Je wajua ni nini Kilichelewesha Albamu ya Anti Tero ya JB Mpiana Sokoni?

May 21, 2012

Na Hadj Le Jbnique, Boston, Massachusetts, Usa.

Wimbo Anti Terro

Mwaka jana tulichapisha makala za kuhusu kuparanganyika kwa kundi zima la Wenge BCBG na hatimaye kujitenga kwa Werasson na wengineo, Baada ya kuangalia kuanzishwa kwa kundi la Maison Merre la Werrason na matatizo yake, Kama uliikosa angalia Sehemu ya Kwanza hapa, ya Pili  ya tatu  na  ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko, kisha tukaitazama kuzaliwa kwa Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, Pia tuliona jinsi WMMM alivyojipanga na ku recruit wanamuziki wapya kama Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapayaniliahidi kuwaletea ni kwa sababu gani Albamu ya Anti Terro ya Wenge BCBG alichelewa sokoni… Endelea sasa.

Kulikua na mambo mengi ya nje ya bendi na ya ndani ya bendi yaliyochangia album ANTI-TERRO ya BCBG kuchukua muda mrefu kutoka sokoni.Miongoni mwa mambo ya nje ya bendi lilikua ni suala la ugumu wa kupata visa za kuingia ufaransa na  ubelgiji kwa wanamuziki toka Congo, na kama inavyofahamika wanamuziki wa Congo walikua wakizitegemea studio zilizoko kwenye nchi hizo kwa ajili ya kazi ya kurekodi nyimbo zao.

Na tukija kwenye mambo ya ndani ya bendi,awali Jb alipanga album hiyo iwe na nyimbo nyingi za Alain Mpela ambae alikua ni kiongozi wa bendi (Chef De Orchestre) pamoja na nyimbo bendi ya vijana wadogo ya BCBG inayofahamika kama PPU (Presidential Protection Unit) ambayo Alain mpela aliipromote sana na mbili tatu za Jb Mpiana mwenyewe huku member wengine wakitakiwa kuweka tu vocals zao kwenye nyimbo za album hiyo bila wao kuwa na nyimbo hata moja,Alain Mpela alipewa chance ya kuweka nyimbo zake sita (6).

Lakini wakiwa kwenye maandalizi ya album hiyo huku wakisikilizia suala la visa na kuumizwa kichwa ni wapi watakwenda kuirekodi ama kuifanyia mixing album hiyo kama visa itaendelea kusumbua kukatokea sintofahamu kati ya Jb na Alain Mpela, rafiki yake mtiifu ambae alimchukulia kama mdogo wake (ikumbukwe Alain Mpela na mdogo wake Bouro Mpela kuna wakati walikua wanaishi nyumbani kwa Jb kama Herritier watanabe alivyowahi kuishi nyumbani kwa Werrason baada ya Jb kumwambia akasome kwanza shule apate degree ndio arudi BCBG).

Kilichosababisha sintofahamu hiyo ya Jb na Afande Mpela ni simu ambayo ilipigwa na Koffi kwa lengo la kumshawishi Alain Mpela ajiunge na Quartier Latin yake na badala yake simu hiyo ikapokelewa na Jb huku koffi akidhani ni Alain mwenyewe ndie aliepokea simu hiyo hivyo kuendeleza mazungumzo yao yalipokuwa yameishia.

Baada ya simu hiyo Jb alikasirika sana na kumuona Alain Mpela kama bonge la msaliti kwa kuwa licha ya ukaribu wao na yeye kumchukulia kama mdogo wake aki share nae mambo mengi hakuwahi kumtonya chochote juu ya mazungumzo yake na Koffi ambae alikua adui mkubwa wa Jb wakati huo, na Jb ana kitu kimoja mpaka leo, hakuna kitu asichokipenda kama usaliti. Hivyo basi kuanzia siku hiyo Jb na Mpela hawakua brothers tena, na ule mpango wa kumpa nafasi Mpela aweke nyimbo zake 6 kwenye ANTI-TERRO Jb akaufutilia mbali na badala yake akamuachia nafasi ya kuweka nyimbo zisizozidi tatu huku kukiwa na mipango ya kumvua u chef d’orchestre.

Kuona hivyo Alain Mpela akasusia kushiriki shows na mazoezi ya BCBG kwa wiki mbili na hatimae akatangaza kujiondoa kundini huku akitoka na single maalum kwa ajili ya kumuimbia na kumsifia adui namba moja wa Jb bilionea Didi Kinuani. Mpaka hapo Jb na kundi wakawa na kazi ya kuziaondoa nyimbo za Mpela ambazo walikua tayari wameshazifanyia sana mazoezi na walikua wakizipiga kwenye shows zao za kila weekend ndani ya Kinshasa na kuanza upya kuandaa nyimbo nyingine na kujipanga upya huku wakiwa hawana mfadhili wala mdhamini kama ilivyo sasa kwa makampuni ya bia ya Congo kutoa sponsorship,wakati huo walikua wakiwategemea matajiri wakubwa wapenzi wa muziki kama huyo Didi Kinuani ambae Jb alikua tayari ameshagombana nae baada ya Dikin kumuiba mke wa Jb mamaa Amida Shatur na kumfanya mkewe.

Alain Mpela “afande” alipoondoka kundini BCBG nafasi yake kama Chef D’Orchestre kwenye bendi ilizibwa na Tutu Caludji ambae awali alikua mkuu wa mambo ya nidhamu kundini ambapo nafasi hiyo na yeye alimuachia mpiga drums Seguin Mignon ambae De La Patria JB amekua akimpenda na kumsikiliza sana akimchukulia kama mdogo wake pia,vilevile Seguin ni mtu wa karibu sana na De La Forret WERRASON na ndio amekua kiungo kati ya JB na WERRA. Hali hiyo ya kuwa na ukaribu na JB ikamfanya Seguin awe na sauti kubwa kiasi cha kwamba ukigombana nae au kama hakutaki lazima uondoke BCBG.

Je unataka kujua nini kiliendelea? Soma hapa kesho…..

[cryptex]piusmicky@yahoo.co.uk [/cryptex]


MTUNZI WA REMISE ET RAPRISE

May 21, 2012
Original ya Mukulu wa Bakulu

Na Hadji

KUMBE MTUNZI HALISI WA WIMBO REMISE ET RAPRISE “TRESSOR MPUTU” WA MAISON MERE SIO WATA NI HUYU HAPA!!

Kumbe Mukulu wa Bakulu ndio mtunzi asilia wa wimbo mpya unaotesa wa Heritier Watanabe na maison mere???!

Msikilize Mukulu hapa then uwasikilize Werra na Wata kwenye copy ya wimbo huo huo mmoja then utoe maoni yako.Wimbo huu ambao Werrason na Heritier wameubadilisha jina na kuuita Remise et Raprise a.k.a. Tressor Mputu Mukulu wa Bakulu ambae ni shabiki mkubwa wa Jb mpiana aliuimba kwa mara ya kwanza kwenye tamasha la Fikin 2010

Copy ya wana

Nani kama Koffi?

May 21, 2012

Hadj Le Jbnique

Enter video caption here
Mwaka 2009 Koffi alifanya show ya ukweli yenye mafanikio makubwa sana upande wa mahudhurio ndani ya Paris katika ukumbi mkubwa na maarufu wa “Zenith”.

Haikua kazi rahisi kupata mafanikio bali kazi kubwa ilifanyika ya kuitangaza show hiyo kwa maana ya kwamba waandaji wa show hiyo hiyo waliijua kazi yao na kutimiza wajibu wao wa kufanyia promo ya kutosho hiyo show ambayo matunda yake yalikuja kuonekana ukumbini, siku zote biashara ni matangazo, kabla ya kuangalia video ya ‘balaa” alilolifanya Koffi ukumbini na kukonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria siku hiyo, hebe tuone video hii inayoonyesha moja ya promo zilizokuwa zikirushwa hewani Tv stations za ufaransa, ubelgiji na nchi nyingine jirani na ufaransa ili kuwahamasisha watu wafike kwa wingi kwenye show hiyo kutoka nchi mbalimbali za ulaya zilizo jirani na ufaransa.

Hapa utamuona Koffi mwenyewe akiimba na gita lake, pia “mkewe” Cindy akiinadi show hiyo ya kufa mtu….

Siku ya siku ikafika,matunda ya kuwekeza kwenye pesa ya kutosha kwenye promo ndiyo haya yanaonekana hapa hatimaye, hili ni fundisho kwa promoters wengine kuacha ubahiri wanapoamua kuandaa show ya mwanamuziki yeyote yule hata vijana wetu wakitanzia, mfano mzuri ni hii show ya diamond mlimani mwisho wa mwezi,sijui kina nani wameandaa ile show but wanaonekana wamejipanga vizuri…big up kwao,matokeo mtayaona siku ya show hiyo na mtakubaliana na mimi show ni matangazo kama biashara nyingine….Pata show murua ya bana Quartier Latin, mamaa Cindy Le Coeur


May 21, 2012


seguin mignon wa Wenge BCBG

May 21, 2012

Alain Prince Makaba 188 Memoir et Mignon Garcon Seguin

Seguin Mignon(kulia) mpiga drums wa bcbg wa sasa enzi hizo akiwa na Alain Prince Makaba”internet”, Ukisikiliza Omba Remix ile Live kuna mahala JB Mpiana alilalamika sana na kuanza kuwaita wanamuziki wake akiwataja sana Afande, Caludji na kisha kuwataja wengine alianza na Seguen kwa wanaosikiliza vizuri Seguen aliliza sana Drumz JB alipomuita huyu ndiye aliyechukua mikoba ya Titina Alcapolne na kwa kweli kazi yake inasikika.

Msikilize JB hapo chini


Flaviana aweka shada makaburi ya wahanga wa MV Bukoba

May 21, 2012

https://fbcdn-sphotos-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash3/536339_271136349651437_100002652237808_539133_692911028_n.jpg

Flaviana Matata akiweka shada kwenye kaburi isiyo na jina Igoma jijini Mwanza kama sehemu ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya MV Bukoba. Flaviana alimpoteza mama yake mzazi.

Pamoja na mambo mengine Flaviana Matata alikabidhi msaada wa maboya (life vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd) kama sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba – ambapo ni miaka 16 tokea meli hiyo ilizama na kuua watu takriban 1,000 akiwa pamoja na mama yake Flaviana

Picha kwa hisani ya Maria Sarungi.


%d bloggers like this: