Kanumba alitabiri kifo chake kwa Wimbo kama Bavon Marie.

Bado tuko kwenye Siku 40 za maombolezo ya kipenzi cha watanzania Steven Kanumba, Majuzi nilisikiliza TBC Radio nikamsikia Thimanga Kalala Asosa akiongelea jinsi Kanumba alivyotabiri kifo chake na kumfananisha na mwanamuziki aliyewika na kupendwa sana huko Congo miaka hiyo aliyejulikana kama Bavon Marie.

Wimbo huu ulitungwa na bwana Bavon Marie –Marie kama kutabiri kifo chake, nakuletea huo Wimbo baada ya kumsikia Papa Tshimanga Kalala Asossa katika kipindi cha TBC Radio akifananisha tukio la Marehemu Steven Charles Kanumba na kifo cha Bavon Kwa wingi wa watu waliohudhuria mazishi ambayo watu Wengi walikosa fursa ya kumuaga na tofauti ni hali ya hewa Bavon Kulikua na mawingu mazito Kule Kinshasa lakini Dar kulikuwa jua kali. Kwa waliofatilia mahojiano yale na kuombaniutafute wimbo huu nimeupata na shukrani za kipekee kwako Le Fimitive Didie Kinuani ya Tunduma Thabit Mwambungu kwa ukokotoo huu.

MASEKE YA MEME- PEMBE ZA KONDOO

BAVON MARIE MARIE

NEGRO- SUCCESS

Famille oyo motema mabe bondoki ekoma mosala,

Mwana moke lokola ngai bakundeli ngai maseke ya meme liboso ya lopango o batii ngai motema motomoto mpo nabala Te,

Familia hii ina roho mbaya uchawi umekua kazi,

Mvulana Kama Mimi wamenizikia pembe za kondoo mbele ya nyumba wamenitia hofu nisiolewe,

Kanda ya nini o bandeko mpo baliaka mbongo na ngaite balongola ngai motema e batia ngai motema ya soso mpo nakoma lokoso nasilisa mibali e ndoki mpe akufaka e nkisi mpe epolaka,

Hasira ya nini ndugu zangu sababu hawatumii pesa yangu wamenitoa roho wameniweka roho ya kuku ili niwe na tamaa nimalize wanaume mchawi huwa anakufa dawa nayo inaoza,

Malamu koboma ngai nakufa e nalembi ngai mwana moto.

Bora/vizuri mniue nife nimechoka Mimi mtoto wa mtu.

Bomengo nini na ngai o nazali na mbongo te o tokowela nini?

Utajiri gani nilionao sina pesa tunagombea nini?

Bondoki eloko mabe o banganga mpe bakufaka e Mokili oyo ya batu

Uchawi kitu kibaya waganga pia hufa dunia hii ya watu

Nalela na vie na ngai o nalembi Mokili te o balingi ngai nakufa e

Nalia maisha yangu sijaichoka Dunia kuishi wanataka nife

Naloba lisusu te o nazela kaka liwa ee

Sitasema tena nangojea mpaka kifo.

Advertisements

5 Responses to Kanumba alitabiri kifo chake kwa Wimbo kama Bavon Marie.

 1. Hadj Le Jbnique says:

  Bavon alikua ndugu yake Franco luambo luanzo makiadi na hata kifo chake kilihusisha na imani za kishirikina huku FRANCO akinyooshewa vidole kwa kifo iko kilichotakana na ajali ya barabarani kama sikosei,na huu wimbo pia ilisemekana bavon alikua anamgonga mzee FRANCO kimafumbo ambae ilisemekana alikua akimonea wivu mdogo wake huyo na kumuona kama tishio kwake,all in all mungu aziweke pahala panopofaa roho za marehemu wote hawa watatu,Franco,Bavon na Kanumba pia ambae nae alimpenda franco na muziki wa congo kiujumla

 2. Tony says:

  Kwel dunia ina mengi kila mtu na la kwake anachojisikia kuongea!

 3. Anonymous says:

  This has been my favoret song since I was a school boy.

 4. hermosa pr says:

  I bet this is probably a simple issue for you. I could not refrain from commenting. Do you have any video of that?

 5. Currently it seems like Expression Engine is the best blogging platform available right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: