Thomas Ulimwengu na wenzake wanusurika Kifo baada ya ndege yao kupata hitilafu.

Thomas Ulimwengu mbele kulia

Mchezaji Thomas Ulimwengu jana amenusurika kifo akiwa na wachezaji wenzake wakati ndege waliyokuwa wakisafiria ilipokorofisha na kuaacha njia na kufakamia pori.

Ulimwengu ambaye alikuwa na wachezaji wenzake walikuwa wakitoka mji unaitwa Kashobwe kurejea Lubumbasi walipatwa na maswaibu hayo wakati ndege yao iliposhindwa kuruka, “Dakika chache zilizopita kungeongelea mambo mengine labda ningeitwa MAREHEMU au ningekua hospital….NIKO NDANI YA NDEGE MM NA WACHEZAJI KAMA KUMI NA TANO NA VIONGOZI NA MAKOCHA NDEGE IMEACHA NJIA NA KUINGIA VICHAKAN N BAADA YA KUSHINDWA KUPAA…’MUNGU MKUBWA” alisema Ulimwengu kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Spoti starehe iliwasiliana na Ulimwengu ambaye alithibitisha habari hizo na kusema kuwa “ni kweli Bro tulikuwa tulikua tunatoka sehemu moja inaitwa kashobwe tunaelekea Lubumbashi ndipo ndege ikagoma kuruka na kuingia vichakani”. alisema Ulimwengu na kuongeza kuwa aliingiwa na hofu kubwa ila anamshukuru Mungu kwa sasa amerejea kwenye hali nzuri kiasaikolojia.

Pia nilimuuliza kama ni ile ndege mpya ya TP Mazembe akaniambia hapana ilikuwa ni ndege nyingine ila ni ya TP Mazembe. Thomas Ulimwengu yuko Kongo akichezea timu ya TP Mazembe na tunashukuru Mungu umepona na uko salama.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: