Mortel Combat toka kwa Mpela Brothers

Wanaitwa Mpela Brothers wakiwa ni makaka wawili Allain Mpela na Geco Bouro Mpela, Hawa vijana wote ni matunda ya makundi mawili makubwa ambapo Allain Mpela alikuwa na kundi la Wenge Musica BCBG chini ya nguli JB Mpiana huku Geco Bouro Mpela ye akiwa anatokea kundi cha Koffi Charls Olomide.

Alain Mpela aling’aa sana alipokuwa na Wenge Musica BCBG hasa kwenye albamu yao ya Titanic ambapo aliimba sana na beti zake kuvutia wengi nyimbo kama Liberation, Serge Palmi na nyinginezo. wakati Geco Mpela yeye aling’ara zaidi kwenye Ultimatum ya Koffi Olomide.

Allain Mpela aliamua kutoka solo na mpaka sasa ana Album moja sokoni inaitwa INTIFADA huku Geco Mpela naye alitoka kivyake na album yake inaitwa ICE DE PROCEDURE, lakini wawili hao huwa wanafanya show ya pamoja na walitoa album moja wote wawili ikiitwa Mortel Combat ambayo ilitengenezwa na Professionally Solorist Allain Prince Makaba huko Bruxells Belgium.

Kwa kumbukumbu tu Mpela na Mpiana hawakukutana barabarani na kuwa pamoja BCBG,Wametoka mbali toka wenge musica 4*4 the best of the world,mpela aliletwa hapo wenge na JB MPIANA,naweza sema alikua ni kijana mwenye bahati ya kupata nafasi ya kufanya kazi na watu wa kazi yeye akiwa bado mdogo,nakumbuka ni yeye na LE GRAND CHIBUTA ROBERTO OKOKOTA ndio walikua wadogo zaidi,ndio maana Alain Mpela licha ya kuondoka BCBG lakini bado amekuwa royal kwa mwalimu wake tofauti na watu kama FERRE GOLA na DE CAPRIO DE KINSHASA FALLY wanavyowatoa jasho walimu wao wakiweweseka usiku kucha namna ya kuwazima vijana wao kimuziki.

Iliwahi kutamkwa kuwa Allain Mpella alikuwa tayari kurejea kundini juhudi ambazo zilifanywa na ZK Zadio Congolo akishirikiana na tajiri mwingine lakini mpela alisema kuwa kwa sasa hawezi kwa kuwa anamipango yake ambayo bado hajaikamilisha pindi ikikamilika basi ataufikiria huo mpango.

Alain Mpela ni moja ya mapigo makubwa sana kwa JB Mpiana kwani alikuwa ana wapenzi wengi sana lichaya ukweli kuwa ana sauti nzuri na tamu.

Weekend njema waungwana.

Advertisements

4 Responses to Mortel Combat toka kwa Mpela Brothers

  1. paul samara says:

    mimi nadhan kuwa allan mpela alifanya a grave mistake kuondoka BCBG YA JB MPIANA kwa sababu tangu ameondoka hajawahi kufanya kitu kinachoonekana na kueleweka. angebaki na mpiana nadhan safari yake ya music ingeendelea vizuri bila shida,nachokiona sasa hivi huyu bwana atakuja kupotea kabisa kwenye ramani ya music kama walivyopotea vijana wengine waliowakimbia wakubwa wao kwenda kuanzisha bendi zao,suala hili la kutaka kujitegemea linaenda na charisma au lucky. fere na fally walikua na charisma na bahati,lakini haina maana kila mtu akijitoa kundini na kwenda kujitegemea atafanikiwa.ni suala la nyota ya mtu.

  2. Appreciating the hard work you put into your site and in depth information you offer. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed material. Excellent read! I’ve saved your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

  3. What I have generally told people is that while looking for a good on the net electronics store, there are a few aspects that you have to take into account. First and foremost, you want to make sure to locate a reputable as well as reliable retail store that has gotten great evaluations and scores from other customers and industry experts. This will make sure that you are dealing with a well-known store that can offer good services and support to their patrons. Many thanks for sharing your notions on this site.

  4. Sales Leads says:

    Hi there! This is my first visit to your blog! We are a team of volunteers and starting a new initiative in a community in the same niche. Your blog provided us valuable information to work on. You have done a wonderful job!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: