R.I.P Mafisango, Utakumbukwa Daima

Mchezaji wa Simba Patrick Mafisango amefariki alfajiri hii baada ya kpata ajali ya gari maeneo ya Tazara.

Habari zinasema Mafisango alikuwa na abiria wengine watano wakati mauti yakimkuta, Kwa mujibu wa Patchou Mwamba ambaye alikuwa Mochuari alipoongea na Spoti Starehe anasema kuwa Mafisango alikata roho mara alipopata ajali hiyo ambayo ilitokana na kukwepa Pikipiki.

MAfisango atakumbukwa kwa mchango mkubwa aliotoa kwa timu ya Simba kwa upande wa soka la Tanzania, Hakika Simba imepoteza talanta ambayo bado mchango wake ulikuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa.

Jana Kocha wa Taifa wa Amavubi ametangaza kumuita Mafisango kwenye kikosi cha Timu ya Taifa na ilikuwa anondoke aende kujiunga na wenzake. Mafisango atakumbukwa hasa baada ya kuiteketeza Yanga na hivi majuzi ndiye aliyekosa Penalti pamoja na kipa Kaseja wakati Simba wakicheza na AL AHLY- SHANDY.

Mungu ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu – Amina

15 Responses to R.I.P Mafisango, Utakumbukwa Daima

 1. Ismael Mhina says:

  Tunahuzunika sana wapenzi wa mpira wa miguu kwa kifo cha Mafisango lakini hatuna budi kumuombea kwa mnyezi-mungu apumzike mahali pema peponi aamina

 2. Anonymous says:

  Tulikupenda sana mafisango ila Mungu amekupenda zaidi .RIP Motesa

 3. Hadj Le Jbnique says:

  poleni sana watu wa simba kwa kuondokewa na mchezaji wenu,pia pole nyingi sana ziende kwa watoto wa congo na ulimwengu mzima wa wazungumza lingala kwa kuondokewa na mcogoman/mnyarwanda huyu.Nawaliwaza kwa wimbo huu wa huzuni toka kwa koffi na cindy le coeur ambapo waliutunga na kuuimba ikiwa ni maalum kwa ajili ya kumlilia Edita sassou nguesso aliyekuwa binti wa mzee denis sassou ngeusso na mke wa rais omari bongo wa gabon kufuatia kifo chake.

  R.I.P. PATRIKE

 4. Anonymous says:

  Nasikitika sana na kifohiki ila kaziyamungu aina makosa tumuombe mwenzetu apokelewe namungu umuhifadhi mahalipema peponi aaamin

 5. Fidelis Siriwa says:

  ni pigo kubwa sana kwa clabu ya simba pamoja na timu ya taifa ya rwanda kwani mchango wake kwenye mchezo wa soka bado ulihitajika sana.

 6. Godson laurent says:

  Nilipo skia taarifa hizi nimeona kama utani lakin kumbe kweli jamani mbona wa africa tuna kufa gafla kuna nn lakn jaman mim nimeenda kwa pokea simba uwanja wa mwalim nyerere tena nikamuona mafisango akiwa amevaa phone za musck maskion eti leo amekufa dar sina hata cha kusema poleni wana simba r i p mafisango we love you forever

 7. jamani nimeshtushwa na kifo cha mafisango niliposikia redioni taarifa za kifo chake mapema asubuhi vijana siku hizi ndio tunaoondoka tukiwaacha vikongwe nani atawazikwa hawa!! haya ni mapenzi ya M/Mungu hayana makosa anayemtaka ndiye atakae mchukua rest in peace Patrick

 8. KIBINAKANWA says:

  kiukweli ni kwamba nipigo limetukuta lakini hatunabudi kulikubali kwani kuitu kilichopangwa kutokea hakiwezi kuzuilika na mwanadamu wa kawaida. MAFISANGO tunakupenda lakini kifo kime kupenda zaidi. umekuwa mwema ktk nchiyako, ktk klabuyako ya simba na pia ktk jamii unayo ishi, ndiomaana ukawa na ujasili na roho ya huruma ya kuokoa maisha ya mwendesha pikipiki na kupoteza UHAI wako. mungu akulaze mahala pema PEPONI….AAAMIIINAAA.

 9. A.LICHUMBU says:

  Ninaumia sana roho jinsi ninavyompenda ila mungu kampenda zaidi

 10. numerous good data and inspiration, each of which I have to have, thanks to give such a valuable information and facts here.

 11. Really good blog and excellent and articles or blog posts.worthwhile style and design, as share excellent stuff with very good suggestions and ideas.

 12. Anonymous says:

  R I P

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: