Koffi na Mkewe Aliyah walipoonyesha jumba lao la kifahari

image

Mwanamuziki Koffi Olomide alitambulisha jumba lake kwenye sherehe ya ufunguzi wa jumba hilo ambalo limegharimu mamilioni ya shilingi na kunakshiwa kwa samani za bei ghali.

Mashabiki walipokea kwa hisia tofauti kitendo cha Mwanamuziki Koffi Olomide kuweka wazi Jumba lake la kifahari huku wengine wakimpongeza na wengine wakimwambia kitendo hicho ni kama dhihaka kwa wacongoman ambao wengi wao wanaishi kwenye dhiki kali huku weingine wakiwa wanataabika kupata mlo wao lakini wanajitolea kuchanga kununua kazi zake au kuingia kwa show zake.

Kiukweli ni jumba la kifahari sana na alialika watu mashahuri kwenye sherehe hii ambayo ilitumia pesa nyingi.

Jumba hili limejengwa kwenye vilima vya Fleury almaarufu kama a mont-fleury eneo maarufu kama Msaki ambapo watu wenye pesa ndio wanaishi huko. Koffi ni mmoja wa wanamuziki wakubwa si tu kwa Congo bali Afrika nzima ambaye kiukweli amekuwa na mafanikio makubwa tangu aanze muziki na amejizolea mashabiki wengi kote Ulimwenguni kutokana na muziki wake.

Kila la heri Mopao Mokonzi.

5 Responses to Koffi na Mkewe Aliyah walipoonyesha jumba lao la kifahari

 1. Hadj Le Jbnique says:

  Yap villa la ukweli,mopao katisha hapa sio siri,naona kaamua kuipa jina la ” VILLA DELPIRLO” likiwa ni jina la mmoja wa watoto zake mopao aitwae Derpirlo,ukiacha huyo Derpirlo pia koffi anao watoto wengine wawili waitwao Didistone na Sean James ndio maana sometimes kwenye nyimbo zake mtasikia anajiita papaa na Didistone,papaa na Derpirlo au papaa na Sean James

 2. samaras paul says:

  ndugu hadj huwa nashindwa kuelewa koffi ana wake wangapi,maana naona hapa mnamzungumzia aliyah,na cindi pia huwa ni mkewe au ni demu wake wa pembeni tu?,na je yule mwanamke mweupe mnene hivi aliekuja na koffi hapa dar mara ya mwisho wakawa wapo pamoja kila sehemu na hata kusaga alipowapeleka dukani kwa zizou walikua wawili,je ndie aliyah au? naomba ufafanuzi

  • Hadj Le Jbnique says:

   sijui aliekuja nae dar maana mimi siko huko muda kidogo but AALIYAH ni huyo cheupe hapo unaomuona akiwa sambamba na mzee na wanae wawili akiwemo huyo Delpirlo ambae babake kaamua kuiita hiyo Hotel yake jina la mwanae huyo ambapo pia Hotel Hiyo ilizinduliwa siku ya kuzaliwa mwanae huyo kipenzi ambae ndio official last born wake,Cindy ni nje cup yake but ameiofficialize kimtindo kwani hata wazazi wa cindy wanajua na pia Aaliyah analifahamu hilo kwa ni koffi mchezo na wacheza show wake hajaanza leo toka enzi za kina yule bonge zina bilao ambae ana watoto nae wawili na anawahudumia

 3. Anonymous says:

  c’est une belle maison

 4. Quite great blog and superb and content articles.worthwhile design and style, as share good things with very good tips and concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: