Acheni WATA aitwe WATA…..

Huyu ni kijana Heritier Watanabe a.k.a.”Wata ya Ngiama”,hii ndio roho ya Wenge Maison Mere ambae katikati ya mwaka jana 2011 kulizuka taarifa za yeye kujiengue kundini humu,hata hivyo shukrani za kipekee kwa Le ROI DE LA FORRET WERRASON na timu yake kufanikiwa kumbakisha kijana kundini,kiukweli mchango wako ndani ya bendi bado unahitajika huku akiwa ni kipenzi cha Bana Zamba wote,kuthibitisha mahaba ya bana zamba kwa kijana tazama video hii mwanzo mwisho uone kiasi cha pesa mchanganyika akizotunzwa siku hii na Bana Zamba(mashabiki wa Wmmm)huku pia kila mtu akitaka kupiga picha na “Wata ya Ngiama”

Pia sikiliza big soung good music arrangement ya kwake mkaanga chips fundi Pappy Kakol,mimi Hadj Le Jbnique I declare interest mimi ni mshabiki wa Jb mpiana na bcbg wa maisha lakini i luv this video kwa kuwa mimi ni mtu muziki pia,maana nimekirekodi kipande hiki cha hii live iliyofanyika Kinshasa Le Grand Hotel kwenye cd nasikiliza mpaka nimekariri hatua kwa hatua mpaka maneno na majina ya ma PDG wanarushwa hapo jukwaani…….msikilizeni mtoto Wata anavyolia na mzee mzima Werra akichombeza kimtindo na sauti yake nzito…

17 Responses to Acheni WATA aitwe WATA…..

 1. Abdallah J. says:

  Watu wa JB mkamzushia kuwa jamaa ametoka si kweli bwana Wata aliomba ruhusa kutoa albamu yake na iko tayari ila Werason alimwambia asubiri na huwa anazipiga single zake na kwa sasa single moja inapigwa sana redioni na inamfanya Wera kuogopa, Huyu hawezi kuondoka anashikiliwa na analipwa vizuri sana.
  Wata ana mkataba mpaka 2017 ndio unaisha wa kufanya kazi na WMMM.

 2. Hadj le Jbnique says:

  Heritier Wata “analia” hapa…

  • mwalimu mkumbe,muheza,tanga. says:

   Lol…ndio maana jb amemsifia huyu mtoto wa kwa huu wimbo leo ndio nimeufuatilia baada ya kusoma pale ulioandika juzi kwamba jb alipoenda hospitali kumjulia hali werrason alipopata ajali aliongea na Heritier na kumpa big up kwa huu wimbo,kweli kijana hapa alifanya kazi na hii ni changamoto kwa watoto wa mpiana kina Nono Fuji na Abraham Mignon kukunwa vichwa.

   thanx wata for this song.

 3. Mamaa Prezident a.k.a. Mwasi ya mokonzi says:

  combination ya werra na wata imekubali sana jinsi wanavyobadilishana na kujibazana kwa sauti zao ni burudani tosha.

 4. Stivin says:

  Werra ni mpishi wa wana! Msimsahau Deplic

  • Anonymous says:

   anatumia uchawi ndio mana watoto wana vipaji wakiondoka na vipaji vyao wanashindwa kutoka,kwanini?aliwaroga marquis de maison mere wakapaganyika kisa walikua wanatishia uhai wake ,ferre kaweza kwa kuwa amesaidiwa sana kiuchawi na kina king kester na jean marie paul ambao ndio walimsaidia pia werrason akaweza kuwafunika kina adolphe na kutwa bendi yao kuwa yake.

   • Stivin says:

    Ya Mpiana ndio misukule, itoke iende wapi, ushaona misukule inatoka?

   • Anonymous says:

    Kuna kitu mnachanganya kwa kutojua nadhani,bcbg sio bendi tu ile ni organisation iliyo stable kwa kuwa imeuza hisa zake kwa wanamuziki,sasa ulishawahi kuona mtu anahama kampuni yake?

 5. Hadj le Jbnique says:

  WENGE MAISON MERE NI KAMA ARSENAL INARECRUIT VIJANA INAWAKUZA THEN WANAONDOKA KUFUATA MALISHO BORA….THATS WHY BENDI KILA WAKATI INAKUA HAIKO STABLE

  WENGE BCBG NI MANCHESTER UNITED,HAFUNDISHWI MUZIKI PALE,KILA ANAEKUJA ANAJUA,SO ANAKUJA KUPIGA KAZI,NDIO MANA MNAONA BENDI IKO STABLE

  HIYO NDIO TOFAUTI YETU

  • Stivin says:

   Hahaha! Hao watoto wa Maison Mere huwa wanapewa nyimbo nzuri kuimba na Werra Halafu wanajiona wako juu! Wa BCBG nyimbo zote nzuri anaimba na Hapendi vijana wamfunike!

   • Hadj le Jbnique says:

    kwani kwenye sayons serieux kama kweli wewe mtu wa muziki sio wa werrason jb katunga nyimbo ngapi?

    Na kwenye malewa werra katunga nyimbo ngapi?

 6. Hadj le Jbnique says:

  mchezaji mpya wa arsenal…wmmm

  • Stivin says:

   Hadji una mambo wewe, nakwambia kama ni soccer Maison Merre ni Barcelona, Full vipaji! BCBG sawa na AC Millan, full wazee!

 7. RICHARD MALEWA says:

  Sasa bendi gani ina mafanikio kati ya Werra na JB Mpiana?

  Hivi kutetereka bendi ni kuondoka kwa members wa Bendi au Kutoa Albamu ambazo haziuziki na kupendwa na watu?

  Albamu gani ya WMMM imewahi flop kama za JB Mpiana?

  Kuondoka kwa wanamuziki na kuingia kwa wanamuziki inaonyesha kuwa ni ukomavu wa uongozi na umadhubuti wa ujasiriamali!

  Sikio haliwezi kuzidi kichwa! ukiwa WMMM wewe ni simply mfanyakazi wa bendi na siyo Partner kama hauwezani na terms za WMMM nenda kaanzishe ya Kwako!

  Na wengi wamefanikiwa kwa hilo kwa sababu walijifunza ujasiriamali wa Werrason na wameanzisha za kwao! Angalia Bill Clinton, Ferre Gora, Kapaya, Celeo, JT, Aimelia Demingongo, La Coste, na Mzee Mzima Adolph domininguez naye alivyoambiwa amka na uanzishe Wenge Tonya Tonya.

  Hivyo Ukoo wa wana WMMM unazidi kuongezeka na ipo siku watakuja kumkumbuka Le Roy De Forret kwa kuwawezesha kuweza kujitegemea! Hivi ukoo wa wana Wenge BCBG nani ametoka kama siyo jamaa kawatia upofu mpaka wanakuwa ni mizigo na kula kulala!

  Kampuni bora hailei magoi-goi as simple as such!

  Wewe ulisikia lini eti Werrason kauza Mwanamuziki kwenda kwa Koffi? Usifananishe biashara ya Muziki na Mpira bwana!

  • Stivin says:

   Baelezee, juzi kwenye post nyingine niliwatumia link ya Malewa youtube ikiwa imetembelewa na watu 1,450,000 nikawaambia waweke ya JB hata yenye watu milioni moja wamechemsha!

   • mchambuzi wa muziki says:

    Hata wanaume TMK walikua na mashabiki wengi wafuata mkumbo hasa watu wa uswahilini kutokana na hasira tu ama stresses za kimaisha unajikuta unawachukia watu amabo unadhani tu kwamba wanakuzidi kimaisha,hivyo watoto wa uswahili wote amabo ndio huwa wengi siku zote wakajiona wako connected zaidi na wana TMK kuliko EAST COAST TEAM watoto wa upanga,na kuamua kuwapa sapoti kwa lolote hata la ovyo TMK WANAUME.

    Nikuulize in reality TMK WANAUME walikua wanaimba vizuri kuliko EAST COST TEAM????

    Hali ndio hiyo kwa WERRASON na bendi yake,mashabiki wake wengi ni watu wa kawaida wa kipato cha chini na ndio wenye muda wa kushughulika na ushabiki wakilala wakiamka wanawaza ushabiki kwa lengo la kuwakomoa washabiki wa JB ama KOFFI ambao wengi ni watu wenye uwezo ama shughuli zinazoeleweka.

    Hata leo bendi yeyote hapa bongo itakayoshindana na msondo itashindwa vibaya sana,kwa kuwa msondo ni bendi ya watu wa kawaida ambao ndio wengi.

 8. I definitely appreciate each minor little bit of it and I’ve you bookmarked to check out out new things of the blog a must study web site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: