Werason aelezea chanzo cha ajali….!!

May 3, 2012

Kwenye Video hii Werasson anaelezea chanzo cha ajali yake ajali ambayo aliipata mwezi Novemba 2011 na kuvunjika mkono kisha akakimbizwa nchini India kupata matibabu.

Nimejaribu kusikiliza walao nitaambulia kitu lakini nachanganywa nitajitahidi kuleta mtohoo wa kinachoongelewa mwanzo mwisho.

Ikumbukwe kuwa kiongozi wa Wenge BCBG JB Mpiana na Adolph Domibguez walikuwa kati ya watu wa kwanza kwenda kumfariji, habari zinasema JB Mpiana alikuwa wa kwanza kufika na alikwenda hospitali huku akibubujikwa na machozi kwani aliyempa taarifa alimwambia Werasson amefariki, “…Kwanza tulishangaa JB alipataje taarifa mapema vile… na alipofika alikuwa akitokwa machozi kwani aliyempatia taarifa alimueleza kuwa Werrason amefariki dunia” alisema Yanki Mpuyi ambaye alikuwepo wakati wa ajali.

Kisha waliwaacha wao wawili tu (JB na Werrason) humo chumbani hospitali kwa zaidi ya nusu saa wakiongea na kisha JB alitoka nje huku bado akibubujikwa machozi aliendelea kueleza Yanki na Heritier pamoja na Kakol ambao walikuwepo Hospitali muda wote, kisha waliingia Frere Patrice pamoja na mama yake mzazi ambaye alikuwa amehamaki na kumbusu mwanaye aliyekuwa akigugumia kwa maumivu makali.

Inasemekana kuwa mashabiki walifurika hospitalini na katishia kuichoma hospitali kama kipenzi chao atafariki ndipo Local Authority walipokaa na kuamua kuwa Werrason apelekwe nje ili kulinda usalama kwani ni kipindi cha uchaguzi hivyo mashabiki wangeweza kutumia nafasi hiyo kuleta fujo.


%d bloggers like this: