Ferre na matatizo ya mke na mume.

Na Hadji Le Geebeenique

FERRE GOLA akimuenzi Mzee FRANCO LUAMBO LUANZO MAKIADI kwa kusema..

1:Matata ya moasi na mobali (matatizo ya mke na mume)

2:Bina nangai na respect (cheza na mimi kwa adabu/ heshima)

angalia vizuri kuanzia dakika ya 7:00,kuna wazee wetu naona ferre aliwakumbusha enzi zao wanamwaga bonge la show in steps & style…..hizi nyimbo mbili zilipigwa kwa mara ya kwanza na mzee Franco na kuitikisa Africa nzima,wimbo wa pili(Bina na Ngai na Respect) uliigwa na bendi moja ya Tanzania nadhani marquis ama orchestra safari sound -oss,mzee kitime anaweza kunisaidia manake sikumbuki sawasawa cuz mimi ni kijana wa leo sio wa zamani but napenda muziki wote tu, lakini wao waliubadilisha kwa kuuimba kwa kiswahili maneno yao ya kiswahili nayakumbuka machache wanasema….

“Mara ya kwanza umeniomba tucheze,
Muziki wa kwetu siwezi kukataa,
Mara ya pili ukarudia tena,
Sio kwa kucheza ila kunifinyia jicho,…
Uliza kwanza, kabla ya kufanya upuuzi wako bwana eeh, mimi nimeishaolewa…
..nimekuja kucheza ..nimekuja kufurahisha mwili wangu bwana weee mimi ni muke wa mutu
..na mume wangu yupo hapa hapaa ..ameniruhusu kucheza muziki wa kwetu
..tafadhali bwana duku duku ni wasiwasi wao jamanii eehe mziki wetu unatia fora
..wasiwasi wao ..sisi wao baridi kwetu

Advertisements

8 Responses to Ferre na matatizo ya mke na mume.

 1. Shaibu Mwambungu says:

  Wimbo huo ulimbwa na bendi ya OSS orchestre safari sound Chini ya almarehem Ndala Kasheba Freddy -Shaibu Mwambungu Mbinga Ruvuma

  • mwalimu mkumbe,muheza,tanga. says:

   kweli kabisa waliimba OSS wakitumia mtindo wa duku duku ila sikuwahi kujua kwamba waliucopy wimbo wote kama ulivyo kutoka TP OK JAZZ asante sana sports starehe kwa taarifa hizi,kweli hapa ni kisima cha info zote za muziki hata wa vijana wa zamani mi nilidhani ni kwa kitime tu kumbe na sisi tumo

   • Stivin says:

    Nyimbo nyingi za Tanzania zamani zilikopiwa Kongo, kati ya hizo nipamoja na “Nataka nipate lau nafasi” umekopiwa neno kwa neno mpaka vyombo!

 2. Hadj le Jbnique says:

  Hii ndio original version ya BINA NA NGAI NA RESPECT live ukiangalia vizuri utamuona madilu hapo katika wenye mashati mekundu……Mzee Franco na gitaa lake pembeni..

 3. mzee mataka says:

  Vijana sasa naona mnaanza kutukumbuka na sisi,asanteni sana.Bina na ngai unaweza kuisikiliza vizuri zaidi hapa ikiwa ndio waliorekodi studio.

 4. Anonymous says:

  Ni kweli kwamba FRANCO alikufa kwa ukimwi?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: