JOSE MOURINHO: KOCHA WA KWANZA KUCHUKUA MAKOMBE YA LIGI NA SUPERCUP KWENYE NCHI NNE ZA JUU KISOKA

August 30, 2012

 

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho ameendelea kuvunja rekodi mbalimbali katika ulimwengu wa soka, baada ya kuwa ndio kocha pekee aliyechukuwa ubingwa ligi kuu za nchi nne tofauti kubwa barani ulaya na vilabu vya Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid.

Usiku wa kumakia leo Jose Mourinho alikiongoza kikosi chake cha Real Madrid kuwafunga mahasimu wao wakubwa FC Barcelona bao 2-1 kwenye mchezo wa pili wa kogembea kombe la Supercup kwenye uwanja wa Santiago Bernebeu. Kwa matokeo hayo timu hizo zikafunga kwa jumla ya mabao 4-4, lakini kutoka na Madrid kuwa na idadi kubwa ya magoli ya ugenini wakatwaa ubingwa huo wa tatu tangu Mourinho afike Bernebeu.

Advertisements

%d bloggers like this: