Harusi za Kimalay: Familia inagharamia kila kitu na marafiki hualikwa ila wanakuja na zawadi.

” Wamalay wanasemwa kutumia pesa nyingi sana kwenye kuandaa sherehe ya harusi na kwao utamaduni ni tofauti na kwetu linapokuja suala la maandalizi ambapo shughuli hiyo hufanywa kifamilia zaidi na familia iko tayari kuchukua mkopo kwa ajili ya kufanikisha sherehe hii inayochukua hadi wiki nzima na wakati mwingine wiki mbili.”

wedd

Ama kwa hakika harusi ni kitu ambacho kila mmoja ana ndoto nacho labda iwe kwa matakwa binafsi na ni siku ambayo kila mmoja anapenda iwe ya kipekee kutokana na ukweli kwamba hairudii tena (labda kwa siye Waislamu ambao tunaweza kuoa hadi mara nne).

Ukipata kuhudhuria harusi au ndoa za Kimalay utafurahi kuna kila aina ya mbwembwe ambazo zinaifanya siku hii kuwa ya kipekee kabisa, hii iinatokana na utamaduni wao ambapo kwa kiasi kikubwa sana unarandana na utamaduni mwa kipwani pwani.

Wamalay wanasemwa kutumia pesa nyingi sana kwenye kuandaa sherehe ya harusi na kwao utamaduni ni tofauti na kwetu linapokuja suala la maandalizi ambapo shughuli hiyo hufanywa kifamilia zaidi na familia iko tayari kuchukua mkopo kwa ajili ya kufanikisha sherehe hii inayochukua hadi wiki nzima na wakati mwingine wiki mbili. Kwa kawaida marafiki hualikwa kuja kwenye sherehe.

Unachotakiwa ni kuja na zawadi, Maharusi hupata kila kitu kwani Wamalay harusi za kawaida hualika kati ya watu 600 hadi 2000 ni idadi kubwa sana. ikumbukwe kwa Walay Kula ni sehemu ya utamaduni wao, kama ilivyo kwa Tanzania kila kona kuna Bar Wamalay wao kila kona kuna restaurant na wanakula muda wote hata uamke saa nane usiku hizi resaurant ambazo ni maarufu kwa jina la Mama Shop huwa zinawatu na unaweza kustaajabu kukuta familia nzima wako hapo wanakula, kwani kula nje ni moja ya utamaduni wao mar chache hupika nyumbani.

wansekimah

Rafiki yangu Wan Sekimah Wan Mazlan akiwa na Mumewe mara baada ya kufunga ndoa yao hapo mwaka jana.

kwwa wastani wa mtu wa maisha ya kipato cha kati harusi yake huwa na bajeti isiyopungua Ringit 50,000 ambayo ni sawa na Dola 15,ooo za kimarekani sawa na Mil.2o,ooo za kitanzania.

Mwaka jana mwishoni mwanamuziki maarufu hapa Malaysia Mawi alifunga ndoa na Mpenzi wake wa siku nyingi Ekin, sherehe iliyotamkwa kama harusi ya mwaka 2008, kwa jinsi ilivyoandaliwa na ilivyopamba vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kutangazwa Live kwenye Channel ya Tv ya Astro (Channel Astro Oasis 106) na kutazamwa Asia nzima ambako astro inapatikana (Astro ni kama ilivyo DSTV huku kwetu). Harusi hii inasemwa kugharimu zaidi ya malaysian Ringit 350,000 sawa na USD 100,000. (gonga Hapa kuisoma), Mawi ambaye alikuwa mshindi wa reality show ya Akademi Fantasia 3, ametokea kupendwa sana hasa na akina dada, kwa sasa ni muimbaji na anaongoza kwa mauzo kwenye kila albamu anayotoa.

Mawi na Ekin wakiwa kwenye sherehe ya Harusi yao mwisho wa mwaka jana.

La ajabu ni kuwa pamoja na gharama zote hizi Malaysia oinaorodheshwa kuwa ni nchi yenye kiwango cha juu mno cha Divorce katika asia (kuvunjika kwa ndoa). Wengi wa wanandoa wanaoana katika umri wa miaka 24 kwa wanaume na wanawake kuanzia 20 Umri ambao kimsingi unakuwa hauko tayari kimaisha na kupelekea ndoa nyingi kuvunjika na wengi wa akina dada umri wa kati ya miaka 30 wamejikuta wakiwa hawana waume ama baada ya kuachika au lah.

Hii inapelekea mageuzi makubwa ya kimahusiano kwani kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la akina dada wenye umri mkubwa kuolewa na vijana wadogo (The Star 17 March 2008). Kwa mujibu wa makal hiyo ya gazeti la The Star wanawake wengi wanasema kuwa wanaume wamekuwa waoga wa maisha ambapo kwa mujibu wa mila na desturi za Kimalay Mwanaume anategemewa kwenye nyumba kwa kila kitu na wengi wa wanaume wa Kimalay hawaruhusu wake zao kufanya kazi.

Pamoja na hayo yote bado harusi za kimalay znabaki kuwa na kumbukumbu kubwa kichwani mwangu kati ya sherehe za aina hii kwa tamaduni nyingine nilizopata kuona.

8 Responses to Harusi za Kimalay: Familia inagharamia kila kitu na marafiki hualikwa ila wanakuja na zawadi.

 1. Gerry says:

  Wow so nice i love the dressing code

 2. Asnath says:

  Kaka Pius i love the dressing unaweza kuniulizia bei?

 3. Anonymous says:

  Duh mihela yote hiyo si bora wangefanya jambo la maana hawa jamaa?

  • Drinkedin says:

   I really like your writing style and how well you express your thoughts. You has interesting and solid content. I am trying to discover more about this issue.

 4. benny wissa says:

  Ina pendeza! Ila hakuna asiye penda, kufanya mambo ya juu uchumi ndiyo unao tukaba tufanye kazi kwa bidii inshalah mungu ata tusaidia 2tafikia hayo matawi

 5. Anonymous says:

  So nice i love the dressing also
  Niangalizie Bro how much ningependa kuvaa hiyo kwenye wedding yangu am serious nipe email yako nikuandikie.
  L.K
  DSM

 6. Fairly particular he’ll have a great go through. Thank you for sharing!

 7. I want you to thank for your time of this wonderful read through!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: