Uzoefu wangu ndani ya Ngorongoro Crater

 

“…kwa muj ibu wa muongozaji wetu anasema kuwa Wapo wanaoamini kuwa Ngorongoro Crater ndipo Safina ya Nuhu ilifikia (ili land) baada ya Nuhu kuijenga Safina kubwa na kuingiza wanyama wawili wawili kwani hata mabaki ya binadamu ambaye anaaminika ni wa kale kupita wote yalipatikana Olduvai Gorge ambayo iko ndani ya bonde hili…”

IMG-20120713-00147

Ni Asubuhi ya saa kumi na mbili alfajiri kwa mujibu wa simu yangu Blackberry Torch 9860 inaniambia ni nyuzi joto 12c ambayo ni baridi sana kwa sisi tunaishi jiji kama Dar es Salaam ambalo linatawa na hali ya hewa ya sentigredi 28 hadi 34c. Tukiwa na makoti tuko nje ya hoteli ya Impala ambapo tunasubiri magari ili kuanza safari ya mbuga ya kipekee duniani ambayo iko kwenye ajabu la nane la dunia la Kreta ya Ngorongoro. ni kundi la watu 14 ambao kwa pamoja  tulikuwa kukihudhuria mafunzo ya Mfumo wa Ufatiliaji na Matumizi ya Barcode ambayo yaliandaliwa na GS1 Global Office ya Belgium na kuratibiwa na GS1 Tanzania yaliyofanyika kwa siku tano jijini Arusha katika hotel ya Impala.

Nusu saa baadaye magari mawili aina ya LAnd Cruiser Hardtop yanaingia, moja ni lakawaida linaloweza kuchukua watu watano na jingine limefanyiwa mabadiliko na kuongezwa urefu wanayaita War Bus ambalo linaweza kuchukua watu nane mpaka tisa. kwa tabia yangu ya udadisi na kwa sababu napenda magari sana naamua kupanda Warbus ili nione uwezo wake na akam kuna tofauti yeyote, tunakaa watu tisa na dereva wetu anajitambulisha kuwa anaitwa Esau na kutuomba msamaha kwa kuchelewa kidogo kwa takribani nusu saa kwani safari yetu ilikuwa ianze saa kumi na mbili kamili, kwa vile kila mtu alikuwa na hamu ya safari ile nusu saa ilikuwa kama masaa matatu kila mtu alikuwa kanuna lakini huyu Bw. Essau kwa jinsi alivyo mkarimu tukajikuta tumemsamehe na safari inaanza.

Alituambia kuwa safari yetu itakuwa ya masaa matatu hadi manne unusu kutegemea na jinsi tutakavyo simama njiani kwani ni takribani kilometa mia mbili na hamsini mpaka Kreta. tunafika Karatu na hapo anatuambia inabidi tusimame kwenye tawi la Benki kwa sababu ya kufanya malipo kwani kule hawachukui pesa ila unatakiwa kwenda na risiti za benki ulizolipia tuu.

IMG-20120713-00123

Hili ni Tawi la NMB Karatu, jimbo la Mheshimiwa Slaa ambalo kila kitu hapa ni Chadema tuu, tunasimama na kupata Supu nyuma pembeni ya Tawi hili na kisha tunaamua kununua mashuka ya kimasai maana tunaambiwa baridi ni kali huko juu, kumbuka ni takribani meta 2000 juu ya usawa wa bahari.

Baadaye safari inaanza tena kuelekea geti la kuingia Kreta, njiani tunakutana na mandhari nzuri kwani kilometa kama 5 toka KAratu tunakutana na sehemu ambayo ndege wakubwa wanaohama toka Ulaya kukimbia majira ya Baridi wanakaa hapo na mwenyeji wetu anatuambia wanakaa hapo kwa miezi miwili ndipo wanageuza kurudi Ulaya.

IMG-20120713-00125

Mr Elibariki Mmari na Mr Oneil from GS1 Global baada ya Supu.

Geti la Kuingia Hifadhi

Baadaye tunafika geti la kuingia Mbuga ya Ngorongoro Kreta hapo inabidi ku park gari na kuonyesha karatasi za kulipia ambapo kuna karatasi nyingine wanapewa hapo na kuhakiki waliomo kwenye gari kwani ni hapo wanakagua malipo, wageni na wazalendo hulipa tofauti, Wageni hulipa USD 50 kwa mtu mmoja takribani elfu themanini, na kwa mzalendo ni Tsh. 1500/- tu, ila gari kama ni lina mzungu au mgeni yeyote asiye mtanzania hulipia Dola mia mbili (200 USD) na akama ni la wazalendo hulipia 20,000/- tu.

IMG-20120713-00133

Kutoka kulia Mimi, Tina, Oneil, Da Judy na Mdau wa Arusha

Safari ya kuingia Kreta yaanza na ara tunaingia getini tunakuta kundi kubwa la Nyani Barabarani huku wakilia kwa uchungu baada ya kusogea tunakuta Nyani mtoto amegongwa na gari na hivyo wenzie wanalia kama anavyolia binadamu hii ni tukio la kwanza naliona wanasikitika huku wakilia kwa kelele kubwa baadaye wanambeba na kusogeza pembeni huku wakimfuta damu lakini masikini ameshakufa, wakakasikrika na kutaka kushambulia watu mwenyeji wetu Essau anasema inabidi tuondoke maana wameshakasirika, tunaenda huku akiednelea kutuelezea tabia mbali mbali za nyani.

IMG-20120713-00135

Mama Nyani ambaye mwanaye aligongwa na gari akilia kwa uchungu

Anatuambia nyani aliyekuwa akilia kwa uchungu ni dume ambaye kwa tabia ili aweze kumrithi yule jike aliyefiwa ni lazima aonyeshe huruma aweze kukubaliwa kujamiiana naye tena kwani Bwana Essau ambaye ni mtaalamu wa Wanyamapori anasema kuwa Nyani ni kama binadamu pia hufanya tendo la ndoa kwa kujifurahisha tofauti na wanyama wengine ambao hujamiiana kwa nia ya kuzaa. Tunaendelea na safari huku kila mtu akijadili tukio lile na katika kona za kupanda vilima vikali Bwana Essau anatueleza kuwa huku huwa wanapatikana Tembo ambao wanapanda toka kwenye Kreta, wote tunashangaa maana ni muinuko mkali hawa tembo wanapandaje, anaendelea Essau “unajua Tembo wanakula chakula kingi sana, hadi kilo 200 za majani ambayo wakati mwingine inabidi atumie muda mwingi kule chini huku juu anapata kwa urahisi na pia huu udongo wa juu una chumvi ambayo wao huipenda sana” kiukweli haikuniingia akilini kwani muinuko ni mkali hata kwa binadamu bado ni pagumu, tunakwenda hadi kufuka juu na kuona mandhari ya Kreta vizuri.

IMG-20120713-00139

Mandhari ni nzuri hapo tunakuta Askari wa Wanyamapori wakiwa na bunduki wakiachukua maemlezo tunaambiwa huyo ndio dereva ambaye amemgonga yule nyani mtoto na anatakiwa kulipa faini ya dola 200 na akirudia kosa kampuni yake inafutiwa kibali nafarijika walao kuwa watu watakuwa makini, kisha safari ya kuelekea Kreta inas=endelea bado ni safari inabidi kuzunguka mpaka kuteremka chini njiani tunakutana na akina dada wa kimasai wanapita takribani mita 50 na walipo tembo bila uoga na mbele tunaona Boma kubwa la wamasai pale tunaambiwa wanaishi na wanyama bila taabu mbele kidogo tunaona vijana wa kimasai wakichunga ng’ombe na pembeni kuna kundi la Punda Milia na kuanza kuwakimbiza Punda Milia.

IMG-20120713-00145

Kiukweli nafurahishwa na kila ninachokiona, mwisho tunafika geti la misho la kuingia Kreta, hapo napo inabidi ugongewe muhuri hivyo tunashuka tena na keewa masharti kuwa hatutakiwi kulisha wanyama, kutupa chochote iwe chupa za maji wala tissue paper kwani kosa lake ni faini au kifungu au vyote viwili.

IMG-20120713-00156

Safari naanza kushuka kiukweli ni slope kubwa mteremko mkubwa kila mtu amekaa kimya kwenye gari inahitaji udereva wa ustadi na kama ni mgeni unaweza kuliacha gari hapo ukarudi hahaha lakini Essau anatuonyesha ustadi mkubwa huku akituhadithia jinsi ajali mbali mbali zilivyowahi kutokea kwa kuteremka huko kwenye Kreta, kisha tunafika na kupokelewa na ubaridi fulani na kundi la Nyumbu waliokuwa wakila pembeni ya ziwa Magadi ambalo lina Flamingo wengi mnoo na kufanya eneo ziwa kuwa la rangi ya pinki.

Ngorongoro Crater na Imani ya Safina ya Nuhu

Mandhali ya Bonge hili yanavutia sio tu kwa wageni bali hata wenyeji sisi Watanzania ambao hatujawahi kufika, kwa mujibu wa muongozaji wetu anasema kuwa Wapo wanaoamini kuwa Ngorongoro Crater ndipo Safina ya Nuhu ilifikia (ili land) baada ya Nuhu kuijenga Safina kubwa na kuingiza wanyama wawili wawili kwani hata mabaki ya binadamu ambaye anaaminika ni wa kale kupita wote yalipatikana Olduvai Gorge ambayo iko ndani ya bonde hili, Esau anasema kuwa katika bonde hili la Ngorongoro wanyama wote wanapatikana ambapo yeye anadai walizaana baada ya kutoka ndani ya Safina  ya Nuhu baada ya Ghalika kuisha, Esau anasema hii ni imani ambayo baadhi ya wazungu wanakuja nayo na wanaamini inasemwa hivyo.

IMG-20120713-00168

Kuanzia hapo tuakaanza kufurahia uumbaji wa Mungu.

IMG-20120713-00173

Swala aina ya Thomson Gazelle.

IMG-20120713-00174

Thomson Gazzele wakila sambamba na Nyumbu mbele ya ziwa magadi

IMG-20120713-00177

Ngiri

 

IMG-20120713-00176

Kongoni

 

IMG-20120713-00179

Punda milia

IMG-20120713-00190

IMG-20120713-00193

Nyati ama Mbogo madume ambao wanasemwa kuwa wanahasira sana.

IMG-20120713-00194n

IMG-20120713-00195

Wakati tukiendelea kuwashangaa Nyati Essau anapigiwa simu na dereva mwenzie kuwa Simba wamekamata mnyama kwenye mto na tuanaaza safari ya kukimbilia huko kwenda kumuona Simba….!!! Inabidi kuvuka kijito kinachotitisha maji masafi meupe na kwenda upande wa pili wa mto kuanza kumtafuta Simba ambaye kwangu nilitamani sana kumuona kwa karibu, baada ya ka mwendo ka takribani dakika tano hivi tu tunaona magari yamezunguka na jamaa wamelala chini kimyaaa wametulia.

IMG-20120713-00216

IMG-20120713-00218

Simba wawili wakiwa wamelala pembeni ya gari.

IMG-20120713-00219

IMG-20120713-00197

IMG-20120713-00203

IMG-20120713-00204

IMG-20120713-00211

Haturuhusiwi kwenda kule mtoni lakini tumebahatika kuwakuta Simba wakiwa wamesogea barabarabi na kupumzika baada ya kazi ngumu ya Mawindo.

Kiukweli ni moment ambayo niliingoja kwa hamu sana kuona. Tunakaa hapo kama nusu saa na kuamua kuendelea na safari kuwatafuta The Big Five member wengine.

20120714-135330

20120714-135235

 

20120713_131614

Kiukweli safari ilikuwa nzuri sana na kuna mengi ya kuyaona tuliona Faru wanne ambao walikuwa mbali kidogo kwa vile nilikuwa nikitumia Camera ya simu haikuwa rahisi kuwazoom na kupata picha nzuri, kila mara wanyama wengine tuliwaona mbali mnoo na mwenyeji wetu Essaualijitahidi sana kutupa maelezo ya kutosha na ya kina, sio tu kwa wanyama bali hata kwa mimea ambayo angezani tulihitaji kuijua, Kwa wastani huna sababu ya kutokwenda kama una nafasi kwani kama nilivyosema mnaweza kujikusanya kama kundi na kwenda.

Prince Philip na Malkia Elizabeth walipovishania Pete

Pia alituonyesha mlima ambao unitwa Mlima wa Meza (Table Mountain), kilima hiki ambacho juu kimekaa kama meza, Essau anatuambia kuwa hapo ndipo Prince Philip alim propose Malkia Elizabeth na kwenda kuvishania pete Kenya, kiukweli sikuwa nalijua hili kabisa sikuhoji sana kwani nilitaka muda kujiridhisha nalo na bado nalifanyia kazi.

IMG-20120713-00220

Hapa wanapatikana Viboko Wengi mnoo kwa vile ni mchana na jua kali wengi wamo ndani ya maji.

IMG-20120713-00221

Tunapumzika na kupata mlo na kupiga picha za kujifurahisha kidogo.

 

IMG-20120713-00520

Lunch Box yangu.

IMG-20120713-00551

IMG-20120713-00223

Me and Carole toka GS1 Global ambaye alikuwa mwalimu kwenye mafunzo yetu, Carole ni Mmalay mwenye asili ya kichina ambaye kwa muda wote tulikuwa tukiongea kimalay na kunikumbusha mbali sana.

20120713_153032

Tunaendelea na safari na kisha muda unakwneda ni saa kumi jioni hivyo tunaanza safari ya kupanda juu ili turejee Hotelini kabla ya kuendelea na mambo mengine….

Tunapandisha gari zikiwa zimeongozana mara ghafla gari ya mbele yetu inasimama na dereva wetu anatuasa tuangalie mbele nashtuka kumuona Tembo kaziba njia ni Tembo mkubwa sana wako wanne na mtoto mmoja.

IMG-20120713-00559

IMG-20120713-00560

IMG-20120713-00561(1)

IMG-20120713-00561

IMG-20120713-00562

Kiukweli jamaa wanamkwara sana na kutisha mnoo lakini Essau anatutoa uwoga na kutwambia huyu tembo ambaye ana mkwaara ni Left Hand na gari yetu iko kulia kwake hawezi fanya kitu, tunashangaa amejuaje haya anatwambia kuwa unamuangalia Tembo meno yake moja linakuwa fupi na jingine refu kiliko jingine, hii inamaanisha ile fupi inatumika sana na huuo ndio unaashairia upande wa huyo Tembo, tulikaa takribani kama dakika kumi na tano tukisubiri wale Tembo wapishe njia ili tupite na ni zaidi ya gari 50 kila upande tukisubiria kwani muda wa kufungwa geti unakaribia geti hufungwa saa kumi nambili.

Baadaye gari zote zinawashwa na kupigwa race ambazo zinawatibua Tembo lakini baadaye walipanda kwenye muinuko na kuondoka na sisi kupita.

Kwa kifupi ni safari nzuri sana na unashindwa kuelewa ni kwa nini nchi yetu masikini namna hii…. Baada ya hapo tunaanza kurejea Arsuaha mjini takribani saa kumi na mbili unusu kagiza kameanza na ndio tunapita Karatu mara gari yetu inazima taa, dereva anapaki pembeni na kuangalia kulikoni bila kupata jibu, chokochoko zaendelea na muda wazidi kwenda ghafla giza nene na gari imegoma kuwashataa, linapita lori tunaashauriana kulifuata kwa kuangalia taa za nyuma bado tuko mbali sana na Arsuaha mjini, lakini mbilo zile zilidumu kama kilometa kumi tu lile lori likatuacha tukapaki tena porini.

Mara inakapita gari nyingine tukaanza kuifata lakini hatukwenda mbali ilituacha pengine ni kwa wasiwasi wa kufatwa na gari iliyozima taa, ikabidi tupaki tena tulienda hivyo mpaka likatokea gari jingine aina ya Noah na kusimama baada ya kuwaeleza kilichotusibu wakakubali tukuongoza kwa kuwasha taa za hazard na tulienda nao mpaka Arusha mjini Mungu mkubwa tukafika na kupumzika.

Gharama

Kwa uzoefu ni vizuri kutumia magari ya kukodi na dereva mwenye uzoefu kwani pamoja na udereva wangu kushusha gari kwenye Kreta si lelemama na pia hawa madereva wanajua wanyama wanapatikana wapi.

Kukodi gari toka Arusha mjini ni 400,000/- Kwa Land Cruizer inayoweza kubeba watu 5 mpaka 7. Hii inakuwa ni kwenda na kurudi, dereva wa kwao na mafuta juu yao pia.

Pia inabidi kulipia Lunch Boz ambayo inagharimu Tsh 12,000/= Ambapo kuna maji, Soda, Juice, Cake, na Chakula kingine.Hairuhusiwi kutupa kitu chochote mbugani hata ganda la ndizi, wala kulisha wanyama kwani hilo ni kosa na lina adhabu ya kifungo ama faini au vyote kwa pamoja.

Kwa Watanzania Gari kuingia Crater inalipa Tsh 20,000/= huku kila mmoja analipiwa Tsh. 1500/= na kama kuna raia yeyote wa kigeni basi Gari linalipiwa USD 200 na USD 50 kwa raia mmoja.

Hakuna malipo ya Cash, unatakiwa kulipia Karatu NMB Bank na kuleta Slip pale Getini au unalipa kwa VISA Card palepale langoni,lakini kuepuka usumbufu na ucheleweshaji ni bora kulipia kabla.

Usisahau….

Usisahau kubeba vitu vifuatavyo:-

 • Sweta
 • Camera
 • Kiona mbali kama unacho

Mawasiliano

Makampuni yote yana minara ndani ya bonde ingawa kuna baadhi ya sehemu signal kidogo zinapungua ama kupotea lakini unaweza ukawa connected na watu wako hata ukiwa huku kwa wale wenzangu na mimi una tweet na facebukisha anytime.

Ushauri wangu Kwenu

Ushauri wangu kwa Watanzania hasa vijana tubadilike na tubadili aina ya starehe kwani kua starehe kama hizi ambazo kama mta ji organise kama kundi inapendeza na gharamasi kubwa kama inavyofikiriwa.

Kwa anayemtaka Essau ambaye binafsi namkubali anicheki tu nitanisha naye.

13 Responses to Uzoefu wangu ndani ya Ngorongoro Crater

 1. Anold josephath says:

  Hongera mr umejifunza meng. safi sana unafaa kuigwa na jamii

 2. Mara ya kwanza kuona swahili post and this well done. Hongera. It was a great safari and everyone who reads this will want to go see the Ngorongoro crater. Keep priding in Swahili, soon it will be international.

 3. Aman Misana says:

  Mkubwa unatisha hii Review nimeipenda sana kiukweli umeandika vizuri mnooo.
  Nimeiprint ili niisome vizuri ni nzuri mno.

 4. Christian Maembe says:

  Kaka asante sana na kwakweli nimeipenda. Nikifika Bongo tu nadhani cha kwanza itakuwa huko, ila sijajua kama kwakipindi cha late November or early December kama ni kipindi kizuri kufanya hivyo. Please advice.

 5. piusmickys says:

  Bwana Christian hiki bado ni kipindi cha Utalii na kwa huku Ngorongoro kipindi chote ni kizuri kwani wanyama hawahami wamo ndani ya Crater tuu

 6. Anonymous says:

  Kaka Mkubwa nasubiri wajomba zako wafunge shule December twende nasi tukafaudu, kwa kweli mlifaudu sana, utanipatia namba ya simu ya Bw. Essau ili tuwe nae sambamba, Inshaallah!!!!!

 7. Musa Oswano says:

  Mkuu asante sana umenitamanisha inafaa uwe muandishi wa vitabu unajua sana kuandika, hii kitu imekaa njema dah kama na mi nilikuwa safarini unavyohadithia.

 8. a lot of terrific information and inspiration, both of which I want, because of supply this kind of a handy info here.

 9. […] Photo Credit: Bjørn Christian Tørrissen, David Berkowitz,  Jonathan Gill, Wikimapia.org, SpotiStarehe.com […]

 10. Collin Joseph says:

  Naomba kuunganishwa na kaka Essau

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: