Sababu za kuchelewa Anti Tero Sehemu ya II

 

Kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kabla ya kwenda South AFRICA bcbg walipitia Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya show iliyoandaliwa na PRIME TIME PROMOTION chini ya Jose Kusaga

 

Wimbo Vicky Nsongi wa PPU ulioleta kizaazaa huu hapa.

Baada ya mabadiliko hayo bcbg kukawa na kambi mbili,kambi ya kwanza ikawa ya Seguin, Pathy Moleso, Jules Kibens, JDL na Boguis Bompema na upande wa pili kukawa na kambi ya Tutu Kaludji, Burkina Faso, Ficare Mwamba, Accompa Alba, ambapo kundi la kina Tutu Kaludji ambalo pia Alain Mpela alikua miongoni mwao likitaka PPU(Gino, Nono Fuji, Abraham Mignon na wengine) wapewe nafasi ya angalau kuweka wimbo mmoja katika album ya ANTI TERRO ambapo vijana wa PPU wakakubaliana miongoni mwa nyimbo zao nyingi wautumie wimbo VICKY NSONGI, wakaanza kuufanyia maandalizi wimbo huo wakiwa Kinshasa chini ya mpiga solo Burkinafaso Mbokalia ambae wakati huo alikua anakisaka cheo cha artistic director wa bcbg kwa hali na mali, katika kazi hiyo ya kuwaongoza vijana wa PPU kuiandaa VICKY NSONGI ili iwemo kwenye ANTI-TERRO, Mbokali alishirikiana na Accompa Alba (mpiga solo na rhythm guitar) kabla kundi zima la BCBG wakiwamo wao halijasafiri kwenda South Africa kwa ajili ya kuzifanyia mixing na kurekodi baadhi ya nyimbo kukamilisha album.

Kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kabla ya kwenda South AFRICA bcbg walipitia Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya show iliyoandaliwa na PRIME TIME PROMOTION chini y Jose Kusaga ambapo walifanya show hiyo katika ukumbi wa Diamond Jubilee na ilikua siku ya sikukuu ya Idd ambapo baada ya show hiyo kesho yake kukaandaliwa event ya kuosha magari kuchangia yatima pale victoria petrol station ambapo Jb Mpiana, Tutu Caludji pamoja na wadada wacheza show wa bcbg wakiongozwa na Monica Seles walihudhuria,na katika kuchangia kwenye event hiyo Jb aliosha gari ya Kusaga kwa gharama ya shilingi za Tanzania milioni moja toka kwa kusaga mwenyewe.

https://spotistarehe.files.wordpress.com/2009/12/bbbbb.jpg

JB Mpiana akiwajibika kwenye Show ya Ubungo Plaza Dar Es Salaam

…………………………………………………………………………………………………………………….

Baada ya shughuli hiyo ya kuchangia yatima iliyoandaliwa na CLOUDS FM na PRIME TIME,BCBG wakiongozwa na JB wakaondoka zao kuelekea South Africa kwa ajili ya kazi niliyoitaja hapo juu,lakini walipofika huko tofauti na makubaliano ya awali kwamba PPU wapewe nafasi ya kuweka wimbo mmoja kwenye ANTI – TERRO,Jules Kibens na Boguis Bompema wakataka kufuta vocals za PPU na badala yake kuweka zao kwenye wimbo VICKY NSONGI lakini wakongwe Ficarre Mwamba na Burkina Faso wakapinga vikali hilo jambo ambapo inaelezwa Ficarre aliwafokea vikali kina Kibens kwa kutaka kufanya hujuma hiyo dhidi ya vijana wa PPU ambao wote walibaki Kinshasa lakini kwa mshangao mkubwa JB hakusema lolote dhidi ya hujuma ya kina Kibens licha ya kuwa Ficarre ni mtu wa siku nyingi na anaeheshimika kwenye bendi ukilinganisha na kina Kibens.

Lakini Seguin Mignon alipowasili eneo la tukio na kukuta sintofahamu hiyo yeye moja kwa moja alichukua side ya kina Kibens na kuwatetea kwa walichokua wakitaka kuwafanyia vijana wa PPU ambapo Burkina Faso kuona hivyo akasimama na kumwambia “nyamaza wewe usiejua kupiga drum” , kufuatia kauli hiyo toka siku hiyo Seguin akaapa lazima ahakikishe anamuondoa Burkina Faso na kundi lake haraka iwezekanavyo, akaanza kumpelekea maneno ya uchochezi JB dhidi ya kina Burkina Faso, Accompa Alba na Tutu Caludji, baadae JB maneno yakamuingia akaanza kumu ignore Burkina Faso kwanza na baadae Accompa na Tutu Kaludji mpaka jamaa wakaamua kujiondoa wenyewe kundini walipomaliza tu kurekodi ANTI TERRO kwa mbinde huku kukiwa na uhasama mkubwa kundini wakati wa kurekodi,waliamua kuiondoa baada ya kuona hawana thamani tena kwa Jb(ikumbukwe Jb akiwa hakutaki anayo tabia kukudharau nje ya jukwaa tu bila kuonyesha dharau jukwaani-mbele ya washabiki).

Lakini wakiwa hapo South Africa VICKY NSONGI hatimae ilirekodiwa ambapo wakongwe “mikuli” kina Kibens,Jdl na wengine ambao Jb alikua akiwasikiliza sana kutokana na wao kuwa nae karibu wakati akiwa na wakati mgumu kufuatia suala lake la kukimbiwa na mkewe Amida Shatur na pia issue ya visa ya kwenda ulaya wakaweka vocals zao na waimbaji kutoka kambi zote mbili hasimu kundini wakalazimishwa kuimba pamoja ili kurudisha amani kundini.Kiufupi Seguin Mignon akawa ni mtu mwenye sauti sana ndani ya BCBG,ndio maana hata vijana kina Gino, Nono Fuji, Abraham,Sakoko n.k. hawaishi kumtaja taja wanapoimba ili kujiweka karibu nae,hakuna anaetaka kugombana nae kwa kuhofia usalama wake kundini kama ilivyokuwa kwa kina Tutu Caluggi na Burkina Faso.

Hicho ndicho kilichotokea lakini hatimae album ya ANTI TERRO ikatoka baada ya vuta ni kuvute ya muda mrefu na ikawa mara ya kwanza Jb kurekodi/kufanyia mixing album South Africa tofauti na Europe(Paris) walikokuzoea.

9 Responses to Sababu za kuchelewa Anti Tero Sehemu ya II

 1. werrasonique forever says:

  ahaa ok,it sounds good…

 2. Stivin says:

  Na albamu yenyewe ikaishia kuwa Flop!

 3. mkemimi,kigoma,ujiji says:

  ndio kaka stiv,wat do u expect katika vurugu hizo kutoke album nzuri????si unajua umoja ni nguvu.Mimi mwenyewe zaidi ya wimbo ESSAU wa mpina sikuona cha maana,labda kidogo na hii vicky nsongi tena baada ya kuisoma stori yake hapa ndo ikabidi niusikilize vizuri na kugundua ni wimbo mzuri tu hasa kwa sisi wa kina dada kwa kuwa unatuzungumzia sisi na maneno yake mazuri,kuupenda ni lazima uwe unapenda nyimbo za taratibu lakini otherwise utakuzingua

  • Stivin says:

   Hapo ndo inathibitisha kuwa Mpiana alikuwa kiongozi jina wa Wenge, the real leaders were Werrason na Masela. Kama anashindwa kuongoza watoto hao angewezaje kuwaongoza kina makaba?

 4. dj papa upanga says:

  Hata werra nae yalimkuta ktk maisha yake ya kujitegemea,tena yeye ndio zaidi anashindwa kabisa kuishi vizuri na ba musicien wake toka ameanza mpaka leo ni kimbia kimbia kila kukicha kwani hukusoma hapa hapa rejewa vurugu zake kimbia kimbia ya kuanzia kina masela,adolphe,baby ndombe,bill,lacoste,mwanae ferre na wote waliokwenda kuanzisha marquis de maison mere,kimbia kimbia haikuishia hapo ikaja zamu ya yule mtaalam wa solo na arrangement ya muziki nimemsahau jina,na juzi tena chupu chupu heritier nae aingie mitini na bado yuko mguu nje mguu ndani,lkn mpiana yuko stable organization hakunaga congo kwa sasa,no hama hama,full nidhani kazi kwa kwenda mbele

 5. mukubwa shabani says:

  Stiven kila m2 anajua wewe ni mpenzi wa werrason,sitaki kuingilia ubishi wenu usioisha na wa2 wa jb mpiana,ila nataka tu kukukumbusha hili,werrason hakuwahi kuwa kiongozi wa bendi kwa maana ya chef d’orchestre,bosi wa nidhamu bendini wala rais wa bendi enzi za wenge muzika licha ya ukweli kwamba alikua mmoja wa waasisi!yeye alikua mtunza fedha tu tena hakua wala mpanga matumizi ya hizo fedha,uongozi wa bendi kaja kuujua sawa sawa maison mere ambako pia wakati bendi hiyo inaanzishwa kiongozi mkuu alikua Adolphe Dominguez,yeye na didier masela walikua wasaidizi adolphe tu,na unajua kwamba alimpindua adolphe na badae kuwadhulumu wenzake bendi na kuifanya ya kwake peke yake??fuatilia utaelewa bora matatizo ya jb yalikua ya muda mfupi tu sasa yuko stable,maison mere haijawahi kutulia toka imeanzishwa!

  • Stivin says:

   Hata kama hakuwa official leader but he was a defacto leader yeye ndio aliyekuwa anaona talents na kuzirecruit, yeye ndie alimrecruit Mpiana? na siyo yeye tu embu soma kipande hiki hapa “It is reported that Alain was recruited through a chance meeting with Werrason in Kinshasa. Alain, then only fifteen years old, living in Matete, spent his holidays in Bandal. One afternoon, he was humming a song by Kester Emeneya. Werrason visiting nearby liked what he heard and approached the boy and convinced him to follow him to the headquarters of Wenge Musica and presented him to the rest of the group who accepted him immediately”

   • Maghambo Philipo says:

    Stephen kujua na kuvumbua vipaji si sababu ya mtu kuwa kiongozi, kuna watu ambao wana uwezo wakuona kama hivyo basi ma Agent wa Wachezaji wangekuwa wanatajwa wao kila siku, We unamjua Agent wa Drogba hata kwa Sura?????
    Muziki ni Tallent na si kila mtu anaweza kuimba kaka wengine wanapiga kelele tu si waimbaji bana, Werason ni mzuri akiimbishwa na akijumuishwa ameweza kukusanya watu wenye vipaji lakini peke yake hatoboi tofauti na JB Mpiana

   • Stivin says:

    Hahaha! Mbona Mpiana ameshindwa kutoboa toka abaki peke yake?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: