KITABU CHA HISTORIA(BIOGRAPHY) YA WERRASON CHATOKA!

Na Hadji Le JBeeneque

Nadhani Werrason ni mmoja wa wanamuziki wa Congo wenye washabiki wengi sana hapa nchini na Africa kama sio duniani kiujumla. Lakini kwa muda mrefu mashabiki na wapenzi wake hao wamekua wakimfahamu Le Roi De La Forret Papaa na Exocee Mobali ya Mama Pastor Sylvie Mampata kijuu juu tu. Lakini safari hii mashabiki wake na wa muziki kiujumla hususan wanafamilia wa wenge wamepewa fursa maalum ya kumjua nguli huyu wa muziki wa congo kupitia kitabu maalau ambacho kimeshachapishwa kikielezea historia ya mwanamuziki huyo binafsi na katika harakati zake za kujiingiza kwenye muziki, kuwa star na mpaka sasa kumiliki bendi kubwa na yenye mafanikio makubwa pia.

Dondoo za yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kwamba ndani ya kitabu hicho werrason anaelezea kwa mfano wenge musica ilivyozaliwa. Katika hilo Werrason anasema mwanzoni kabisa walikua yeye Werra, Aime Buanga, Jean Belix Luvutula, Didier Masela na Christian Zitu, ambapo Aime Buanga alichukuliwa kama muanzilishi wa kundi kutoka na yeye kujitolea nyumba ya wazazi wake alimokua akiishi itumike kama sehemu ya kufanyia mazoezi ya kundi lao hilo na pia Didier Masela nae kwa upande mwingine akichuliwa kama muanzilishi pia kutokana na kwamba wazo la kuanzisha bendi lilitoka kwake.Lakini wakati fulani kwenye siku hizo hizo za mwanzo mwanzo za kundi lao Aime Buanga alitaka kuachana na kundi hilo changa ili aendeleze kipaji chake kwenye sanaa za mapigano (martial arts) huku akimpa masharti rafiki yake werrason kwamba kama unataka nirudi kundini na wewe jiunge na mimi kwenye sanaa za mapigano (martial arts) sharti ambalo kwenye kitabu hiki werra anadai alilitekeleza kwa kujumuika na swahiba wake kwenye martial arts.

Wakati ya Werrason na Aime Buanga yakiendelea hivyo kwa upande mwingine Didier Masela alikua shule nje ya Kinshasa katika mji mdogo uitwao Mbanza Boma pamoja na Alain Makaba.Baadae huku nyuma Jb Mpiana akafika kuja kujiunga na bendi ambapo werra anasema katika kitabu hiki akamueleza “rafiki yangu nimesikia wewe ni muimbaji mzuri sana kama hitajali naomba uniimbie wimbo kidogo nikusikie na mimi” baada ya kauli hiyo ya werra jb inaelezwa akaimba wimbo uitwao “Abidjan” wa Viva la Musica uliotungwa na Debaba,ambapo Werrason mwenyewe na kila aliekuwepo pale wakavutiwa nae sana kiasi cha kumpigia makofi kwa wingi na watu wote, baada ya hapo werra akapendekeza Jb ajiunge na bendi ambapo Jb alikubali bila kusita.

Siku hiyo miongoni mwa waliomshuhudia Jb akiimba pamoja na werrason ni Didier Masela na Jean Belix.Na aliyemleta na kumtambulisha Jb hapo kundini alikua ni Jean Belix Luvutula ambae walikua wakiishi jirani na alikua akimuona Jb akiimba mtaani.

Baadae Blaize Bula akaletwa na Makaba kujiunga na bendi kama mpiga drums kutokana na kwamba alikua mpiga drum wa bendi ya shule waliyokuwa wakisoma lengo likiwa aje achukue nafasi ya binamu yake werrason  aliyekwenda kwa jina la Ladins Montana ambae ndio alikua mpiga drums, lakini Sele Bula akaonekana hana muonekano wa bcbg lakini Makaba kwa kujua kipaji cha Sele kwenye uimbaji pia akasisitiza aingizwe kundini. Hivyo wakawa wamempata Blaize(sele)Bula kama muimbaji,na kwa upande mwingine Jb ambae alikua tayari kundini alikutana na Tata Mobitch Adolphe Dominguez ambae alikua ni mtoto wa tajiri mkubwa sana Congo lakini pia akiwa na dancer mzuri akicheza sana nyimbo za DEFAO.

Jb na Adolphe baada ya kujuana kutokana na Jb kuvutiwa na uvaaji wa Adolphe wakatokea kuwa marafiki wakubwa huku Adolphe akimpigisha Jb pamba za ukweli kiasi cha kung’aa mbaya miongoni mwa wanabendi,ndipo baadae Jb akamtambulisha Adolphe kwa Werrason na wengine kundini ambapo wakaanza kumfundisha muziki Adolphe hapo hapo kundini huku yeye akilipa fadhila kwa kuwafadhili upande wa mavazi kupitia utajiri wa babake!

Kitabu kimeongelea mambo mengi hatuwei maliza ngoja nitoe dondoo za alichozungumzia werra kuhu su maisha yake binafsi.Katika maisha yake binafsi werra anasema alikutana na mkewe kipenzi Mama Pastor Silvie Mampata akiwa shule kupitia rafiki yake kipenzi wakati huo aitwae Wasenga Kipuni.Sylvie alikua ni binti wa mfanyabiashara tajiri na aliutumia utajiri wa babake kuisadia sana wenge huyu mama kupitia kwa werrason.

Kuhusu mgawanyiko kitabu kinaeleza kwamba ni uamuzi wa Jb kurekodi “Feux de l’amour” kwa kuwashirikisha wanamuziki wengine toka nje ya wenge kama alivyofanya Alain Makaba kwanza kwenye album yake solo iitwayo “Pile ou face” hapo ndipo mgogoro wa kiuongozi ulipoanza kuibuka,ambapo baada ya mafanikio ya Feux de l’amour Jb kwa kushirikiana na SIMON SIPE ambae ndie alikua meneja wao akisimamia kila kitu mpaka production zao wakanogewa na kutaka kutoa album nyingine solo ya pili ya Jb,hapo ndipo werra alipokasirika na kuitangaza album yake Kibuisa mpipa huku akiwa hana hata nyimbo moja wakati huo akiitangaza ila tu alitaka kumuonyesha Jb kwamba hawezi kutoa album solo ya pili wakimtazama tu.

Baada ya hapo bendi ikagawanyika na werra  ili kushindana na Jb akawa na mawazo ya kuanzisha tu bendi haraka haraka na kuanza kuperfom matokeo yake akachemsha sana mwanzoni kwenye concerts zake za awali zikawa “flop” mpaka ndugu zake wanaotoka kijiji kimoja kina Marie Paul wakamuonea huruma na kuamua kumsaidia ambapo Marie alimpa bure mwanamuziki wake JDT na yeye mwenyewe akawapata watu kama Didier Lacoste,Adjan n.k. ndipo mambo yakaanza kwenda vizuri sasa na kutoa FORCE INTERVENTION RAPIDE.

Ambapo badae mwandishi wa kitabu hiki nae alimpa wazo werra la kutarget zaidi concerts za watu wa kawaida kuliko za VIP kama wafanyavyo Bcbg,pia werra akapata msaada mkubwa toka kwa mamaa Tshala muana,baadae wakapata kazi ya kwanza ulaya kwa kualikwa kwenda kupiga London ambapo muandishi wa kitabu hiki alifanya kazi ya ziada kwa ku organize umati wa watu kwenda kumpokea werra na bendi yake airport katika safari ambayo masela aliachwa kin na ikawa mwisho wako kundini.

13 Responses to KITABU CHA HISTORIA(BIOGRAPHY) YA WERRASON CHATOKA!

 1. Stivin says:

  Asante sana Haji! nimefurahi kuisoma historia hiyo! Nadhani Werra na Wivu na choyo Wenge isingefika hapo ilipo! Ila Mpiana nae ana ubinafsi, kwa nini alitaka kutoa albamu ya pili? Ndio maana Mungu amemlaani akashindwa kufikia mafanikio ya Feux D amor mpaka sasa.

 2. ozaaa likolooo Patron Pius merci mingi

 3. Anonymous says:

  Sports starehe never boring lol…stori kama hii huwezi kuipata popote pale si kwenye radio wala tv stations hapa hata papaa zuberi msabaha amabe ndio tunamuamini kwa info cha mtoto,hivi hawa watangazaji wa vipindi vya bolingo wanaitembeleaga hii blog kweli?ningekuwa mimi wao hapa ndio pangekua sitting room pangu

 4. wenge kumbela says:

  ahaaa kumbe werrason ndie aliyemuinterview jb eeeh?bila werra hakuna jb mpiana leo ndio nimelifahamu hilo,jb kiburi cha bure tu,shwain…!

 5. Richard rich stivin says:

  Muandishi wa hii kitu naomba namba yako mzee wangu,unaonekana unaifahamu sana wenge na hawa kina werrason na jb mpiana kuliko mtu yeyote humu na mimi ni fan no.1 wa wenge original na sasa nimeegemea zaidi maison mere,pia ni mtangazaji wa redio moja hapa nchini,kuna mambo natka unisaidie ndugu yangu.nilisoma pia ulivoandika mwaka jana hapa hapa ile historia ya wenge mpaka kuvunjika na jinsi bcbg na maison mere zilivoanza kwa kweli lilikua somo ambalo sikuwahi lipata popote

  asante sana

 6. Richard rich stivin says:

  SAWA KAKA NIWIE RADHI BASI MIMI NITAKUWA NAMBA 2

 7. Anonymous says:

  mimi ni mkongomani naishi province la maniema ville kindu quartier 3Z nimejuwa kwakirefu tena wanamziki wa congo.

 8. jacob maskas says:

  Nimeshukuru kwa kusoma historia hii na kujuwa ukweli zaidi ya kundi la bcbg musica .naweza kusema kwamba jb mpiana ni mwanaume mwenye busara kwa kuhisababisha kundi hili litengane ili kila mtu ajitegemee !

 9. PETER says:

  MIMI NATAKUJUA WERRA ANAUTAJIRIWAKIASI GANI

 10. Attractive component of content. I simply stumbled upon your blog and in ccession capital to say that I acquire actually enjoyed account your blog posts.
  Anyway I will be subscribing on your feeds and even I achievement you
  get entry too consistently rapidly.

 11. Mia Trennell says:

  I believe this really is an informative post and it is experienced and incredibly helpful. I would want to thank you for your efforts you’ve produced in writing this article.

 12. Iwanowski says:

  I will be commenting in order to show you such a wonderful experience my personal child relished examining your own web page. Your lover seen a wide variety of bits, while using the introduction associated with what it’s just like on an awesome helping type to achieve the relax without having inconvenience grasp a few difficult is important.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: