PATRICK MUTESA MAFISANGO Updates

May 17, 2012

385662_412941292073589_11436933_n

Kwa mujibu wa Mitandao jamii ambamo picha hii imewekwa, Hili ndilo gari alilopatanalo ajali Patrick Mafisango usiku wa kuamkia leo mitaa ya Chang’ombe.

Mipango ya kuzika au kusafirishwa inafanyika na Kiongozi wa Simba Ismail Aden Rage amesema ataujulisha Umma baada ya kuwasiliana na kuzungumza na familia ya Marehemu.

Mungu amlaze mahala pema peponi Amen.


TAFITI: Werasson ni Maarufu kuliko wanamuziki wote, Kama Papa Wemba miaka ya 70 – 80

May 17, 2012

image

Werrason Ngiama Makanda

image

Papa Cherry Le Suvereee

Werason amekuwa ni mwanamuziki mwenye wafuasi wengi tangia Wenge BCBG iparanganyike, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Digital Congo Werason ameweza kufikia record iliyowekwa na Papa Wemba miaka ya 70 na 80.

Tangu kuvunjika kwa kundi hili mwaka 1997 Werason amekuwa hapewi nafasi na JB Mpiana huku wakipumuliana kwa mashabiki na umaarufu.

Utafiti huo umechapishwa kwenye mtandao maarufu wa Digital Congo unasema kuwa Werra amejizolea umaarufu si ndani ya Congo pekee bali hata nje ya Congo. Kadhalika utafiti huo unasema kuwa Werrason amekuwa akipendwa zaidi na “walala hoi” na hii inatokana na tabisa yake ya kufanya maonyesho mengi sehemu wanazoishi watu hao huku JB Mpiana akiwa na mashabiki wengi wenye maisha ya kati na matajiri.

Wenge ambayo iliingia kwa kasi katika ulimwengu wa burudani kwa staili ya SAPE (société des ambianceurs et des personnes élégantes) ambayo ilianzishwa na Papa Wenga, lengo la Papa Wemba ikiwa ni wanamuziki ambao watanashati wanavaa vizuri na kujiweka kwenye maisha ya juu ikiwa ni pamoja na sehemu wanazoishi, Wanamuziki hawa walikuwa wanatoka wote eneo lijulikanalo kama Bandalungwa ama Bandal ambalo ni maarufu kwa maisha ya mjini kama vile Kinondoni ambapo wajanja wote wanaishi huko, ila baadaye yalipowachanganyia wakahamia eneo lijulikanalo kama Socimat kama masaki ambapo watu wenye pesa zao wanaishi.

Mwaka 1997 swali kubwa ilikuwa nani anaweza kuikuza hiyo Spirit ya wana Bandal maana BCBG WENGE walijitambulisha kama familia moja. lakini baada ya kuparanganyika kila mtu kivyake waliwagawa mashabiki pia na kujikuta kila upande unaangukia ama kwa JB Mpiana ama kwa Werasson.

Kwa mujibu wa tafiti hiyo ambayo ilichapwa wiki iliyopita ndani ya mtandao wa Digital Congo Werasson ameonyesha kupendwa zaidi wa masela ambao ni wengi huku JB akisemwa kuwalenga zaidi watu wa Grade B kwenye Show zake. Kiukweli wakurumba hawa wawili wanaendelea kutawala mashabiki wa muziki wa Congo mbali na vijana wengi wanaochipukia kwenye muziki huu na ushindani kati yao ndio umekuwa chachu ya mafanikio ya muziki huu mpaka leo.

Hakuna aliyedhani JB Mpiana na Koffi wangeweza kuja kuwa marafiki walivyosasa urafiki ambao mashabiki wanasema kuwa urafiki wa mashaka na unatokana na Koffi kuhama toka kwa Werrason kwenda kwa JB Mpiana, hilo lilizidi pale Werra alipokataa kwenda kumpa mkono Koffi na kumuangukia ili uhasama kati yao uishe, Werra alikataa hilo mbele ya mashabiki wake takribani elfu 20 ambao walimshangilia sana.

Werrason alifanikiwa kupata Kora Award na baadaye kuchaguliwa kuwa Balozi wa UNICEF na Mjumbe maalumu wa Amani huko Congo nafasi ambayo anaitumikia bado.


JK, Mama Salma wakisalimiana na Bekham

May 17, 2012

https://spotistarehe.files.wordpress.com/2012/05/imag0191.jpg?w=300

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete wakisalimiana na David Bekham ambaye walikutana naye uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London Jumatano, muda mfupi kabla Rais Kikwete na Mama Salma kuelekea Washington DC.

Kikwete alitumia muda huo kumkaribisha Bekham Tanzania kuja kutembelea vivutio vya utalii. Picha kwa hisani ya Blog ya Jamii


R.I.P Mafisango, Utakumbukwa Daima

May 17, 2012

Mchezaji wa Simba Patrick Mafisango amefariki alfajiri hii baada ya kpata ajali ya gari maeneo ya Tazara.

Habari zinasema Mafisango alikuwa na abiria wengine watano wakati mauti yakimkuta, Kwa mujibu wa Patchou Mwamba ambaye alikuwa Mochuari alipoongea na Spoti Starehe anasema kuwa Mafisango alikata roho mara alipopata ajali hiyo ambayo ilitokana na kukwepa Pikipiki.

MAfisango atakumbukwa kwa mchango mkubwa aliotoa kwa timu ya Simba kwa upande wa soka la Tanzania, Hakika Simba imepoteza talanta ambayo bado mchango wake ulikuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa.

Jana Kocha wa Taifa wa Amavubi ametangaza kumuita Mafisango kwenye kikosi cha Timu ya Taifa na ilikuwa anondoke aende kujiunga na wenzake. Mafisango atakumbukwa hasa baada ya kuiteketeza Yanga na hivi majuzi ndiye aliyekosa Penalti pamoja na kipa Kaseja wakati Simba wakicheza na AL AHLY- SHANDY.

Mungu ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu – Amina


%d bloggers like this: