TAFITI: Werasson ni Maarufu kuliko wanamuziki wote, Kama Papa Wemba miaka ya 70 – 80

image

Werrason Ngiama Makanda

image

Papa Cherry Le Suvereee

Werason amekuwa ni mwanamuziki mwenye wafuasi wengi tangia Wenge BCBG iparanganyike, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Digital Congo Werason ameweza kufikia record iliyowekwa na Papa Wemba miaka ya 70 na 80.

Tangu kuvunjika kwa kundi hili mwaka 1997 Werason amekuwa hapewi nafasi na JB Mpiana huku wakipumuliana kwa mashabiki na umaarufu.

Utafiti huo umechapishwa kwenye mtandao maarufu wa Digital Congo unasema kuwa Werra amejizolea umaarufu si ndani ya Congo pekee bali hata nje ya Congo. Kadhalika utafiti huo unasema kuwa Werrason amekuwa akipendwa zaidi na “walala hoi” na hii inatokana na tabisa yake ya kufanya maonyesho mengi sehemu wanazoishi watu hao huku JB Mpiana akiwa na mashabiki wengi wenye maisha ya kati na matajiri.

Wenge ambayo iliingia kwa kasi katika ulimwengu wa burudani kwa staili ya SAPE (société des ambianceurs et des personnes élégantes) ambayo ilianzishwa na Papa Wenga, lengo la Papa Wemba ikiwa ni wanamuziki ambao watanashati wanavaa vizuri na kujiweka kwenye maisha ya juu ikiwa ni pamoja na sehemu wanazoishi, Wanamuziki hawa walikuwa wanatoka wote eneo lijulikanalo kama Bandalungwa ama Bandal ambalo ni maarufu kwa maisha ya mjini kama vile Kinondoni ambapo wajanja wote wanaishi huko, ila baadaye yalipowachanganyia wakahamia eneo lijulikanalo kama Socimat kama masaki ambapo watu wenye pesa zao wanaishi.

Mwaka 1997 swali kubwa ilikuwa nani anaweza kuikuza hiyo Spirit ya wana Bandal maana BCBG WENGE walijitambulisha kama familia moja. lakini baada ya kuparanganyika kila mtu kivyake waliwagawa mashabiki pia na kujikuta kila upande unaangukia ama kwa JB Mpiana ama kwa Werasson.

Kwa mujibu wa tafiti hiyo ambayo ilichapwa wiki iliyopita ndani ya mtandao wa Digital Congo Werasson ameonyesha kupendwa zaidi wa masela ambao ni wengi huku JB akisemwa kuwalenga zaidi watu wa Grade B kwenye Show zake. Kiukweli wakurumba hawa wawili wanaendelea kutawala mashabiki wa muziki wa Congo mbali na vijana wengi wanaochipukia kwenye muziki huu na ushindani kati yao ndio umekuwa chachu ya mafanikio ya muziki huu mpaka leo.

Hakuna aliyedhani JB Mpiana na Koffi wangeweza kuja kuwa marafiki walivyosasa urafiki ambao mashabiki wanasema kuwa urafiki wa mashaka na unatokana na Koffi kuhama toka kwa Werrason kwenda kwa JB Mpiana, hilo lilizidi pale Werra alipokataa kwenda kumpa mkono Koffi na kumuangukia ili uhasama kati yao uishe, Werra alikataa hilo mbele ya mashabiki wake takribani elfu 20 ambao walimshangilia sana.

Werrason alifanikiwa kupata Kora Award na baadaye kuchaguliwa kuwa Balozi wa UNICEF na Mjumbe maalumu wa Amani huko Congo nafasi ambayo anaitumikia bado.

61 Responses to TAFITI: Werasson ni Maarufu kuliko wanamuziki wote, Kama Papa Wemba miaka ya 70 – 80

 1. samara paul says:

  nadhan mbali ya show zake werra kuwalenga watu wa chini lakini pia tangia mwaka 2000-2012 albam zote anazotoa zinawashika sana mashabiki wa muziki wa DRC ndani na nje ya congo,kushinda zile anazotoa JB MPIANA ,sina hakika sana kama mpiana amewahi kushinda kora kama ilivyo kwa WERRA,na wapenda muziki wote afrika wanaamini kama hujashinda kora huwezi kujiita umefikia kilele cha mafanikio,KORA ndio grammy ya afrika.

  • Hadj Le Jbnique says:

   kORA haina mpango na kwanza sijui hata kama bado ipo,naona ilishajifia ama kupoteza umaarufu kutokana na kujaa “uswahili” wapo manguli kibao akiwemo papa wemba eti hawajawahi kushinda kORA at the same time AWILO eti ndio kashinda tuzo nyingi zaidi kuliko mkongoman yeyote yule..!wewe hii inakuingia akilini kweli yani AWILO ni bora kuliko hata Youssou N’dour,Koffi,Papa wemba n.k.?

   • Stivin says:

    Kaka kubali tuu, kila kitu kiko wazi, Werra ni Mwanamuziki mkubwa kuliko Bwana mdogo JB, Werra ni balozi wa UNICEF, JB ni wa nini?

 2. edmas says:

  NADHANI UTAFITI HUU UMEMALIZA UBISHI WA MIAKA MINGI KUWA NANI NI MKALI. WAFUASI WA JB INABIDI WAIMEZE HII.

  WAZUNGU WANASEMA ”NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK”. SASA TUNA RIGHT YA KUSEMA KUWA WERRA NI MKAREEEEEEEEEEEEEE…..!

 3. Stivin says:

  Wera Wera! Kila siku nikisema Werra Azali Champion naambiwa leta data! Asante Digital Congo! hata Koffi hamfikii Werra Kwa sasa!

 4. K'Odero says:

  PiusMicky mbona usiwe majsiri mara moja na umtambue Werrason kwamba ni bingwa wa Congo badala ya kuingizaingiza jina la J.B. Mpiana kila unapomtaja Werra? Kuongezeaongezea nukuu za J.B haibadilishi ushindi huo.

  Edmas nakubaliana nawe kabisa! Hapo awali nilipotaja kwamba Werrason ndiye alikuwa nguvu wa utunzi ndani ya kundi lile awali la Wenge Musica BCBG 4 x 4 Tout Terrain, wadau kama akina Omari na ma Le JBnique wengine walizua malumbano eti mimi sina langu la kusema eti J.B ndiye alikuwa kichwa cha Wenge. Baadaye nikawaambia talanta na ujuzi wa Werrason haiwezi kufutwa na sauti la J.B hata kama yeye ndiye kiongozi wa bendi maanake jukumu la umaarufu wa Wenge ilikuwa ni sanaa kubwa wa Werra, J.B akiwa ndiye uso wa Wenge.

  Kinachonifurahisha hapa ni kwamba sasa hao wote wametulia tuli, kama maji ya mtungi, au kama shamba linalonganganiwa, hawana la kujibu maanake ukweli umejitokeza dhahiri shahiri kwamba kwa muda mrefu wamejifunika kwenye handaki la upuuzilifu na kudhani kile wanachokifahamu pekee kimetoshea ukweli wote.

  Samara Paul umenena jambo la busara kabisa. Wengi wamesema eti Concert Olympia yake J.B (1999) ndiye tamasha kikubwa zaidi kwenye historia ya muziki ya Congo lakini hayo yamepitwa na tukio ya baadaye ambapo Concert yake Werrason ya Kikwit (2006/7) ndiye iliwahi hudhuriwa na watu wengi zaidi kwenye historia ya Congo Music. kama ulivyotaja hapo pia, hakuna album yoyote ya Werra imewahi kukosa kufua dafu kwenye soko. J.B Mpiana hajawahi kushinda tuzo kikubwa chenye kiwango cha Kora, leave alone hata kuchaguliwa uwakilishi wowote wa kimataifa kama vile Werra alichaguliwa kuwa mwakilishi wa swala la watoto UNICEF na pia mwakilishi wa amani na Pope John Paul II. Kumbuka kwamba Werra alishinda Kora mara tatu, moja hapo ni Double Kora akituzwa na mwanamuziki wa kimataifa halimaarufu Shaggy.

  Kwa ufupi; WERRASON is an ‘International Heavyweight’ , while J.B. Mpiana is just a Local Hero

  • Hadj Le Jbnique says:

   UNACHANGANYA MAMBO MENGI SANA NA KUYAWEKA PAMOJA,HILO NI TATIZO JAPO HUJUI KWAMBA UNALO!

   • K'Odero says:

    Hadji hebu rudia ulilosema maanake hueleweki

   • Hadj Le Jbnique says:

    issue hapa hapa ni utafiti unaodaiwa kufanywa baada ya werra kuanza kujitegemea lakini wewe kwa makusudi umeamua kuhamishia hasira zake kwenye kutaka kuchakachukua historia ya wenge musica 4×4 tout terrain ambayo mnaiitaga wenge original kwa kujaribu kutumia huu utafiti kutaka kuumanisha umma kwamba werra ndio alikua anaibeba wenge kabla ya kusambaratika kitu ambacho ukiwa peke yako chumbani umelala unajua si kweli,niambie wimbo gani wa wenge ile ambao sauti ya jb haipatikani ndani yake bila kujali umetungwa na nani?mimi na hata wewe tunazijua nyimbo kibao ambazo sauti ya werra haimo,sasa hapo utasema nani alikua kichwa cha bendi?jibu hilo swali dogo tu ndio ntajua kama wewe ni mtu wa muziki ama ni mtu wa werra,maana tunao watu wa werra humu ndani wanajulikana,wao hawaujui muziki wanamjua werra tu basi,sasa na wewe ukijibu hapa tutajua tukuweke kundi gani,kama tukujumuishe na wenzako au tukuweke kwenye kundi la watu wa muziki.

    Na pia kama unayo maelezo yeyote ya sababu za waanzilishi wa wenge kumpisha “wakuja” jb awe kiongozi wao utakua umeisaidia sana hadhira inayosoma haya tunayoyaandika,mtuambie tu ilikuwaje jb akawaovertake waanzilishi na akawa yeye ndio kiongozi wa bendi yenye mafanikio?je alitumia ubabe na wote wakaufya mkia au ilikuaje kuaje?

    asanteni sana,sas twende hoja kwa hoja,mi sijisifu but hakuna kitu ninachokifahamu zaidi duniani katika historia ya wenge,na hii haikuja hivi hivi tu bali ni mapenzi yangu kwake na kuisoma sana hiyo bendi ikiwemo maisha binafsi ya wanamuziki karibu wote wa hiyo bendi,so mimi ni mtaalam(mtu anaejua mambo mengi sana katika kitu kimoja-wenge)wa mambo na historia yawenge musica 4×4 tout terrain

  • Anonymous says:

   Kama ni suala la sauti basi Heritier ni Mkali kuliko Werra, kwa sababu sauti ya heritier iko katika nyimbo zote!

   • Anonymous says:

    habari ndio hiyo unazani kwanini werra anamng’ang’ania,anajua ndio anaibeba bendi

 5. Anonymous says:

  mdau kuweka kumbukumbu sawa tu hiyo concert ya kikwit unayodai ilivunja rekodi ya mahudhurio ilikua na show ya wazi,yani kiingilio ilikua ni mguu wako tu wa kukuwezesha kufika pale kwani mdhamini kampuni ya bia ya congo alilipa kila kitu na werrason akawadhulumu wanamuziki wake hakuwapa chochote ndio moja ya sababu ya wanamuziki waliokua wanambeba kama yule mpiga solo na mtaalam wa arrangement ya muziki jina lake nimemsahau kidogo kumkimbia

  • K'Odero says:

   nawe mdau asiyekuwa na jina Kikwit ilihudhuriwa na watu au na nzige na panzi? Show iwe open ama paid bado ni show maanake hata J.B na Koffi wamewahi kuandaa open shows lakini hazikuhudhuriwa kiasi hiki. Event yoyoye ikishaingia kwenye kumbukumbu, haina haja muanze kuibadilishia details ni kama nyie ndio mlichapisha hizo taarifa kwenye nakala

   • Stivin says:

    Hiyo show ya JB ya Olimpia aliifanya mwaka 1999, wakati akiwa bado na nguvu kubwa ya Wenge BCBG ambayo werra alimuachia, kumbuka kuwa Werra ndie alieajiri karibu wanamuziki wote BCBG akiwemo Mpiana, halafu nashangaa kila siku Olimpia Olimpia ina capacity ya watu 4000 wakati Zenith ina capacity ya watu 6300 fanyeni homework.

 6. Hadj Le Jbnique says:

  OUT OF TOPIC:BREAKING NEWZZZ TOKA KIN

  Kwa wapenzi wa JB MPIANA na BCBG,jb mpiana na bendi yake wamepata mwaliko wa kupiga concert ndani ya United Nations department of kinshasa,hii ni records kwani anakuwa mwanamuziki wa kwanza wa congo kufanya kualikwa kupiga show kwa ajili ya watu hao wa kimataifa.

  • K'Odero says:

   Ina dhamana gani ikilinganishwa na uzito wa mada tunayozungumzia hapa kwa sasa? Mbona haya yanatajwa tu wakati huu na haina nukuu lolote pahali pengine? Mnanifurahisha sana

 7. mamaa prezident mwasi ya mokonzi says:

  Hivi malewa no 2 jamaa ataitoa lini mbona imekuwa kama tamthiliya isiyoisha ya dayz of our lives, werrason bwana kwa vituko na mashabiki wake kutengeneza tafiti za uongo na ukweli hajambo

  • K'Odero says:

   Afadhali Werra kwa mwaka iliyopita alikumbwa na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kuvamiwa, kuumizwa na hata shughuli za kisiasa kufuatia uchaguzi uliopita, je malewa2 ukilinganisha na namna purukushani za JB na Pipiyu zilimweka nje kwa miaka kabla kutoa Kipe Yayo na huku upakuaji wa Suit et Fin hata kwa internet karibu ikuwe rekodi nyingine?

 8. Stivin says:

  Mpiana ni bwana mdogo, bado anaendelea kutembelea nyota ya Wenge Musica BCBG, zaidi ya nyimbo alizosaidiwa na Makaba kuarange ndani ya Wenge sijasikia wimbo mwingine wa maana wa Mpiana, ndio maana amebaki kupiga kelele Mulolo wangu Mulolo wangu, si atunge mwingine mzuri kama huo? JB ni historia!

 9. Benmundele says:

  Naipenda sana blog hii ya Pius kwa maana inatupa up to date habari kuhusu wana Mziki wa kikongo nasema Shukrani , lakini haimaanishi kama wewe ni mfuasi Sugu wa JB Mpiana Lazima Kila unapo mtaja Werrason pia umguzie JB Mpiana..hapo umekuwa na unuonge flani wa mapendeleo

  Inakera pia..Kama Werrason ni Mkareeee ni Mkareeee na kama fanatic mkubwa wa Werrason sikubaliani na Jinsi unavyofanya blogging kwa kumpa JB Mpiana Umaarufu Usiofaa.

  Werrason ni Mkareee na ndio itasalia vivyo hivyo….Album mpya ya Mpiana ya lets get serious here ni bure kabisa lakini bafans wake hawakubali hilo kwa machungu wanadungadunga Werrason na yetu kali ya Techno Malewa…..

  Pius…kuwa fexible ili blog hii iweze kupata umarufu kote duniani, usiegemeze fikira zako pande moja….(ANALETA MAMBO MSICHOKE)

 10. Benmundele says:

  @K’Odero sielewi mbona Pius anamiliki unyonge huo wa Kisiasa.

  Napenda talanta yake Nzuri ya blogging na utafiti wa hali ya Juu sana kwa sababu ya sisi wapenzi wa Congo Music…asitulazimishe kumpenda JB Mpiana….

  Tafadhali nakuomba bwana Pius uitoe picha ya JB Mpiana katika Umaarufu wa IGWE… Mgala mpe haki yake…

  • K'Odero says:

   YAA WERRA YAA WERRA YAA WERRA !!!!!!

   Hata akiamua kukimya nina hakika ametupata loud and clear Bw. Benmundele

 11. Hadj le Jbnique says:

  Mbona mawerasonique mko kihistoria zaidi???naona mnatapatapa tu wa2 walele wawili mmejaza macomment kibao za kihistoria mmekazana De la Forret alifanya de la forret alifanya,tunataka kusikia ya sasa,ana nini sokoni,ana style gani mpya mwaka mzima wa jana?kimya,mmoja anasingizia ajali aliyoipata eti mwishoni mwa mwaka jana,je mwaka mzima alikua wapi au ndumba zimeisha nguvu baada ya kuambiwa akitaka mafanikio tena inabidi this time afe yeye kwa ajali,mungine anasingizia uchaguzi wa congo,je ni Le Roi De la Forret pekee ndio alishiriki kampeni za joseph kabila wa kabange mwana ya muzee?jibu hapana,so wat happened to u bana zamba last year no even a single concert in Poto mkiulizwa ooh visa je huo ubalozi wenu wa unicef bado hauwasaidii kuaminika kupewa visa?mbona bcbg wanaenda na kurudi daily?juzi mungu wenu ‘wata’ ya ngiama kawatingisha kidogo anahama bendi na kurudi bcbg alikofundishwa muziki PPU acha papaa na Exocee mobali ya mamaa pastor sylvia mampata a.k.a. Le Roi De la Forret aweweseke na mshukuru jb alishaweka msimamo hataki wanamuziki toka bendi kubwa kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

  • Stivin says:

   Kila siku haji unasema mwaka 2011 Werra hakwenda Ulaya hkwenda Ulaya hapa ni Manzese?

   • K'Odero says:

    Hadji tafadhali kwa ufupi naomba tusaidiane hivi:

    1. Mimi sihitaji kuwekwa kwenye kikundi chochote na mtu yeyote ati ‘Team Werra’, Team Wenge’, mara team j.b. especially kama ni wewe ndiye unaweka watu kwenye vikundi, mimi sio mteule wako

    2. Wewe ni mtu mmoja na una kura moja pekee, je wewe ndiye kipimo cha misimamo yote na maoni yote ambapo hata baada ya utafiti zingine na machapisho hapo awali, bado tu ni lazima wewe ndio uaminiwe kuliko wengine? Wewe ni mtaalam ulitahiniwa na kupitishwa na nani?

    3. Kama haukunipata basi pole kwasababu nilisema tena clear sana; ‘hata kama J.B. alikuwa kichwa cha Wenge kama president wa bendi, Werra alikuwa na jukumu na changio kuu la utunzi ndani ya Wenge kwa hivyo Wenge haikuinuliwa na mkono mmoja pekee eti J.B. J.B. J.B. peke yake kila saa, hapo usitudangaje kwa kujificha ndani ya taji la kujiwekea ya mtaalamu. Wenge ilikuwa team ya wenye talanta tofauti kila mtu akiwa ameshikilia upande wake na J.B hangeweza uongozi bila kazi kubwa alilofanya Werra kama mwimbaji mwenza, accounts manager na pia second singer in command. Usigeuze jina Wenge Musica BCBG Tout Terrain ati iwe ”Wenge J.B. Mpiana Kichwa”…

    4. J.B anataka kurecruit talanta mpya miaka hiyo yote alikuwa amekazana na wakongwe kwenye bendi hakujua manufaa wa talanta chipukizi? Baada ya Werra kumuonyesha nuru ya usajili wa new talents ndio siku hizi amejifunza? Watta alitutisha kwani Watta anashinda the invincibles wenye walihama bendi hapo awali kama Ferre? Tangu Allain Makaba atoke mbona music arrangement imempotelea j.b mpaka sasa huku Werra album zake zote zikiuza kama keki moto sans nouvel arrangeur? Unadai Werra hakufanya lolote mwaka jana, kando na jibu uliopewa hapo juu na Stivin, mbona umesahau J.B hakutoa chochote between Anti Terro 2004 na Kipe Yayo 2007 na haikuwa issue, sasa mwaka moja ya Werra inakua chanzo cha ubishi? Kweli nyani haoni ngokoye?

    5. Machungu na ubinafsi wa msimamo makali haitabadilisha ukweli uliotolewa na kikundi kirasmi maanake wewe kama mwenye kura momoja hakuna utafiti umetufanyia ya kudhibitisha madai yako eti wewe ni mtaalam. Utaalam unaonyeshwa na ushahidi (research, publications, keynote addresses etc) Mtaalamu ana balanced opinion na fair views kwa pande zote wala sio kukwamia msimamo mmoja hadi jina lako pekee ni ishara ya upande ulioegemea.

   • Stivin says:

    JB alikuwa interviewed na Werra, akakubaliwa Wenge kwa sababu ya sauti yake nzuri hilo halina ubishi, Ila Haji analazimisha ionekane kuwa Wenge ni JB Mpiana kwa sababu alikuwa kiongozi, uongozi wa JB ulikuwa ceremonial zaidi, Kiongozi gani hakuwa na madaraka na Fedha za Bendi? Unajua kuwa JB aliwahi kumwambia Werra kuwa akiwa kama kiongozi bendi imnunulie gari kama la Koffi? Unajua Werra alimjibu nn? alimwambia kitu pekee unachoweza kufanya bila kuulizwa ni kuchubua uso wako na sio kutumia fedha za bendi kwa faida yako.

   • K'Odero says:

    Ha ha haaaa…… Stivin wapi yule ‘mtaalam’ atuambie kama anajua hiyo pia, na kwa nini hajawahi kutuelezea juu ya J.B kuhojiwa na Werra kisha akaanza kudai starehe starehe kando na vipodozi?

   • Hadj Le Jbnique says:

    Ha ha haaa stiv unaweza kutusaidia kutuhakikishia hiyo video uliyoichomekea hapo ni ya mwaka jana na hapo ilikua ni wapi????

   • Anonymous says:

    uhakikishiwe kivipi, hiyo ni ya mwaka jana kaka

   • Hadj Le Jbnique says:

    Odero hii yako,hakuna pahala niliposema lazima uniamini mimi,lakini ungejibu basi hoja kuliko kutoa povu jiiiingi bila sababu za msingi,twendeni hoja kwa hoja tutaelewana tu,narudia tena,niambie wimbo gani wa wenge ile ambao sauti ya jb haipatikani ndani yake bila kujali umetungwa na nani?mimi na hata wewe tunazijua nyimbo kibao ambazo sauti ya werra haimo,sasa hapo utasema nani alikua kichwa cha bendi?ila nimefurahi angalau baada ya kukutingsha kidogo umerudi kwenye mstari na kukiri kwamba wenge kumbe ilikua ni team na si werra,Rejea kipengele hiki ulichoandika kumtukuza werra na si team wenge musica nzima,ulisema hivi “Hapo awali nilipotaja kwamba Werrason ndiye alikuwa nguvu wa utunzi ndani ya kundi lile awali la Wenge Musica BCBG 4 x 4 Tout Terrain, wadau kama akina Omari na ma Le JBnique wengine walizua malumbano eti mimi sina langu la kusema eti J.B ndiye alikuwa kichwa cha Wenge. Baadaye nikawaambia talanta na ujuzi wa Werrason haiwezi kufutwa na sauti la J.B hata kama yeye ndiye kiongozi wa bendi maanake jukumu la umaarufu wa Wenge ilikuwa ni sanaa kubwa wa Werra, J.B akiwa ndiye uso wa Wenge”mwisho wa kukunukuu.

    Na hii nairudia pia maana unajifanya hukuiiona,je uko na maelezo yeyote ya sababu za waanzilishi wa wenge kumpisha “wakuja” jb awe kiongozi wao utakua umeisaidia sana hadhira inayosoma haya tunayoyaandika,mtuambie tu ilikuwaje jb akawaovertake waanzilishi na akawa yeye ndio kiongozi wa bendi yenye mafanikio?je alitumia ubabe na wote wakaufya mkia au ilikuaje kuaje?unadhani nini kiliwasukuma?tuwekane sawa kwanza hapa then tuendelee..mwisho nadhani wata na umuhimu wake kwenu bado huujui lakini de la forret mwenyewe anajua bila wata hakua maison mere,sasa hebu mstazame na kumsikiliza hapa kwenye kitu chake “Remise et reprise” a.k.a. Tressor Mputu ndio utanielewa ninachokisema na kuachana na historia ya hao invicibles wako

   • K'Odero says:

    Hadji unajua ni kwa nini sijisumbui na kujibu maswali yako finyofinyo hata ukinichokora? Ni kwa sababu ur not worth it. Mada huu ni umaarufu wa Werra lakini umeshinda umekwamia uongozi wa JB kana kwamba maisha yako yote inategemea ukubwa wa JB zaidi ya mambo mengi muhimu. Mimi kawaida sipendi watu wa kunirudisha nyuma na sitakupa mileage yenye hustahili kwa kujibizana nawe huku sioni authority yoyote kwenye utaalam unaokazania. Hebu pumzika baada ya kukubali kwamba wewe sio reseacher au specialist. Sawa

   • help Belize says:

    Your blog post is absolutely on point! This will definitely be very useful for me when I get a chance to create my own write up. Your site is so mind blowing that my mouth starts bleeding when I look at it. Not everyone is great at thinking outside of the box and still being detail oriented. I just now found this blog but I’m at the gym as I write this so I’ll have to read the rest of this later on when I get back home and I’m able to read it without being distracted. Listen to your feelings then back it up with some facts.

 12. Hadj le Jbnique says:

  Mbona mawerasonique mko kihistoria zaidi???naona mnatapatapa tu wa2 walele wawili mmejaza macomment kibao za kihistoria mmekazana De la Forret alifanya de la forret alifanya,tunataka kusikia ya sasa,ana nini sokoni,ana style gani mpya mwaka mzima wa jana?kimya,mmoja anasingizia ajali aliyoipata eti mwishoni mwa mwaka jana,je mwaka mzima alikua wapi au ndumba zimeisha nguvu baada ya kuambiwa akitaka mafanikio tena inabidi this time afe yeye kwa ajali,mungine anasingizia uchaguzi wa congo,je ni Le Roi De la Forret pekee ndio alishiriki kampeni za joseph kabila wa kabange mwana ya muzee?jibu hapana,so wat happened to u bana zamba last year no even a single concert in Poto mkiulizwa ooh visa je huo ubalozi wenu wa unicef bado hauwasaidii kuaminika kupewa visa?mbona bcbg wanaenda na kurudi daily?juzi mungu wenu ‘wata’ ya ngiama kawatingisha kidogo anahama bendi na kurudi bcbg alikofundishwa muziki PPU acha papaa na Exocee mobali ya mamaa pastor sylvia mampata a.k.a. Le Roi De la Forret aweweseke na mshukuru jb alishasema hatapokea dogo yeyote toka kwenye bendi kubwa za congo kuepusha migogoro bali atarecruit new talents toka kongo nzima ili kumsaidia rais kutengeneza ajira kwa watoto wa congo.

 13. Hadj le Jbnique says:

  Sorry kwa usumbufu wadau nimejikuta natuma 2 comments bahati mbaya cuz natumia nokia yangu ya torch halafu nilikua naandika fasta cuz I was in the train,but nashukuru ujumbe umefika though

 14. sabra kazi says:

  Werra yuko juu sana hata ukiandgalia kwenye you tube nyimbo za werra ndo zimeangaliwa sana kwa mamilioni kuliko jb. Werra mkali sio siri. Wanamziki wake wote vijana pia weny vipaji vikubwa.

  • stivin says:

   Nimewahi kumchalenge Hadji atuwekee wimbo wa JB ambao umeangaliwa na watu milioni moja You tube akashindwa!!!

   • Hadj Le Jbnique says:

    SIKUSHINDWA KAKA,BALI SIKUONA KAMA HIYO NI DETERMINANT YA UBORA WA MUZIKI,UKWELI NI KWAMBA UNAWEZA KUWA MASHUHURI LAKINI HUNA MUZIKI,NIMEWAHI KUKUTOLEA MARA KADHA MFANO WA AWILO,ALIWAHI KUWA VERY FAMOUS AFRICA KULIKO MWANAMUZIKI YEYOTE WA CONGO LAKINI HAKUA NA MUZIKI WOWOTE UNAOELEWEKA,NA HICHO KI AWARD KIMOJA CHA KORA MNACHOPIGA NACHO KELELE YEYE ALICHUKUA 3 KWA MPIGO.MFANO MUNGINE NI HAPO BONGO,TMK WANAUME WALIKUA MASHUHURI SANA LAKINI HAWAKUA NA MUZIKI WOWOTE WA MAANA UKILINGANISHA NA EAST COAST TEAM,WAO KAMA WERRA WALIKUA MAARUFU KWA KUWA WALIJIPAMBANUA KAMA ALAMA YA WATU WA KAWAIDA(WA USWAHILINI) AMBAO HUWA NDIO WENGI MAHALI POPOTE AFRICA,HIVYO KUJIKUTA WAKIPATA SAPOTI KUBWA KUTOKA KWA WATU HAO BILA KUJALI WANAIMBA NINI,WAO HUONA KAMA WAKO CONNECTED NAO NA KUAMUA KUWAPA SUPPORT,NA KWA WERRA HIYO ILIKUA NI STRATEGY NILIWAHI KUELEZA HAPA (REJEA POST YANGU KUHUSU KITABU CHA HISORIA YA WERRASON(REJEA POST YA KITABU CHA HISTORIA YA WERRA CHATOKA,IPO HUMU)STRATEGY HIYO ALIPEWA NA MWANDISHI WA KITABU HICHO,NA KWELI IMEKUA IKIMSAIDIA,KWANI JB NA KOFFI WAO TARGET YAO NI KWA WATU “CLASSY” WENYE NAFASI ZAO,MAY BE WAKO WRONG BUT NDIO HALI HALISI,SO INAWEZA KUWA CHALLENGE KWAO KUBADILIKA NA KUWATAZAMA WATU WA KAWAIDA PIA

   • K'Odero says:

    Hadji nilishakujibu ya kutosha, kama bado huoni uwazi na kuendelea kusisitiza mambo mepesimepesi basi ni heri tufunge mada huu. Pius hebu leta flava nyingine

  • K'Odero says:

   Sabra na Stivin hebu mnisaidie kumkumbusha huyu mtaalamu kwamba facebook page ya Werra iko na likes 28,759 kwa sasa huku ya j.b ina 1,779 pekeee…… nani kama Igwee Noel Ngiama Makanda Werrason Le Roi De La Forret Le Grand Formateur

 15. Hadj Le Jbnique says:

  ‘Ha ha haaaa…… Stivin wapi yule ‘mtaalam’ atuambie kama anajua hiyo pia, na kwa nini hajawahi kutuelezea juu ya J.B kuhojiwa na Werra kisha akaanza kudai starehe starehe kando na vipodozi?’
  Sayz odero

  Nakujibu hapa,issue ya utaalamu iskunyime usingizi sana,huo ndio ukweli,clan wenge nimeisoma na kuifanyia research ya kutosha,so naijua kuliko kitu kingine chochote hii haiwezi kubadlika,kuhusu issue ya kuhojiwa jb na werra alipokuja kuomba kazi wenge baada ya kuwa introduced kundini humo na mmoja wa member waanzilishi Jean Belix Luvutula ambae alikua akiishi mtaa mmoja na kwa kina jb mbona niliiadress hapa kwenye post yangu kuhusu kitabu cha historia cha werra,ngoja hapa kama hukupata chance ya kuisoma wakati huo,https://spotistarehe.wordpress.com/2012/04/18/kitabu-cha-historiabiography-ya-werrason-chatoka/,siko hivyo kama unavyofikiria,sema mimi huwa napenda kusema kile ambacho kipo lakini watu huwa hawapendi kukisikia,werra akifanya jambo zuri nimekua nikilisema hapa na wazoefu wa jukwaa hili kama wataweka unazi pembeni watanitetea kwamba licha ya upenzi wangu kwa papa na daida salvatora de la patria jb mpiana lakini pia akichemsha nimekua nikimgonga vile vile,mfano mara kadha nimesema hapa kwamba sipendi style ya jb ya ku pay attention zaidi kwenye live concerts muziki unakua mnene zaidi kuliko kwenye studio recording ,lakini mashabiki mashabiki wa werra kwao ni tofauti kidogo,wao kwao jamaa hakosei wananikumbusha ile kauli ya mkubwa hakombi mboga akikomba ili kuondoa ukali wa maneno tunasema kaipenda lakini ukweli unabaki palepale kakomba mboga,ndio mana mimi huwa nasema nyie jamaa sio watu wa muziki bali ni watu wa werra.

  • Hadj Le Jbnique says:

   Odero,gonga hapa nadhani utaisoma freshhttps://spotistarehe.wordpress.com/2012/04/18/kitabu-cha-historiabiography-ya-werrason-chatoka/

  • K'Odero says:

   Siku nitakapoambiwa kwamba Hadji alifanya research ya muziki akachapisha publication ama isemekane ulitunikiwa zawadi ya udadisi wa ngoma ndipo nitarudi kwako kukusikiza, lakini kwa sasa, hautanilazimu kukusikiza ukijitetea kwamba wewe msomi wa muziki. Nadhani nina vitu vingi vya maana vya kufanya kuhusu muziki

 16. Hadj Le Jbnique says:

  “Hadji nilishakujibu ya kutosha, kama bado huoni uwazi na kuendelea kusisitiza mambo mepesimepesi basi ni heri tufunge mada huu. Pius hebu leta flava nyingine”
  sayz Odero

  Odero hakuna ulichokijibu kuhusu ilikua kua vipi mpaka jb ambae tunaona kwamba hakua founder wa hiyo bendi ana alikua kuomba tu kazi na de la forrret ndio aliemuinterview mbele ya kina General Kwek Le fondateur Didier MaselaDidier Masela na Jean Belix akaja kuwa kiongozi????

  Na pia nimeuliza werra ana nini skoni au kwa sasa na ana style gani toka mwaka jana mzima mpaka sasa ambayo imewashika watoto wa congo?there ar somany unanswered question but u try to dodge na kujaribu kushut down questioning,huwezi kuja hapa kusema tu then utegemee kutokua tested kwa maswali,never,umust be prepared bro!

  Mimi naanza na jb mwaka jana,amekuja na style kibao,akianza na amataka na mpunda,biloko,rota rota,liboko,hizi hapa kwa vitendo sio hadithi,weka za werra last year tuone hizo style zake mpya.

 17. Anonymous says:

  Ok odero kila la kheri..but mawerasonique wengine ntaendelea kuwapa challenge mtuambie mna kipi sokoni kwa sasa ndio twende sawa otherwise sitakaa kimya mkija na hizo he said she said zenu lazima muwe mmejiandaa vya kutosha kufanya mjadala,zile zama za eti wanasema jb alimwambia werra,werra alimwambia jb zimepita sana,nowdayz thanx dunia imekua kijiji ukitaka kulifaham jambo kiundani milango iko very open utalifaham tu,hakuna kudanganyana tena kwa hadithi za kutunga.Mwisho kwa werrasonique yeyote wa ukweli anaejua malewa 2 itatoka mwaka gani atufahamishe hapa,otherwise piga kimya kama hata wewe huna info yoyote ya bendi unayodai kuipenda

 18. stivin says:

  Hahaha, ukiangalia kilichoko sokoni kwa sasa, nadhani hata Fabrice kampita huyo Mungu wako Mpiana, hahaha, ina maana Justine beiber ni mkali kuliko Michael Jakson kisa ana albamu sokoni kwikwikwi, Kajipange upya Hadji, JB ni bwana mdogo sana kwa Werra, wala hamkaribiii.

  • Hadj Le Jbnique says:

   kwa hiyo kijana wa miaka 20 leo ukimuuliza nani mkali wa muziki atamtaja michael jackson!!!!!!

   acheni ujanja ujanja wa kuishi kihistoria,jamaa inabidi azihirishe ubora wake kwa kwanza kuitoa malewa 2 na pia aje vitu vingine vya kisasa,sio kukalia ooh tulijazaga zenith sijui kikwit haijapata kutokea,tunataka sasa mnafanya nini?

   N astiv unapenda sana kuikumbushia concert ya de la forret zenith lakini unasahau kwamba mafanikio ya show ni promo na promo zio kazi ya mwanamuziki kwa kuwa yeye anakua kishalamba dola laki moja yake tokea akiwa kinshasa so ni kazi ya waandaaji kuitangaza show,huwa napenda sana kuwapa mfano wa concert ya zenith ya koffi 2009 ambayo ni historia jinsi waandaaji walivyojipanga kwa promo toka bendi inatua airport ni macamera tu mpaka siku ya show,na matokeo yakawa haya……..

  • K'odero says:

   Ndugu Stivin napenda nama umeamua kutojibizana zaidi na paragasha huyu tangu hii mada aianze amekwamia mambo mawili pekee mwaka mzima eti oooo… J.B kiongozi wa Wenge, ooooo…. nini mpya mwaka huu kutoka WMMM, ooooeeeeaaaaauuuuuooo…..
   mtu kama huyu tunafaa tumhurumie maanake umaarufu wa Werra imempiga shock kubwa hawaamini Werra anaweza kumpwiku hata Koffi (J.b hata hatumhesabu hapa) kwenye ufwasi. Ati Kora ni fake kwani Awilo mtu mmoja atatia mchanga umuhimu wa Kora yet wazito wengine kama Extra Musica, Kidjo, Mtukudzi, Brenda, Keita, Yossour Ndour, Wazekwa, Meiway na Koffi wote walipiatia mkojo huo? Uchungu wa huyu bwana ni kwamba J.b hakuwahi hata kuwa nominated ndio maana anaipaka Kora matope huyu jamaa anafaa ahurumiwe tu sana. Anajirudiarudia na ‘yepi mapia…j.b kiongozi…ooooo….eeee….’ hata J.b hakutoa chochote 2004-2007 mbona hujajibu hiyo? Hata Mobutu sese seko alikuwa kiongozi lakini yu wapi sasa? Achana na fixations za huyu mtaalam hizi ni dalili za frustration na bitterness kwani ‘nini mpya’ imekuwa jambo la uzito kushinda swali hujajibu mpaka sasa? Ana aibu kubwa alipogundua kwa nini facebook page ya Werra ni 20 times more visited than J.b na hakuna wimbo wa j.b imepata 1 million YouTube hits!!!!!…………….., ameze wembe na asitijibu tena, looser!!!

 19. Hadj Le Jbnique says:

  muziki haupigwi na kuchezwa kwenye face book kaka,hatutaki kuwa watu wa kizamani ndio mana tunataka kuona vitu vipya…u talking about kora leo 2012!kweli umekwama kwenye shimo refu sana la mambo ya kizamani,unakasirika watu wakiuliza mambo mapya unataka kulamizimisha tuishi kizamani kama wewe au?lete hoja acha vioja na ni vyema ukazungumza lugha unayoiweza kuliko kuforce kiswahili,hapa tunazungumza kila lugha kuanzia lingala mpaka jaluo si lazima sana swahili kama ni ngumu,na mwisho wa siku hapa huwa tunajadiliana kistaarabu zaidi kwa hoja,ndio utamaduni wetu hapa ndio mana tumedumu licha ya tofauti zetu,na upinzani wa jb na werra its given dunia nzima katika mitandao na yote ni katika kuleta changamoto wewe kama unafanya ni kama big deal saaaana kimpango wako lakini sisi tutaendelea kupeana challenge ili kuchangamsha baraza letu hili tusikae kama tuko msibani.Habari ndio hiyo.

  Na huo mfano wako wa mobutu kwa nini usiutumie kuacha kuzungumza mambo kizamani ya kora ambayo hata sijui ilikufa mwaka gani kama mobutu tu,hutaki kabisa kuzungumzia uongozi wa jb kwa kuwa unadai ilikua ni zamani lakini unapeeeenda kuzungumzia kora utadhani jamaa alishinda mwaka jana,ha ha haaaa!nadhani uko na stresses tu kaka,nakusamehe bure.

  kwa kukukumbusha tu ni kwamba internet ya jb ilishawahi kuwa nominated kwenye hiyo kora yako,kama kitu hufahamu uliza usilete uzishi usio na mpango.

  Hoja zako zote nazijibu lakini wewe una dodge,ukishikwa pabaya unadai huna muda wa kujibizana at the same time kiujanja unajibizana,acha uoga,come out brother,about J.b hakutoa chochote 2004-2007,”stay tuned” nitaweka hapa makala kinaga ubaga kuelezea watu wasome kilichosababisha hali hiyo kwa watakaopenda watasoma,kama hutaki unaacha..hulazimishwi.

  • K'odero says:

   Ah! Ur so petty Hadji, spare me please!
   Be civil for only one minute n learn to shut up,
   Nothing uv said so far that will change anything

   • Hadj Le Jbnique says:

    labda uache kuingia humu tu lakini kuninyamazisha kirahisi namna hiyo huku wewe ukiendelea kuchonga itakua ngumu mzee,utaharibu keyboard yake kwa kutype kwa hasira,mimi nacheka tu kila unavyozidi kukasirika na kununa mimi ndio naona raha,sawa sawa muzee..karibu sana sports starehe siku nyingine

   • K'odero says:

    Maybe u bypassed the oral stage, u sound so retarded. Ur next reply will confirm it

 20. Stivin says:

  Hadji wewe ndo unatype kwa hasira kwa sababu Mungu wako JB kaachwa mbali na Werra, kila kitu kiko wazi, Fan Base, Mauzo ya Albam hata Digital Congo ya Wakongo yenyewe imethibitisha hilo, wewe nani upinge? Kameze Wembe, Wera Champion Weraaaaaaaaa!

 21. Hadj Le Jbnique says:

  Ulifikiri swahili rahisi now imekushinda sio? but it’s not gonna help u either…chungu lakini ni dawa,unaumwa tulia utibiwe upone,that’s my confirmation,right?

 22. Stivin says:

  Wewe Hadji ndo unatakiwa umeze hata kama chungu kuwa Werrasone is the most popular Congolese Musician hata kama humpendi, chungu lakini meza! Werra Werra!

 23. Werra ni mkali kuliko JB. Anaesema kuna nyimbo Werra hakuimba Wenge original hajui muziki. Kuimba si lazima uimbe verse. Werra alikuwa mnogeshaji wa kibwagizo! Hakuna wimbo ambao hakuimba kabisa.

  Bado tunabishania umahiri, kuna satellite+2 tuirejee

 24. rashidi siganda says:

  napenda sana

 25. Its my good pleasure to go to your blog site and to enjoy your good posts here. I like it a lot. I can feel that you just paid significantly interest for anyone posts, as all of them make sense and are very practical.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: