JB Mpiana na BCBG waihama Crystal Club

Mashabiki wanadai kamkimbia Werasson.

 [http://www.congobilili.com/5385#]

Baada ya kuwa wakipiga shows zao kila jumapili katika kiota cha maraha cha CRYSTAL CLUB  ndani ya KIN kwa takriban miaka miwili,hatimae bendi wa wenge bcbg chini yake Salvatora De La Patria Papaa na Daida Mobali ya Amida Shatur JB MPIANA imeuhama ukumbi huo na sasa itakua ikitumbuiza katika ukumbi wa VENUS HOTEL(Ambiance),hivyo kwa mtakaotembelea Kinshasa kuanzia sasa basi msisumbuke tene kwenda CLUB CRYSTAL siku ya jumapili,kwa sasa mambo yote ya concerts za bcbg za kila jumapili yapo VENUS

Hii hapo juu  ni sehemu ya video iliyopigwa kwa simu ya mkononi siku ya kwanza bcbg kutumbuiza kwenye hicho kiwanja chao kipya kwa kila siku ya jumapili,show hii ilihudhuriwa na mastaa kibao katika tasnia ya muziki wa congo akiwemo Bill Clinton,baby ndombe,alain mpela na baadhi ya wanamuziki kutoka katika bendi ya Fally Ipupa

Hivi karibuni ilitangazwa kuwa Werrason na kundi zima Wenge Musica Maison Merre nao wameanza kupiga ukumbi jirani na hapo Crystal Club.

Kitendo cha mahasimu wawili kupiga kwenye eneo moja kinafanya wote kuwa na wakati mgumu kwani kila mmoja anatakiwa awaelimishe hasa mashabiki wao kuvumiliana na si kuleteana fujo kutokana na kuwa na ukweli kwamba mashabiki wa Werra na JB ni kama Simba na Yanga.

Werrason ametangaza kuachia Single yake inayojulikana kama « Honorable député ».

Kwa upande wake Werrason alitangaza ukumbi wa La salle Carlos ulioko Kinshasa kuwa ndio utakuwa ukumbi wake wa kujidai na kila jumapili atakuwa akipiga kwenye ukumbi huu ulioko complex Mwana Nteba

Mashabiki wa Wenge BCBG walikuwa wameshazoea kupata burudani kila jumapili kutoka kwa kipenzi chao JB Mpiana na bendi nzima ambapo wanafanya sho zao kila jumapili katika ukumbi wa “The Crystal Club” ambayo iko barabara ya 30Juin ambayo ni eneo moja na ambako Werrason atakuwa anapiga.

Inasemekana JB Mpiana amenunua ardhi jirani na hapo na ameanza ujenzi ambapo inasemekana anajenga studio pamoja na ukumbi wa kufanyia mazoezi na pia club. habari zinasema kuwa ujenzi umeshaanza kwa hiyo mashabiki watakuwa wameongezewa burudani zaidi.

3 Responses to JB Mpiana na BCBG waihama Crystal Club

  1. Hussein Ameir Mwanaporto says:

    kwa kweli JB Mpiana Bin Adam au Papaa Chituka yeroo ni zaidi ya jabali katika D.R.C na kama watajaribu japo mara moja tu kukaa kama WENGE MUSICA BCBG Ile tuijuayo ya kina Blaise Bula Engeneur,Adolf Dominguez Elongo,Alain Mpela Afande,Werrason Ngiama,Didier Masela,Ficare Muamba,Ekoko ekokota n Roberto Wunda bila kumsahahu Tutu Kaludgi na Alain Prince Makaba,Emeliya lyase pamoja na mkaanga chips maridadi Titina Alcapone.Wapige moja tu album halafu wasambae tena basi nna uhakika itavunja record ya mauzo Duniani kama sio africa.

  2. Anonymous says:

    KWELI KABISA MUKULU HAKUNAGA NA WALA HAITOTOKEA BENDI KAMA WENGE ILE KAMILI,ZILE NYIMBO MPAKA LEO ZIKIPIGWA MTU UNAENJOY

  3. Right here is some really useful info. I really like your writing style. Thanks for sharing your thoughts. There are certainly a lot of details to take into consideration.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: