Koffi apata ruhusa kuimba nyimbo za Franco

image

Baada ya Concert yake iliyofana ya Koffi chante Tabu Ley na Koffi chante Lutumba mwanamuziki nguli Koffi Olomide ameomba ruhusa kwa watoto na familia ya marehemu Franko Luambo Luanzo Makiadi ili aweze kupiga Concert na huku akiimba nyimbo za mwanamuziki huyo mahiri aliyetamba na bendi ya T.P Ok Jazz

Koffi amesema kuwa kutokana na Matukio yaliyojiri kwa wanamuziki wa Congo waliokuwa wakim support Rais Kabila huko Europe ameamua kuongeza show zake nchini Congo na anataka awaridhishe mashabiki wake kwa kuwapa ladha na kile kitu roho inapenda.

Akiongea na Digital Congo Koffi amesema kuwa anajiimarisha kwenye ziara za Africa zaidi kwa mwaka huu ambapo amepanga kufanya maonyesho kadhaa.

Kwa mujibu wa habari ambazo zimetolewa na Koffi mwenyewe anasema kuwa amepanga onyesho hilo la kumuenzi Luambo limepangwa kufanyika July 7, 2012, kwenye bwawa la kuogelea la Hoteli maarufu ya The Grand huko Kinshasa.

Koffi amesema kuwa mazungumzo yameshafanywa ya awali na tayari familia ya marehemu iliwakilishwa na Emongo ambaye anasema kuwa alimuandikia yeye binafsi na kumuomba aziimbe hizo nyimbo za marehemu baba yao na mazungumzo yakaanzia hapo.

Haikuwa jitihada zangu bali ni wanafamilia ya Mareemu hasa baada ya kuona picha na video za show ya Simaro Lutumba na Tabu Ley.

“Nisingeweza kukataa nafasi hiyo adhimu ya kuiimba sauti ya yule mzee kwakweli hata ungekuwa wewe ndio mwenye kipaji kama changu usingekataa aliongeza Koffi”.

Nakuwekea kibao Mamou chake kilichoimbwa na TP Ok Jazz.

 

Advertisements

4 Responses to Koffi apata ruhusa kuimba nyimbo za Franco

  1. Hadj Le Jbnique says:

    Ni kweli kabisa na kwa kuongezea tu hapo ni kwamba kuonyesha kwamba Le Rambow Du Zaire Quadra Kora Man Papaa na Sean James,Papaa na Delpiro na pia Papaa na Didistone ni kwamba tayari ameshaanza kuzifanyia mazoezi nyimbo za mzee Franco akiwa na wanamuziki wake na pia ameshawasiliana na baadhi ya members wa TP OK JAZZ walio hai ili washiriki pia kwenye concert hiyo,Lakini pia ameendelea kugonga VIP concerts zake kama kawa ndani ya KIN ambapo kuna moja hivi karibuni imevunja rekodi kwa kuacha nje ya ukumbi watu mara tatu ya walio ndani kutokana na kukosa tiketi zilizokwisha kabla hawajafanikiwa kuzipata huku bei ya tiketi ikiwa dola 100 very expensive,kiufupi Abracadabra is now on top in KIN

  2. nziki wa franco unapendwa na wengi na utaenflea kupbndwa

  3. Anonymous says:

    Picha Ya Koff

  4. Elenor Birt says:

    Quite great blog and excellent and content articles.valuable layout, as share good things with very good concepts and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: