Sauti za Busara kuwakutanisha JB Mpiana na Werrason

IMG-20120627-WA000

Kwa mara ya kwanza Tamasha la Sauti za Busara mwakani litawakutanisha wanamuziki wakongwe wenye uhasimu mkubwa kimuziki JB Mpiana na Werrason.

Kwa mujibu wa mtandao wa Digital Congo waandaaji hao wameamua hivyo baada ya kuona muziki huo ni mmoja wa ladha zinazokubalika sana barani Afrika na hivyo kuamua kutanua wigo wa vionjo ili kuleta ladha kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwezi wa pili wa mwaka.

“Extra Musica, JB Mpiana, Werrason, Fally Fally ni miongoni mwa wanamuziki ambao waandaaji wanatarajia kuwaita” umesema mtandao huo. Waandaaji wameonyeshwa kusikitishwa kwao na ushiriki mdogo wa wanamuziki kutoka Congo huku wakiwataja wanamuziki wachache kama Freddy Massamba, Samba Mapangala na Virunga and Super Mazembe kuwa ndio waliowahi kushiriki tangu kuanzishwa kwa Tamasha hilo, uliongeza mtandao huo.

Waandaaji watapitia maombi na vikundi vyote kujua pamoja na mambo mengine kama muziki wanaopiga ni wa kiafrika, kama kazi ya msanii husika ni orijino ya kwake, umaarufu wa mwanamuziki au kundi kwa watanzania, pia wataangalia kama hawatahitaji pesa nyingi kulingana na bajeti ya waandaaji, kulingana na matakwa hayo na mengineyo tutajitahidi kuwaalika wanamuziki wote maarufu wa Kongo kama Extra Musica, Staff Benda Bilili, Konono No. 1, Kasai All Stars, musicians Fally Fally, Werra Son, JB Mpiana na wengineo ambao tunategemea wanamuziki na watanzania mbali ya kujifunza wataburudika pia, ilisema ripoti ya waandaaji.

Advertisements

4 Responses to Sauti za Busara kuwakutanisha JB Mpiana na Werrason

  1. K'Odero says:

    Hii kwa hakika itakuwa Bombshell!!

  2. edmas says:

    Hapa ndipo Werason atakapomgaragaza JB mbele ya macho ya waTZ

  3. Anonymous says:

    Wataimba pamoja na sio mashindano ya nani zaidi kaka Edams

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: