Dessert ingeta (Malewa 2) ya WMMM iko jikoni

Na Hadj Le Jbnique,Boston,Massachussets,USA.

Hayawi hayawi sasa  yanaelekea kuwa,baada ya zile danadana nyingi kwa takriban miaka miwili za kukamilika kwa sehemu ya pili ya album ya malewa ya kwao wenge maison mere wakiwa pamoja na mzee mzima Le Roi De La Forret WERRASON sasas kwa uhakika mzigo uko mbioni kuwa realeased ambapo mashabiki wa WERRA na wa muziki wa lingala kiujumla watapata nafasi ya kuisikiliza na hatimae kuicheza album hiyo ambayo itakwenda kwa jina la “DESSERT INGETA” sasa itakua na nyimbo 14 badala ya 10 zilizopangwa kuwemo awali.

Album hii ingeweza kuwa sokoni mapema zaidi kabla ya mwezi huu wa july 2012 lakini kukatokea matatizo ya kiufundi ambayo yalisababisha kufutika kwa kazi kubwa ambayo tayari ilikua imesharekodiwa kitu kilichowalazimu Bana Maison Mere kurejea tena studio kuweka sawa mambo kazi ambayo wanaendelea nayo mpaka muda huu naandika hapa ambapo kwa sasa  Heritier Wata ya Ngiama a.k.a. Heritier Watanabe pamoja na kina Eboa Lotin, Capuccino, Papy Kakol, Olivier na Japonais ndio wanaingiza sauti zao ndani ya  “DESSERT INGETA” na baadae kundi lote lwa waimbaji watafuatia kutia vocals zao humo,je album hiyo itamaliza ubabe wa album ya SAYONS SERIEUX “mpunda” ya wenge bcbg uliodumu sokoni kwa takriban 2 years now?ama kwa hakika hilo ni suala la kusubiri na kuona

Pata kitu “likambo” hapa kama utangulizi tu wa raha zitakazokuwemo ndani ya DESSERT INGETA”,Sikiliza Congo Rhumba hilo,kamata mamaa cheza  malinga nayee Taratibu eeeeh…ha ha haaaa!

6 Responses to Dessert ingeta (Malewa 2) ya WMMM iko jikoni

 1. edmas says:

  “je album hiyo itamaliza ubabe wa album ya SAYONS SERIEUX “mpunda” ya wenge bcbg uliodumu sokoni kwa takriban 2 years now?”

  HIVI HII ALBAM IMETAMBA LINI JAMANI? MTU UKIPENDA KITU, HATA CHONGO HUITWA KENGEZA.

 2. mwana congo says:

  Msipende ligi ya ubishi kwenye kila jambo,muandishi katung’ata sikio kuhusu ujio wa hiyo ingeta,cha muhimu kwanza ilitakiwa kuwapa pongezi wenge ya werason kwa kukamilisha album hii ambayo tumeisubiri sana kiasi ktk hali ya kawaida ya ushindani wa bcbg na maison mere ni wazi kwamba kwa muda wote tuliokua tukiisubiri hii album album latest kwa hizi bendi 2 shindani imekua ni sayons serieux ambayo ilikuja kumaliza ubabe wa malewa 1,so baada ya hapo sayons ndio ikawa inatamba tukishuhudia bcbg wakipata kazi nyingi nje na ndani ya congo ikiwemo ulaya kwa ajili ya sayons serieux,kama album hiyo haikujulikana kwenye mji au kijiji ulichopo wewe haimaanishi kwamba album hiyo haikua maarufu,tumeshuhudia concert nyingi sana toka mwaka juzi bcbg wakitamba na sayons serieux yao,u can google u tube zitakuja hizo ma concert kibao then utachagua na kutizama mapokezi ya hiyo album.All in all tujiandae kuipokea desert ingeta tuone nayo itakuwaje.

 3. Fatuma Mtanga says:

  NGOJA TUSUBIRI KUONA IKO KIMYA KINGI

 4. mama nzawisa says:

  Well said dada fetty mtanga

 5. Anonymous says:

  we jamaha muongo sn mulize jema hii nyimbo kitambo sio wabongo tunadanganyana sn mm gent usitudanganye bwana kwa nn usiandike kuhusu sikinde D juu ndege nn !! makuta

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: