Ninelle mwana sassou: Wimbo Koffi alomtungia mtoto wa Rais Sassou Nguesso

May 7, 2012

Na Hadji Le JBneeque

Ninelle mwana Sassou,wimbo ambao Koffi Olomide ameuliutunga maalum kwa aajili ya binti wa rais wa Congo Brazaville mzee Denis Sassou Nguesso,ni wimbo fulani wa taratibu wenye ujumbe mzito wa kimapenzi ndani yake.

Familia ya rais Sassou Nguesso akiwemo mzee mwenyewe pamoja na mkewe mama Antoinnete “Antou” Sassou la premiere dame du Congo licho ya kuwa wanatoka  upande wa pili wa Congo Kinshasa yani Congo Brazzaville ni wadau wakubwa sana wa muziki na wanamuziki wa Congo Kinshasa kiasi cha kwamba ni aghalabu (kawaida) sana kwa wanamuziki toka Congo hiyo ya Joseph Kabila kualikwa kwenye sherehe za kiserikali na binafsi za familia ya rais Nguesso.

Huyu mzee ana watoto wengi sana na wengi wao wamekuwa wakitungiwa nyimbo na kuimbwa na wanamuziki karibu wote wakubwa wa congo.miongoni mwa watoto hao wa rais ni mamaa Edith-Lucie Sassou Nguesso ambae kwa sasa ni marehemu,ambae pia alijulikana kama Edita Omari Bongo a.k.a.

Edita mwasi ya mokonzi kutokana na kuolewa na rais wa Gabon marehemu Rais Omari Bongo,pia baadhi ya watoto wengine wa mzee Denis Sassou Nguesso ni Claudia Sassou ambae ametungiwa wimbo uitwao Etoile Du Berger na Jb Mpiana unaopatika kwenye album ya sayons serieux,pia yupo  Blandine Sassou Nguesso,kiki nguesso wa kiume ambae inahisiwa anaandaliwa na babake kumrithi kwenye urais na watoto wengine wengi list ndefu


TANZIA NA SHUKRANI: MAREHEMU RAYMOND MADINDA MANG’ATI

May 7, 2012

 

madinda

Familia ya Bibi Nkinde Mwakitalu (Mrs. Nkinde Raymond Mang’ati) wa Makumbusho, Dar Es Salaam, inatoa shukrani za dhati kwa Ndugu , Jamaa na Marafiki

Kwa kushiriki kwenu kwa hali na mali wakati wa Msiba wa Mpenzi marehemu Raymond Leornald Madinda Mang’ati aliyetwaliwa na Bwana tarehe 23 April 2012 na kuzikwa tarehe 26 April 2012 Kiondoni, Dar Es Saaam.

Hatuna maneno ya kutosha kuelezea ila tunaomba mpkee shukrani zetu kama sehemu ya kutambua mchango wenu na moyo wa upendo mliotuonyesha wakati wa kipindi chote cha Msiba na hatimaye kumsindikiza mpenzi wetu Marehemu Raymond Leonard Madinda Mang’ati katika safari yake ya mwisho.

MWENYEZI UNGU AWABARIKI SANA.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIDIWE

“MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU RAYMOND LEONALD MADINDA MANG’ATI MAHALA PEMA PEPONI AMEN.

image


Chezea Twanga wewe…!!

May 7, 2012

Mshindi wa BSS Haji Ramadhani na Mshindi wa Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis! Twanga Pepeta Bendi ya Washindi!


Sandra, Mcheza Show wa JB Mpiana aliyeponzwa na Didie “Stone” Kinuani

May 7, 2012

Anaitwa Sandra Lina, huyu aliwahi kuwa Mcheza Show wa JB Mpiana na alifukuzwa kwenye bendi baada ya kubainika kuwa alipokea pesa (alisaidiwa) na Didi Kinuani jambo ambalo lilimkasirisha sana JB Mpiana.

Baada ya kufukuzwa Sandra ambaye alikuwa na urafiki mkubwa sana na Bibiciya Mfwengi ambaye kwa wakati huo alikuwa ni kiongozi wa madancer wa Wenge Musica Maison Mere baada ya kubwaga manyanga akitokea kwa Koffi Olomide, (lakini kwa sasa Koffi amefanikiwa kumrejesha tena kwake). Bibiciya alimuombea Sandra ili ajiunge na WMMM lakini mwanamuziki mwingine na muandamizi wa Wenge BCBG Seguin Mignon alimpigia simu Werason na kumtahadharisha kuhusu sakata hilo na mpango mzima ukafa.

image

Sandra ambaye ni yatima alihangaika na wakati fulani alikimbilia Ivory Coast na kujiunga na bendi moja ya huko hatimaye ameibukia kwenye uimbaji na kutoka na kibao hiki ambacho aliki dedicate kwa Didi Kinuani.

Sandra amesaidiwa kwa kiasi kikubwa sana na Didi Kinuani ambaye pia ilisemekana  aliwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Mkorogano wa JB Mpiana na Didi Kinuani ulijitokeza pale tajiri huyo ambaye ni mshirika mkubwa wa Presidaa Kabila kuamua kumchukua mke wa JB Mpiana na kufunga naye ndoa, jambo ambalo hata wanamuziki wenzie na wapenda burudani pia hawakulifurahia.  Werason kiongozi wa WMMM binafsi alikataa kwenda kutumbuiza kwenye harusi hiyo licha ya donge kubwa alilotengewa kwa madai kuwa yeye alikuwa mshenga wakati JB Mpiana akienda kumchumbia mwanamke huyo, na kuongeza kuwa tofauti zao ni katika burudani tuu na si kimaisha.

Pata kibao chake Sandra.


%d bloggers like this: