Maisha Plus kurejea kwa kishindo

Kile Kipindi cha Reality Show cha Maisha Plus kinaendelea na safari hii kikiwa kimenogeshwa zaidi.

Akizungumza nami mtaarishaji na muanzilishi wa kipindi hicho Masud Kipanya amesema kuwa watu wengi walidhani maisha Plus imekufa lakini ilisimama kwa vile ilibidi mabadiliko makubwa yafanyike ili kuboresha “maisha Plus haikufa wala kuondoka isipokuwa tulisimamamisha mwaka jana ili tufanye maboresho ikiwa ni pamoja na kufunga Camera na mic za kisasa pale kijijini na kuboresha miundo mbinu zaidi” alisema Masoud.

Audition itaanza mwezi ujao na itaanzia Arusha na kuzunguka mikoa tofauti na hatimaye mwezi wa kumi washiriki wataingia kijijini rasmi. Aidha Masoud aliongeza kuwa umri ni kati ya miaka 21 na 26 huku akisema kigezo cha elimu ni kidato cha nne “age 21-26, elimu O’level, na ujue jinsi ya kuishi, Ukiwa na ujuzi wa ziada ni faida zaidi” alisema Kipanya.  Aidha Masoud ameongeza kuwa kipindi cha Maisha Plus kitarushwa na Television ya TBC ambapo kila kitu kimekamilika na atawajulisha mashabiki muda na wakati ambapo kipindi hiki kitakuwa hewani.

Kipindi cha Maisha Plus kimejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na mguso wa maisha halisi na tamaduni sio tu za Kitanzania bali za kiafrika zaidi.

Usikose kupitia Spoti na Starehe mara kwa mara ili upate updates za kuhusu kipindi hiki ambacho binafsi nakifagilia sana.

6 Responses to Maisha Plus kurejea kwa kishindo

  1. ndingi mwana nzeki says:

    mtanisamehe kwa commoent yangu,lakini kiukweli kipindi cha maisha plus kilikosa mwelekeo na ndio maana kikafa,tpia taarifa za uhakika zinaonyesha kuwa TBC ilikikataa hicho kipinda kuwa hakina tija kwao tbc wala public,na kipanya amekua akihaha kila tv ili kiweze kurushwa bila mafanikio,ingawa hawezi kukiri haya.any way yawezekana sasa tbc wamekubali ingawa nina mashaka.

  2. Anonymous says:

    MAISHA YA KANUMBA

  3. Veronica says:

    Nimemefurahishwa sana na kipindi hiki cha maisha plus kinachorushwa na television ya taifa tbc coz ni inafafanua maisha halic ya mtanzania am happy with that

  4. Admiring the time and effort you put into your website and detailed information you provide. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed material. Wonderful read! I’ve bookmarked your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

  5. Mittie Dike says:

    Its my fantastic pleasure to visit your blog site and also to get pleasure from your fantastic posts here. I like it lots. I can feel that you just paid considerably focus for anyone content articles, as all of them make sense and are incredibly handy.

Leave a comment