMM

Baadae tena Adolphe Dominguez akawaleta kundini SERGE MUBIALA na DIDIER LACOSTE wote walikuja kuibeba sana maison mere kwenye safu ya uimbaji, pamoja nao Adolphe alimleta pia mpiga kinanda Thiery Synthe, baadae Adjani nae akajiunga akitokea bendi ndogo ya mtaani, then akaja mpiga rythm guitar Kojack, baada ya hapo wakawajaribu tena mamia ya vijana wa congo miongoni mwao ni atalaku Brigade na muimbaji CHOU LAY (mtoto wa EVOLOKO) Lakini bahati mbaya Chou Lay hakuchaguliwa baada ya majaji kumuona Bob Lorenzo ni bora zaidi kutokana tu mvuto wa sura yake lakini hakua muimbaji mzuri kuliko Chou Lay, mwanzo tuliona Fally Ipupa akiletwa kwenye usaili, nadhani mtakua mnajiuliza ilikuwaje, je alifeli usaili?

Jibu ni kwamba hapana, hakufeli usaili, sasa kwanini hakujiunga? jibu ni kwamba Fally alijiondoa kwenye usaili mwenyewe kutokana na kuwa na mapenzi makubwa na Quartier Latin ya Koffi Olomide bendi aliyokua akiipenda toka akiwa bado kijana mdogo na kwa mujibu wa Willy Bula (kaka yake na Blaize Bula) anasema Fally pamoja na Bouro Mpela (mdogo wa Alain Mpela) walikua wakimsumbua mara kwa mara enzi hizo wakimuomba awaunganishie wapate nafasi ya kujaribiwa Quartier Latin ya Koffi Olomide ambayo yeye Willy Bula alikua mmoja wa wanamuziki huko, Bula baadae alifanikiwa kumshawishi Koffi awajaribu wadogo zake hao lakini baada ya majaribio Bouro Mpela ndio akawa wa kwanza kufaulu majaribio na kujumuishwa kundini huku Koffi akimwambia Fally aendelee kujifua na wao QL watakuwa wanafuatilia maendeleo yake na wakati mwingine kujumuika nae mazoezini na kwenye local shows za QL, hivyo Fally akaona asije akajiaribia mipango yake na Quartier Latin kwa kujiunga na Maison Mere,ndipo akajitoa kwenye usaili, nadhani kuna watu walimshauri asifanye haraka, aisubiri QL, hivyo basi Fally hatuwezi kumuhesabu kama ex-maison mere, hakuwahi kujiunga nayo japo alijaribu.

image

Hii ni moja ya Albamu ambazo zimefanya vizuri sokoni

Mpaka hapo bendi ikawa imekamilika na kuanza mazoezi,nini kilifuata,tuendelee kufuatana hapa hapa siku ya jumatano ambapo tutakamilisha miaka mitatu ya WMMM na baadaye tutaangalia walivyoendelea.

Huu ni mfululizo wa Historia ya Wenge Musica na kwa kuanzia tunajaribu kuangazia kilichopelekea JB Mpiana na Werrason kutengana na miaka ya mwanzo ya bendi husiki huku tukitazama kwa kina jinsi wanamuziki walivyopatikana na walioondoka na kwa nini waliondoka. Simulizi hiizi za kusisimua kwa wapenzi na wanafamilia wa Wenge ni za pekee na zitakujia hapa hapa kwenye Blog yako ya Spoti na Starehe.

Nawaacha na Kibao Heritier Itere toka kwake Werrason Ngiama Makanda, Hiki kilikkuwa katika Albamu ya Pentagone wakati huo wakifanya kazi pamoja.

Salamu zangu za dhati kwa Werasonique woote ndani ya Blog hii nadhani mmeridhika na habari za bendi yetu ya WMMM. Shukrani a kipekee kwa Papaa Henry Kasapira nakati ya londone, Juma Mukubwa Muzee ya Air Port, Le Big Prodyuza Maghambo tuko pamoja, Papaa Julie We Ston weeee Ndenge nini papaa?, Papaa Hadji Le Becebegeeque Nambari wan!! Uko Juu Papaaa, Mamaa Tabou Fatou ya Tanzanie weeeee Kitokoooooo, Papaa Farid Wa Muscat, Mamaa Perovee, Mukubwa Shabani, Papaa Mwalimu wa Muheza Waambaze Mgoshi?,  Sadik Titanike weeee, Alain Kamangu Merci Mingi papaa, Mamaa Fatuma Mtanga tuko Pamoja Meree, Samson wa Delila karibu sana, Mke Mimi nakati ya Ujiji Chighoma, Ubeleji na wachangiaji na Wasomaji wote tuko pamoja na Asante kwa support yenu, kwa wale wanaonitumia email na kunipigia simu pamoja sana najitahidi kujibu email zenu wote.

Merci Mingi, Till then…. Kama uko kwa Facebook basi ungana na page yetu kwa kubofya join/like hapo juu kulia basi utapata habari live kwenye notifications zako kila tunapochapisha kitu kipya.

Kama unaswali au maoni tafadhali niandikie piusmicky@yahoo.co.uk au nitwangie Hotline no. +255713 666616

2 Responses to Wenge Musica Maison Mere – Prince Au Congo

  1. After I believed about matters like: why this kind of details is without spending a dime right here? After you create a guide then a minimum of on promoting a guide you will get a percentage, because. Thank you and superior luck on informing people today far more about it.

  2. Rochel Hupka says:

    Reasonably sure he’ll possess a good study. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: