Mpela Brothers wanakuja Kivingine

 

https://i2.wp.com/www.digitalcongo.net/UserFiles/Image/Musique/Mpela/mpela_alain_geco.jpgKwa mara nyingine tena wale ndugu wawili Allain Mpela aliyekuwa Wenge BCBG na Geco Mpela aliyekuwa kwa Koffi Olomide kwa pamoja wametangaza kila mmoja kurudi kwenye game kivingine na kila mmoja akiwa na albamu yake.

Afande Mpela yeye ndiye aliyeanza kutangaza nia kwa kuitangaza albamu yake ijayo inayoitwa Flèche empoisonnée (Mshale wa Sumu) na majuzi Geco Bouro Mpela ambaye alitamba kwa sauti nzuri na uchezaji wa madoido aliitangaza albamu yake itakayoitwa Bankoko.

Ndugu hawa waliwahi kutoka na albamu ya pamoja iliyoitwa Mortal Combat, mi niliipenda ila huku nyumbani haikujulikana kwani haikuwahi kupewa Air Time kabisa.

Kuna wakati Geco alitoka na single yake iliyoitwa intifada ambayo iliongozwa na kaka yake Allain Mpela ambayo kwa kiasi fulani ilikimbiza huko Congo na kwa mashabiki wa Congo Music kiujumla.

Tusubiri tuone ni nini kitakuja toka kwa ndugu hawa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: