Japonais Arejea WMMM kwa Mbwembwe

Mwanamuziki mkongwe aliyewahi kutamba wa Bendi ya WMMM yake Werason Ngiama Makanda amerejea kwenye kundi hilo baada ya kuihasi bendi hiyo kwa takribani miaka 10.

Japonais alitambulishwa wili iliyopita kwenye onyesho la kila jumapili la WMMM na kwa sasa ndiye kiongozi mkurugenzi wa Bendi (Directeur artistique).

Kabla Japonais hajarejea kwenye bendi nafasi hiyo ya uongozi ilikuwa kwake Papii Kakol ambaye atapewa madaraka mengine. Japonais ambaye alitamba kwa upigaji gitaa la solo atasikika kwenye nyimbo mpya ambazo WMMM wanazifanyia mazoezi na pia umati ulilipuka kwa mayowe. Japonais alisikika vyema kwenye Solola Bien na aliamua kuondoka mwenyewe ili akafanye kazi yake yeye kama yeye na baada ya mambo kutomuendea vizuri ameamua kurejea kwenye bendi yake akiwa ni mmoja wa waanzilishi wa WMMM.

Kwa sasa WMMM wameingia Studio kwa ajili ya albamu yao mpya itaitwa « Flash India ».

9 Responses to Japonais Arejea WMMM kwa Mbwembwe

 1. K'Odero says:

  Nakuambia ‘TAZAMA NAFASI HII’…………………….
  Mabo mazito yaaja

 2. Anonymous says:

  Japonais Maladi, Mtunzi wa Solo la Ndombolo ya Solo!

 3. Anonymous says:

  Mtunzi wa solo la ndombolo ya solo..!!!ulikusudia kusema nini labda mzee?

  • Anonymous says:

   Wimbo wowote unapotungwa kuna kazi ya kutengenza melody za vyombo, wakati ndombolo ya solo unatungwa, japonais ndio aliotengeneza sola la wimbo huo

   • Anonymous says:

    Pia ndie aliecreate solo la Titanic kabla ya Wenge kusambaratika, ndio maana ukusikiza Force d iNtervention Rapide na Titanic zinaanza kwa kufanana! na mbele kidogo kuna vionjo vingi vinafanana.

 4. Anonymous says:

  Werra anakula matapishi yake,kaona mambo hayaendi 2 yearz without album,dhulma mbaya atawaangukia mmoja mmoja na bado didier masela na adolphe dominguez,halafu pappy kakol lazma aondoke

 5. Nedra Kristy says:

  I unquestionably enjoy just about every little bit of it and I have you bookmarked to examine out new things of the website a should read through site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: