Happy Birthday JB Mpiana Babaa Daida

JB Mpianaaa

Leo June 2 ni siku ya kuzaliwa Papaa Sherii Salvatory De La Patria JB MPIANA, kama wapenzi wa muziki wa Lingala tunaungana nae katika kusherehekea siku yake hii  ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka 45. JB alizaliwa 1967 na mzee Mpiana Lusambo na mama Agnes katika eneo liitwalo Kananga ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo akiitwa jina lake halisi Jean Bedel Mpiana wa Tshituka.

Tangu aanze kujihusisha na muziki Jb amejipatia sifa nyingi za utunzi na uimbaji bora ikiwemo kuwa mwanamuziki wa kwanza katika kizazi chake(cha nne) cha muziki wa Congo kujipatia tuzo ya GOLDEN DISC,Mtunzi wa wimbo bora wa mwaka 1988-Mulolo ambao uliipandisha sana Wenge MUSICA 4×4 tout terrain na kuifanya ijulikane Africa nzima,pia Jb aliweka rekodi nyingine pale 1999 alipokuwa mwanamuziki wa kwanza kwa kizazi cha nne cha wanamuziki wa Congo kupiga kupata nafasi ya kupiga katika kumb maarufu duniani zilizopo Paris ufaransa ziitwazo Zenith, Olympia, Bercy pamoja na Stade des Martyrs ambapo show yake ndani ya Olympia ikaja kuwa voted kama best show of the 20th Century kwa wanamuziki wa Congo.

Pichani JB Mpiana akiwa amembeba kipenzi mwanaye anayeitwa Daida kama utasikia anamtaja sana kwenye nyimbo zake. 

Happy Birthday Papaa na Daida Jb Mpiana, tunakutakia maisha marefu na mafanikio katika kazi yako

20 Responses to Happy Birthday JB Mpiana Babaa Daida

 1. Stivin says:

  “Aliweka rekodi ya Kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kizazi cha nne kupiga kwenye kumbi kubwa……. for heaven sake that was Wenge BCBG including Makaba and Bula, 1999 bado JB alikuwa anatembelea nyota ya Wenge BCBG, tuwekee mafanikio yake baada ya Makaba na Balise Bula kuondoka.

 2. Anonymous says:

  Kwa zenith 1999 sele bula alikuwepo?makaba mwenyewe alishiriki kupiga gita kwenye wimbo mmoja tu ‘omba’ muwe wafuatialiaji basi kama mnapenda ubishi.

 3. Anonymous says:

  Mi naomba kujuzwa jambo kabla ya mimi kuwakaza kitako kuwajuza yangu niyajuayo kuhusu maisha ya kimuziki ya memberz wote wa wenge baada ya msambaratiko wa mwisho ambao ulifananishwa na kuzama kwa meli ya titanic ambapo wapo wachache walionusurika licha ya meli hiyo kuzama,naomba kuuliza,kama alain makaba na blaize bula ndio walikua wakimbeba jb mpiana na wenge yake bcbg iweje baada ya wao kuachana na jb ndio iwe kama mwisho wao kimuziki huku waliokua wanambeba akiwa bado anapeta na bendi yake ikiendelea kupata mialiko africa na ulaya?blaize hajawahi kualikwa akatumbuize hata mpwapwa,huyo makaba alijaribu kutoa visolo album vyake hakuna hata aliyejua kama viko sokoni,kajaribu uproducer hakuna hata mmoja msanii mmoja maarufu alimuamini kufanya nae kazi,sasa hivi nasikia yuko kinshasa anataka kufungua studio hapo akidhani atapata soko kubwa kwa kuamua kuwafuata wasanii hapo makao makuu ya muziki afrika,hii ni baada ya kuchemka ulaya,jb mwanaume wa shoka na ndio kilikua kichwa cha wenge ndio maana wanaoachana nae wanapotea kimuziki,kwa kuwa walikua wanamtegemea yeye

  • Stivin says:

   Kichwa cha Wenge kilkuwa Werra hilo halina ubishi, Nakuapia JB ndop angetoka Wenge na kuacha wanamuziki wote angebaki historia!

  • Stivin says:

   Nasisitiza kuwa 1999 JB alikuwa anatembelea nyota ya Wenge, 1999 bado albamu ya Titanic ilikuwa inatamba, kama unakumbuka mwaka 1999 alikuja Tanzania, Tulitangaziwa kuwa Wenge BCBG inakuja, wakaja bila Makaba na Blaise Bula, tukaambiwa wmebaki Paris kutengeneza albam zao, ikabidi Mpiana akodishe majeshi kutoka kwa Suzuki, nionyeshe show ya maana Mpiana alifanya baada ya hiyo ya 1999.

 4. JB Mpiaana ndio kichwa cha Wenge mtake msitake, Wenge bila JB ni kazi, Werason ni mzuri wa kupanga vijana na kuwapa majukumu, JB ni mwanamuziki kwa maana ya Kwamba anatunga, Anaimba, Ana compose na kupanga sauti. … Amini nakwambia kama we ni mfuatiliaji wa muziki utayajua haya.
  Kwa JB Mpiana kama unapenda Muziki na sauti JB ndio mwenyewe ila kama unapenda Sebene na Kelele basi Werason anaweza.

  • stivin says:

   Kama ni sauti hata Manda chant anayo tamu kuliko JB, Niwekee hapa wimbo wa maana aliotunga JB baada ya Wenge kusambaratika, Kila siku Mulolo mulolo, nitajieni albam ya kuanzia mwaka 2000 ya JB ambayo imefikia platnum,!

 5. Anonymous says:

  Naomba kuingilia kati nataka kuwakumbusha mawili tu wenge musica 4*4 imetoka au kujulikana kupitia wimbo wa mulolo ambao mtunzi jb baada ya hapo ikaja wimbo wa kin est bouger ndo ya pili toka wenge ilianza nazani jb ndo alikua president hadi leo DiDie masela,alain makaba,alain mpela, tutu kaluji,marie paul,mande chante,roberto wanaendelea kumuita jb preident.

  • Stivin says:

   Kwanza Mulolo haukutungwa na JB, pili Wenge ilijulikana zaidi kwa wimbo wa Kala yi Boeing, utunzai wa Werrason

 6. Isambo says:

  Huku kwenyu Tanzanie ndiyo Kala Yi Boeing Mulisikilishaga munamba mojja, Mu Kinshasa Mulolo ndio ilitoa Wenge, chipindo hicho Muzee Nyoshi Nyoka Longa wa Mukolo Mboka ndio alikuwanga anashika moto mahala pote. we unasemanga nini sasa?

 7. Hadj le jbnique says:

  Stiv kichwa cha bendi ni rais wa bendi siku zote,hiyo ndio system ya muziki congo ilivyo otherwise tuendelee kubishana kuhusu hili ktk kuchangamsha barza letu hili tu lkn hakuna tunachoweza kubadilisha hata kama tungependa,ndio maana mpaka leo werrason ndio rais wa wenge maison mere,jb ameendelea kuwa rais wa wenge bcbg yake,koffi ql yake

 8. jacob maskas meneja wa bwiza says:

  Nasema aksanti sana kwa kusoma habari hii ya mwanamziki mahalufu kwa kifupi ,nampendezwa na nyimbo zake mungu amzidishie !!

 9. Bea Tkacik says:

  a lot of fantastic facts and inspiration, the two of which I have to have, due to present this kind of a valuable facts right here.

 10. Kamala Salt says:

  Coming from my observation, shopping for technology online can for sure be expensive, but there are some tips and tricks that you can use to acquire the best deals. There are always ways to come across discount specials that could make one to have the best electronics products at the lowest prices. Thanks for your blog post.

 11. Thanks for the marvelous posting! I truly enjoyed reading it, you are a great author.I will be sure to bookmark your blog and will eventually come back from now on. I want to encourage you to definitely continue your great work, have a nice day!

 12. We stumbled over here by a different web page and thought I might check things out. I like what I see so now i’m following you. Look forward to finding out about your web page repeatedly.

 13. Fantastic post but I was wondering if you could write a litte more on this topic? I’d be very grateful if you could elaborate a little bit more. Many thanks!

 14. Admiring the time and energy you put into your blog and detailed information you offer. It’s nice to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed material. Excellent read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

 15. I’m really loving the theme/design of your blog. Do you ever run into any web browser compatibility issues? A few of my blog visitors have complained about my website not working correctly in Explorer but looks great in Opera. Do you have any suggestions to help fix this problem?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: