Fally naye aingia Studio

Sawasawa Concert ya Fally Ipupa huko Kenya, nakuonjesha. Kwa sasa Fally ndiye mwanamuziki mwenye show nyingi nje ya Congo kuliko wote ma champions.

 

Baada ya ukimya wa muda Mwanamuziki Fally Ipupa amerejea Kinshasa akitokea jimboni Lubumbashi ambapo alikuwa na show kabambe huko, Kabla ya hapo Fally alikuwa nchini Zambia katika Jimbo tajiri la Copperbelt (Copperbelt Province,) ambapo alifanya tamasha kubwa la kusherehekea miaka 94 ya kuzaliwa Rais wa zamani wa Africa ya Kusini Nelson Mandela, tamasha ambalo lilihudhuliwa na viongozi kadhaa wa Africa ya Kusini akiwemo Balozi wake. Pia Fally na kundi lake watatumbuiza Kenya kwenye ziara ambayo bado inamashaka kwa mujibu wa mtandao wa Digital Congo.

Fally anarejea Studio kuendelea na Production ya Albamu yake mpya huku kazi hiyo ikikatizwa tena safari hii August 5 anatakiwa Zambia tena na baadaye atakwenda Angola na Tunisia, wachambuzi wa Muziki wa Congo wanabainisha kwamba Fally ndiye mwanamuziki anayeongoza kwa sasa kuwa na Ziara nyingi za nje ya Congo huku akiwa na ratiba ya miezi saba mbeleni tayari kwa show.

Ikumbukwe kuwa Fally ni mmoja wa wanamuziki wachache wakubwa wa Congo ambao hawana kinyongo na bifu na Bana Congoo (Le Combatent)  kundi la wanaharakati vijana wanaoishi nje ya Congo ambao hawakubaliani na utawala wasasa wa Congo DRC ukiongozwa na Rais Kabila, wanamuziki wengine Kama Werasson, JB Mpiana na Koffi wao walilazimika kufuta ziara zao nje ya Congo hasa huko Tshengeni ambako wanakuwaga na show nyingi kutokana na kufanyiwa fuo na makundi hayo jambo linalopelekea uvunjifu wa amani. FAlly naye ana toa albamu yake ambayo pia inatengenezwa kwa Producer mmoja na JB Mpiana pamoja na Werasson.

One Response to Fally naye aingia Studio

  1. Nga Haapala says:

    I surely enjoy every single very little little bit of it and I’ve you bookmarked to check out out new things of one’s weblog a have to go through web site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: