Wenge ya zamani on stage…

Hawa walikua watu wa kazi mwanzo mwisho,kila mtu aliijua kazi yake,waimbaji waliimba,wapigaji walipiga na kucheza pia,yani jukwaa zima ni full shangwe mwanzo mwisho,nani kama hawa???bila shaka hakuna na wala haitotokea kama hawa,tutaendelea kuzikumbuka kazi zao tu kama hivi sawa na mtu mliekuwa nae duniani then akawatoka na hawezi kurudi tena…..!

We miss u guyz…please do us a favour walau ka album kamoja tu ka pamoja basi!

Wadau wasomaji ombi maalum kwenu naomba mumtizame ALAIN PRINCE MAKABA kuanzia dakika 05:35 na mpaka mwisho then mumpe heshima yake kidogo, mi naanza kwa kusema Alain Makaba “SHIKAMOO”

11 Responses to Wenge ya zamani on stage…

 1. mamaa prezident mwasi ya mokonzi says:

  it sounds cul…

 2. Anonymous says:

  Alain makaba alikua juu sana,alikua ananifurahisha sana na style yake ya kuchezesha chake kwa style ya aina yake na kwa hisia kali wakati anapiga gitaa lake

 3. Anonymous says:

  hivi huyo mfupi aliyevaa suruari ya blue kama ya draft na kizibao cheusi anaitwa nani na yuko wapi siku hizi labda?

  mchangamfu sana stejini

 4. Anonymous says:

  sorry sio na kizibao amevaa na koti jeusi na miwani kaiweka kichwani

 5. Stivin says:

  Huyo anaitwa Manda Shante, aliondoka baada ya albamu ya kalayi boeing kwa kukwaruzana na Mpiana! ndo akaletwa Aimelia kujaribu kuziba Pengo lake

 6. Joachim says:

  Tuache utani. Wenge walikuja juu kati ya mwaka 1989 baada ya bendi nyingi za Congo kusambaratika. Ila wazee wa kazi of all times ni Zaiko Langa Langa. Hakuna mcongo anayebisha hili. Zaiko ndiyo waliotuletea hizi sebene za Wenge mpaka tukaja kuwajua kina Bozi, Papa Wemba, Evoloko, Manuaku, Defao, Emeneya, Zipompa Pompa, Awilo, na wanamuziki kibao ambao wote kwa namna moja ama nyingine ni matunda ya Zaiko. Thanks to Papa Nyosh (Nyoka Longo) and his abilities kuona mbali mpaka akaja kutupa masebene ya nguvu. I would say, after zaiko then Wenge ile ya zamani si hizi za siku hizi za mabanga.

  • Anonymous says:

   well said joachim,sasa hivi hakuna ki2,wanamuziki wamekua mateka wa mabanga kina claudia sassou nguesso,tabou fatu,zadio kongolo,Alexii kayembe “shentembaa,joseph kabila,didi kinuani,joseph kusaga na wengine wengi wenye pesa wanaopendwa kutungiwa nyimbo na kuimbwa ama kutajwa,hawa jamaa ndio wanolipia pesa ya studio kwa ajili ya kurekodi na pia wanawalipa watunzi wa nyimbo kwa nyimbo husika,mimi nawaona kama wanachangangia kuharibu ladha ya muziki wa congo……..

 7. Hadj Le Jbnique says:

  Joachim naomba uitizame hii video hapo chini ambapo wenge na zaiko baada ya ubishani mkubwa sana wa wapenzi wa bendi hizo mbili kwamba nani zaidi huku wengine wakidai wenge imekuja kumaliza ubabebwa zaiko ndani ya kinshasa,kuliandaliwa onesho hili la pamoja kati ya vijana wenge,na wazee wao zaiko,huu ni wimbi AZIZA wa zaiko ambapo hapa unaimbwa kwa pamoja na wenge na zaiko wenyewe,lakini kilichovutia siku hiyo ulikua ni mpambano wa marepa wawili wa bendi hizo ambao waliwaumiza vichwa wapenzi wa muziki eanzi hizo kujua nani zaidi,hapa nawazungumzia Le Grand Chibuta Roberto Ekokota wa wenge na Atalaku Mombele wa Zaiko,kwa mtazamo wako wewe baada ya kuitazama hii video,nani alikua juu kati ya Ekokota na Mombele???but binafsi namheshimu sana papa Nyoshi…

 8. I’m still learning from you, as I’m trying to achieve my goals. I certainly enjoy reading all that is written on your website.Keep the stories coming. I loved it!

 9. Aliza Mews says:

  I think this is often an informative submit and it truly is experienced and incredibly handy. I’d like to thank you for the efforts you might have manufactured in writing this post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: