JB Mpiana na Werasson “macho kwa uso” kwenye msiba wa Mcheza show wa Wenge BCBG Monica Celes

IMG-20120627-WA000

Werasson Ngiama Makanda wa Wenge Musica Maison Merre akiwa na Papaa JB Mpiana wakijadili na kufatilia jambo kwenye msiba wa Mcheza Show mahiri wa Wenge Musica Monica Celes aliyefariki wiki iliyopita. Monica atakumbukwa kama mcheza show na kiongozi wa wanadada ambaye JB Mpiana alimpa kazi ya kumlea Mwana Nchuka, kale katoto kalikojiunga na Wenge kakiwa kadogo sana mpaka sasa amekuwa mdada.

Habari zinasema watu walilipuka kwa mayowe alipoingia Werasson msibani na wapambe wake na alijumuika na waombolezaji na kushiriki mpaka mwisho.

JB alimlilia sana Monica kwani ni mmoja ya wakongwe katika bendi ya Wenge Musica.

Shukrani za kipekee kwako Papaa Julie Weston Le Carismatique Le Presidaa Bana Congolee na Darisalaaam.

Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu – Amen.

9 Responses to JB Mpiana na Werasson “macho kwa uso” kwenye msiba wa Mcheza show wa Wenge BCBG Monica Celes

 1. Anonymous says:

  Mungu aiweke roho ya marehemu Monica mahali pema peponi

 2. Papaa Julius says:

  Weka picha yake basi maana sie wengine hatumjui.

  • Hadj Le Jbnique says:

   Tizama video hiyo hapo juu kuanzia kwenye dk 0:50 utamuona dada mmoja kavaa vitu white kuanzia suruali mpaka kichwani pama jeupe anarap akianza kwa kusema “tata koko…” na pia kama unajua lingala utamsikia anasema “omoni monica lelo nayembi…” akiwa na maana unaniona monica leo naimba,huo ndio marehemu monica enzi za uhai wake akiwa bado dnacer wa bcbg,badae monica alifanywa kuwa mwalimu na mtahini mkuu wa wacheza show wa kike wa bcbg,pia monica amewahi kuondoka bcbg enzi hizo baada ya tiatic album na kujiunga na quartier latin lakini hata hivyo hakudumu sana huko akaamua kurejea yumbani bcbg ambapo hakuondoka tena mpaka kifo chake,na hii video ilikua ni single maalum ya wa bebee cherie(wacheza show wa kike wa bcbg ya papaa cherie)ambayo inapatikana mwishoni wa video ya anti terro.

 3. Anonymous says:

  Hiyo Picha ya Werra na JB ilipigwa siku ya msiba wa mjomba wake na Werrason sio mazishi Monica.

 4. Malik Kondo says:

  hivi huyu monica alikuwapo kwenye ile album ya TH – Toujours Humble? Na wale madada wawili kwenye ile album ya TH wako wapi siku hizi? Zambrotta pia yuko wapi? Haya maswali nakuuliza wewe Hadj Le Jbnique, mze wa dozi!

 5. Hadj Le Jbnique says:

  Ndio monica seles alikuwepo kwenye TH,Ukitizama video ya wimbo TH uliobeba jina la hiyo album kati ya wasichana watatu waliovalia sketi na blauzi za pink monica selea ni huyo alie katikati ya wenzake pembeni yake kulia kwake amesimama Nonoo Diamat-(Nonoo Diamond)ambae alitokea kwa koffi baada ya album ya Loi ya koffi ndio akahamia bcbg.Baadae pia koffi alilipa kisasi kwa kumchukua monica seles lakini badae monica alirejea nyumbani bcbg akatumika kidogo kama dancer then akaacha kupanda jukwaani na kuwaachia vijana kina zambrotta, virginie, tantine, yetsi, nina, ananancy, sandralima,chermaine,brinette(muana nsuka) andbeverly,blanche n.k. Monica seles akaenziwa na bendi kutokana na mchango wake kwa kupewa cheo cha choreographer(dancer recruiter and trainer)kwa tafsiri isiyo rasmi muajiri na mkufunzi/mwalimu wa madancer wapya yani bila monica kukupitisha hupati ajira ya kucheza show bcbg hata ujuane na jb.Cheo ambacho amekua nacho mpaka kifo chake.

  Nadhani nimejitahidi kujibu maswali yako kamanda.

 6. Malik Kondo says:

  Ahsante kwa dozi Mze au mkuu wa wakuu Hadj Le Jbnique. Swali lingine, wale madada wawili katika ile album ya TH wako wapi?

 7. At this time it appears like WordPress is the preferred blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

 8. I’m really loving the theme/design of your web site. Do you ever run into any internet browser compatibility issues? A small number of my blog audience have complained about my site not working correctly in Explorer but looks great in Firefox. Do you have any recommendations to help fix this problem?

Leave a Reply to Malik Kondo Cancel reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: