Ferre, King Kester,Jb Mpiana

Ferre Gola live on stage akiwaenzi kaka zake kwa kuimba nyimbo zao. Hebu tumtazame na kumsikiliza akimpa shavu rais Jb Mpiana ambae yeye mwenyewe mpaka kesho anamtambua kama ndio alikua rais na kiongozi halali wa wenge musica bcbg 4×4 tout terrain.

34 Responses to Ferre, King Kester,Jb Mpiana

 1. Anonymous says:

  “ambae yeye mwenyewe mpaka kesho anamtambua kama ndio alikua rais na kiongozi halali wa wenge musica bcbg 4×4 tout terrain”.

  HAPA UMEKOLEZEA CHUMVI KUTOKANA NA MAPENZI YAKO NA JB, NI VIZURI UNGEISAPOTI KAULI YAKO NA MISTARI YENYE USHAHIDI KUWA KWELI FERRE AMEONGEA MANENO HAYO.

 2. Mtu Wa Zamani says:

  Tunaipenda hii blog yako lakini kwa sababu unaegemea sehemu moja ya JB mpiana tunakerwa sana.. JB awe mkongolie, awe mfalme wa wafalme….awe Legend kama Zola,Zidane,Raul,Pele,Maradona, Franco,Ndomge Opetum…ama yeyote yule bila kumsahau wewe mwenyewe… wakati wao ulipitwa… Tuhudumie kisawa… Tupe habari na updates bila ya kubagua kuhusu wanamziki wote hata kama huwapendi !… Ni muhimu kwetu kujua jinsi wanavyoendelea wanamziki wa kikongo…Wacha pia kutupotosha wakati mwengine kwa kujihusisha na mwanamziki wako unaempenda JB Mpiana.

  Sisi pia tunampenda JB lakini tuangazie kuhusu Koffi,Werrason, Ferre Gola, Wazekwa, ahmedjan,Fally,Zaiko, Mama Tshala muana, Papa Wemba,Extra Musica kutoka pande zote mbili, Akina Marie Paul,Didie La Coste,. …Kizazi chote Kipya…kuwa Fair and transparent Blog yako hii itakuwa na ufuasi wa kushangaza ukkitilia mkazo fairness.. Itakuwa Maarufu zaidi kote duniani kama vile sasa Kulingana na utatifi Werrason Ngiama Makanda, Le phenomene, Igwe, Le Roite de la Forest ni mwana mziki maarufu Kote Ulimwenguni… tunajua bila kufanya Reserch ukiwacha kile wazungu wanaita favourizm, Pius utakuwa na umaarufu mkubwa.

 3. Anonymous says:

  Hata mm nakerwa sana na hii blog, kila ukifungua JB JB JB, wakati hatuoni jipya kutoka kwake wapo wengine wengi tungehitaji kujua wako wapi na wanafanya nini kama akina Blaise Bula, Alain Mpela, Alain Makaba, Tutu Caludji, Roberto Wunda Ekokonta, Adolphe Elongo Dominguez n.k.

  Kwa kusawazisha tu, Capitaine Benelux ni utunzi wa Alain Makaba, JB aliuimba tu kwa sehemu kubwa kama ilivyokuwa kwa nyimbo nyingi za Makaba, alipendelea JB kuziimba mfano: Cest Trop Tard Djenga (Kalay Boeing Album), Dizoizo (Pentagone), Barakuda (Titanic) n.k.

 4. edmas says:

  One of the best female dancer who was in Wenge BCBG and Koffi Olomide QLI has died.
  Follow this link for the video discussing the loss. May she RIP. Amen

 5. Anonymous says:

  nashukuru sana kwa maoni yenu wadau ili kufanikisha blog hii. lakini mbona pius anadokoadokoa kila mwanamuziki? au jb hamumpendi? kiukweli mi nasomaga habari za wanamuziki kibao nyie tu

 6. Hadj le jbnique says:

  Samahani kwa kuingilia kati,mdau unaesema capitaine de benelux ni ya prince sio ya jb,ina maana wewe unaweza kuwa unaijua wenge kuliko ferre gola?!unless kama na wewe umeingia ktk mkumbo wa waliotangulia kucomment hapo juu kwa jazba bila kuitazama video husika na kumsikiliza ferre gola ambae mawerasonique huwa wanatuaminisha kwamba alikua ni mtoto wa de la forret werrason aliemleta wenge eti kwa lengo la kumfunika jb eti wakidai sauti ya ferre na ya jb zinalingana,ukiitazama video hii vizuri bila jazba utamuona na kumsikia ferre mwenyewe akimpa shavu jb kwa kutamka mkilingala kwamba tunaimba wimbo huu capitaine de benelux wa prezidaa jb,hayo ni maneno ya mtoto wa werrason-ferre gola. Endeleeni kubishana,mi nasign out kama ifuatavyo..

  • Anonymous says:

   Nadhani unakariri mambo ndugu yangu…. kwa ushahidi mdogo njoo hapa.

  • Hadj Le Jbnique says:

   wadau hizi nyimbi za wenge mkifuatisha wanavyoandika kwenye u tube mtachanganyikiwa sana kwa kuwa wenge kama kwa mnaoijua vizuri enzi zile kwenye audio cassete na video zao hawakua na desturi ya kunadika majina ya watunzi most of the time,hawa wanaozipost kwenye u tube hizo nyimbo si wa kuwaamini sana,bali mtu kama ferre ni wa kumuamini zaidi kwa kuwa yeye hao kina makaba na jb amefanya nao kazi kundini humo hivyo ni reliable source kwenye issue kama hii,ferre sio mjinga kusimama jukwaani mbele ya kadamnasi tena kinshasa na kuupotosha umma wote mle ndani na hiyo ipite hivihivi,how can you guyz believe someone anonymously ambae he/she was just post the video on tube na kujaribu kumuignore member halali wa wenge original tena mabae hakua close na jb kundini humo?!!!!!!!!!!!

   But huu ni mtazamo tu mnaweza kuchagua kumuamini “bwana muandishi wetu” wa huko u tube haina shida lakini kwangu members wa wenge original kwanza then ‘muandishi wetu” baadae,mabishano yaendelee na sign off kimtindo tena

   • Anonymous says:

    sehemu zote you tube zinzonyesha ni wimbo wa makaba, lakini wewe upofu wa mapenzi yako kwa Mpiana unaamini kila kitu kizuri ni cha mpiana, pole

   • Hadj Le Jbnique says:

    sio mimi ni ferre gola mzee ndio ametamka hadharani tena ndani ya kinshasa live bila chenga,sasa nikusikilize wewe kuliko ferre gola ambae alikuwemo kundini?hebu pima mwenyewe hapo halafu uone kama nakosea ama laa,tusipende kukariri tatizo mbongo akishaingiza kitu kichwani kukitoa ni ngumu sana

    msikilizeni ferre kuanzia dk ya 5:50 ya video hiyo anachosema ni kwamba tozo beta nzembo ya prezidaa jb akiwa na maana tunapiga nyimbo ya rais jb full stop sijaongeza neno hata moja mimi

 7. mwana congo says:

  Watu wa werason mnapenda sana kudeka na kujisononesha bila sababu,mnadai blogger kila siku analeta habari za jb tu lkn mnajisahaulisha kwamba wiki iliyopita blogger huyuhuyu katufukulia Alain konkou ambae wengi tulishamsahau,huko nyuma pia aliwahi kumfukunyua bivons gato na pia scola miel wa bozi boziana,wapi utaipata hiyo kama sio hapa ambapo leo mnanyea kambi kupaponda kila leo ni jb katajwa sio werrason kama jana,acheni hizo,acheni kudeka leteni album sokoni tutawajadili otherwise hamna album for 2 yearz bado mnataka muandikwe tu thats not fair bwana

 8. Hadj Le Jbnique says:

  msikilizeni ferre kuanzis dk ya 5:50 ya video hiyo anachosema ni kwamba tozo beta nzembo ya prezidaa jb akiwa na maana tunapiga nyimbo ya rais jb

 9. Anonymous says:

  Werrason haitaji kubebwa na Pius, he is the most famous musician in Congo right now, Dunia inajua na Pius anajua!

 10. Anonymous says:

  Eti alikuwa rais halali, kumbe wenge kulikuwa kuna rais mwingine ambaye hakuwa halali? Hahaha!

  • Anonymous says:

   yupo mmoja sitaki kumtaja kwa kuogopa fitna yeye alikua cashier tu lakini watu wake humu wanalazimisha ionekane alikua kiongozi na kichwa cha wenge wakati hata nyimbo ukiacha chache alizotunga yeye alikua hashirikishwi kwa kuwa hakua na sauti nzuri,sema tu alipata bahati kwa kuwa alikua mmoja wa waanzilishi tu,lakini hakua talented kama wengine ambao hawakua waanzilishi walikuja baadae na talent zao na kuiinua bendi

   • Anonymous says:

    Ila sasa hivi ni maarufu kuliko hao wenye talent waliobaki kunga’nga;nia historia, ndugu yangu sauti ingekuwa inamfanya mtu kuwa mwananmuziki Manda Chant angekuwa maarufu kiliko Mungu wako JB, Aimelia na Mpela wasingepotea, Suzuki asingerudi kulamba miguu ya Kofi! Mtabaki kungangania historia sisi tunasonga mbele! Werra ndo Luambo wa Congo wa kizazi hiki, Meza hata kama ngumu!

   • Anonymous says:

    Werra ndio luambo wa congo wa sasa???! du Hii nilikua sijawahi kuisikia haya bwana tumesikia tunasubiri sasa mumtawaza kuwa ndio michael jackson mpya…ila tunasubiri album ya malewa no.2 kulikoni mbona bwana luambo mpya amekua kimya,nyie anawaeleza nini kuhusu hilo au mnampenda sana kiasi hamuwezi hata kuongelea hilo,two years bila album sokoni kwa mtu kama Luambo wetu mpya ni kulidhalilisha jina mzee Luambo

  • Anonymous says:

   Wewe unadhani kwa sasa Congo ni nani maarufu kuliko Werra?

   • Anonymous says:

    maarufu katika nini mtu miaka miwili hana jipya sokoni

   • Jama Abdul says:

    Jipya la nini wakati zilizopo sokoni bado zinakimbiza? watu wengine washamba sana. suala si kujaza albam sokoni, yeye anauza kazi yake nzuri ambayo bado ni hot cake.

   • Anonymous says:

    Eti miaka miwili hana mpya sokoni, yamekuwa maandazi, Hivi baada ya Wenge kusambaratika JB ameimba wimbo gani wa maana zaidi ya kulia lia, Mara Mulolo na washabiki wake kila wombo wa Wenge mnataka kumpa, kuna siku Pius katuwekea Daddet Autat anatwambia ni wa JB, leo tena Capitane de benelux mnasema ni wa JB! acheni wizi!

   • mwana congo says:

    acheni kupiga mayowe leteni album na style mpya ya uchezaji sokoni tuwatathmini,hii kulia lia wakati jamaa haumizi kichwa,huwezi kuzijua nyimbo za jb wala za yeyote congo zaidi ya werra kwa kuwa wewe sio mtu wa muziki bali ni mtu wa werra

 11. edmas says:

  Historia inaonesha hata Original Wenge walikuwa hawatoi albamu kila mwaka au mfululizo. Albam moja ilikuwa inakaa sokoni atleast miaka miwili ndio kitu kingine kinaingia.

  Kwa maana hiyo, hakuna haja ya kusema eti miaka 2 hakuna albam. Hivi watu wanataka albamu zijae sokoni au kazi za uhakika ndio ziwe zinaingia sokoni…!? Unaweza ukawa na albam moja au mbili kali na mwezio akawa na kumi za ovyo, na ww ukauza zaidi ya yeye.

  • papaa nelson,makambako,iringa says:

   sawa lakini werra yeye alipoanza kujitegemea ndio alikua na huo utamaduni wa kutoa album mfululizo ndio maana tunashangazwa na ukimya wake kwa kuwa alituzoesha hivyo,jb kabla ya anti terro alijikuta akisemwa sana na kwa kutokwenda sambamba na werra kutoa album mfulilizo sasa ni zamu ya werra kusakamwa,muwe wavumilivu tu haina haja ya kuvimba na kutokwa na povu jingi kiasi hicho,huo ndio upinzani ulivyo

   • Anonymous says:

    Albamu Mfululuizo? acha kuweweseka! Werrason hajawahi kutoa albamu kila Mwaka! kumbuka kuwa jamaa alipata ajali na kuwa nje ya muziki, subiri kishindo chake, Werra huwa hatoi albam mbove kama ant-tero hata siku moja!

   • Anonymous says:

    mashabiki wa werra achenoi kudeka na kile ki ajali,kuweni wakweli malewa namba mbili imechelewa sana kuingia sokoni kama anti terro ilivyochelewa kiasi cha kwamba hata ikitoka itakosa mvuto kutokana na kupitwa na wakati,pia kama walivyosema wengine hata kama hamna album sokoni basi leteni hata mtindo mpya,wenzenu bcbg wamekuja na mpunda,rota rota,biloko n.k.tena ndani ya mwaka mmoja tu 2011 na zinatesa nyie stori tu na kutwa kujifananisha na watu wa kizamani kama mzee luambo,labda tusubiri huyu jamaa mliyemrejesha kundini juzi na kumpa uongozi atakuja na mpya maana werra alikua akimtegemea sana kabla na alipoondoka bendi ilipwaya mpaka imebidi akampigie magoti na kumlamba miguu

 12. Chia Levi says:

  When I imagined about issues like: why such details is totally free here? After you write a book then at the least on promoting a book you get a percentage, simply because. Thank you and fantastic luck on informing persons more about it.

 13. At this time it seems like BlogEngine is the best blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

 14. I’m really enjoying the theme/design of your web site. Do you ever run into any browser compatibility issues? A few of my blog readers have complained about my site not operating correctly in Explorer but looks great in Chrome. Do you have any recommendations to help fix this problem?

 15. We absolutely love your blog and find almost all of your post’s to be just what I’m looking for. Does one offer guest writers to write content for you personally? I wouldn’t mind creating a post or elaborating on many of the subjects you write about here. Again, awesome site!

 16. Appreciating the time and effort you put into your website and detailed information you provide. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed material. Excellent read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

 17. Admiring the dedication you put into your site and in depth information you provide. It’s nice to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed information. Great read! I’ve bookmarked your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: