Salamu za Rambirambi za Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa watanzania kupitia Twitter na Facebook.

image
Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya filamu nchini hautasahaulika.
Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii. Tutaendelea kumkumbuka kwa mchango wake huo kwa nchi yetu. Namwomba Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu wadau wote wa tasnia ya filamu nchini za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake. Aidha, naungana na wanafamilia na wasanii wote kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.

2 Responses to Salamu za Rambirambi za Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa watanzania kupitia Twitter na Facebook.

  1. Anonymous says:

    DA IMETISHA KIFO CHA KANUMBA

  2. Anonymous says:

    DU 2LIMPENDA SANA KANUMBA,HAKUNA MSANII KM KANUMBAJ

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: