Nani mtunzi wa Voyage Mboso?

Kuna nyimbo ambazo kwa mashabiki wa Wenge Musica kwa ujumla wanazikumbuka sana wimbo huu wa Voyage Mboso, Wengi walijua huu Wimbo ni Wimbo wa JB Mpiana lakini ukweli ni kuwa huu ulikuwa ni Wimbo wa Adolph Dominguez na ndio maana walipoparanganyika Werasson alikuwa akiupiga sana wakati bado yuko na Dominguez na walipoanchana Werasson aliacha kuupiga na Dominguez aliendelea kuupiga. Angalia hapo chini utaona Voyage Mboso ya Werason pia.

Kwenye Original Version utamsikia vizuri Ekokota Machine Roberto Wunda,kwenye vyombo ni Patient Kusangira, Didie Masela Vando Mass, Mbonda na wengineo.

3 Responses to Nani mtunzi wa Voyage Mboso?

 1. K'Odero says:

  Ukweli kabisa bwana Pius maanake wimbo huo huo hata kwenye album Terraine Eza Mine yake Werrason, ni sauti ya Adolphe na bana WMMM ndio ungesikia. Werrason mwenyewe hakupiga hata beti moja kwenye wimbo huo.

 2. Hadj le Jbnique says:

  Voyage officially ni utunzi wa tata mobitch Adolphe kwa kuwa aliununua na kuusajili ndani ya wenge kama wake lakini kiukweli kabisa hakuutung yeye bali mtunzi halisi ni Bogus Bompema ambae yuko bcbg kwa sasa,ni yeye pia alietunga coco madimba na kumuuzia werrason,hii ni kawaida sana congo kwa wanamuziki ambao tayari wana majina makubwa huwa haumizwi sana vichwa bali hununua ‘mistari’ toka kwa vijana ma under ground na kuzisajili kama zao,mfano wimbo cavalier solitaire wa jb kwenye feux d’amour jb aliununua kwa Jules Kibens enzi akiwa under ground hajulikani,kwa sasa kibens yuko bcbg na ni huyu huyu kibens ndie alitengeneza mistari yja wimbo maarufu wa blaise bulla uitwao filandu kumuuzi sele ambae aliurekodi na wenge kama wake,ipo list ndefu ya nyimbo maarufu za wanamuziki wakubwa congo niliwahi kuiweka humu ambayo inaonyesha watunzi halisi lkn hawajulikani,mkubwa pius kama utapata chance unaweza kuirudia kuipost ile list ya kushangaza ya watunzi halisi-melesi mingi

 3. Farid 4x4 says:

  Bonini yosalase boyee voyage
  yokotika mutu na sousi voyage
  soki likambo nani akosalisa ye voyage
  Daima Kaka Pius hua unachagua nyimbo zile ambazo moyoni zinaleta furaha sana,
  melesi mingi , mimi binafsi huu mwimbo ulinitesa sana kipindi nipo mbali na kipenzi cha roho yangu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: