Umaarufu unalevya wasanii.

“Its easy to be number one but its hard to maintain to be number one” nimeanza na msemo huu kwa vile wengi wa wasanii wakipata umaarufu wana tabia ya kujisahau. hili mara nyingi limekuwa likileta manung’uniko kwa si tu mashabiki bali hata watu wengineo ambao si washabiki wa sanaa zao.

Nachelea kusema kuwa wanakuwa wanalewa ama sifa ama vijisenti ambavyo wanakuwa wamevipata na kusau mashabiki ndio wamewafanya wawe na umaarufu walionao na si tu mashabiki bali vyombo vya habari ndio vimewafikisha hapo walipo.

Binafsi nimekerwa sana na kitendo cha mwanamuziki Dully Sykes kukosa adabu akiwa si tu studio bali akiwa Live kwenye kipindi ambacho mashabiki wake wengi wanamsikiliza. Ndani ya wiki moja msanii huyu ameweza mara mbili kukosa adabu tena kwenye radio moja hiyo hiyo.

Wiki iliyopita akiwa live kwenye kipindi cha XXL Dully Sykes alimjibu fyongo mtangazaji Adam Mchomvu wa kipindi hicho mwanzo nilidhani ilikuwa utani lakini Dully alisisitiza kuwa hawezi kuongea na mtu mchafu kama Adam Mchomvu, “siwezi kuongea na mtu mchafu kama wewe angalia mi nywele yako…. mi naongea na Boss wako biashara si mtu mchafu kama wewe” alisema Dully. Baada ya kuangalia kipindi kile kesho yake kupitia Nyuma ya Lensi kupitia Clouds TV nikaona jinsi ile ilivyomuumiza Adam Mchomvu na alivyokuwa akitulizwa asiendelee kujibishana na Dully kiasi alivua headphones na kukaa pembeni.

Kumbuka Dully alikuwa akifanya mahojiano juu ya wimbo wake mpya ambao ameutoa kwa kumshirikisha Mwana FA. Baaada ya Single hiyo inayokwenda kwa jina la Ameen kupigwa hewani watu wakaanza kusema kuwa Single hiyo imefanyiwa sampling kutoka kwenye wimbo mmoja wa huko Jamaica. Hii ilimpelekea Gossip Cop wa Clouds fm kuruka hewani na kumuuliza kwanza Mwana FA juu ya hiyo ambaye alikiri kwa kiasi fulani midundo imefanana lakini alisema ailizwe Dully Sykes ambaye naye baada ya kupigiwa badala ya kujibu alionyesha kukerwa na swali hilo inawezekana style ya kuulizia ya Gossip Cop lakini Dully alimjibu kuwa haongei na mashoga na kumuonya asipige tena. (Gonga hapa kusikiliza zaidi)

Kiuungwana kitendo kile si kizuri  na si cha kiungwana na si kwa Dully tu lazima ujue ngaz unayopandia ndio utakayoshukia, waliokupandisha ni pamoja na vyombo vya habari ukifanya mchezo ndio watakaokushusha.

Nimeandika haya kiroho safi, wala isieleweke vibaya. Pamoja sana.

Advertisements

4 Responses to Umaarufu unalevya wasanii.

  1. edmas says:

    SHULE HUWA INASAIDIA SANA. HUYU DOGO HAJAENDA SHULE KWA HIYO MSIMLAUMU SANA, MSAMEHENI BURE.

  2. Anonymous says:

    HUYU DULLY KAZOEA KU-COPY NYIMBO ZA WASANII WENGINE. HANA JIPYA KATIKA FANI. HATA ILE NYIMBO YAKE YA HIVI MAJUZI BIBERON KAI-COPY KUTOKA TECHNO MALEWA YAKE WERRASON.

  3. Isshaq says:

    Dull mara mia atafute chakufanya kabla aja zalilika

  4. Pretty selected he’ll have a superior go through. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: